Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Hakuna hata moja lililo la kweli! wee mwandishi mzuri sana wa michezo ya kjuigiza pengine Kanumba na Ray watakuhitaji sana..
 
Zaidi ya haya yote yupo Mungu ambaye hana upendeleo....amesikia kilio cha wanyonge....hakuna fisadi atakaye kanyaga ikulu ya Tanzania tena; kama kati yao kuna atakaye mrudisha Yesu katika kaburi lile ambalo likowazi leo na watalii wanenda kulishuhudia basi na asimame anyanue mguu kuelekea huko tuone alivyo na nguvu!

Mkuu kwani hao mafisadi walioingia sasa Mungu alikuwa likizo..!!!!, tuache kumsingizia Mungu..., ni binadamu ambae ataondoa huu wizi kwa njia ya Kura (au vinginevyo) na kuhakikisha kwamba Tume ya Uchaguzi inafanya kazi yake..

Au umesahau ya Kaisari muachie Kaisari....!!!!, watu wanahongwa na Tshirt alafu unadhani Mungu atampiga radi Fisadi..., (kwa mawazo haya tutaendelea hivi mpaka siku tunaamka na kugundua kwamba hata sisi wananchi tumeshauzwa na ni watumwa wa mtu fulani) 🙁
 
Kwa nani?

Nafikiri unafaa sana kutengeneza maneno ya propaganda..

Kama inauzwa si mkanunue nyie

Mkuu mbona ipo wazi kabisa hii zile mali ambazo Mzee wetu alisema tuzikalie mpaka tutakapopata akili (tunazigawa kama pipi); sehemu nzuri na zenye rutuba wanapewa watu kwa jina la uwekezaji (na wananchi inabidi waende mbali zaidi kuwapisha hawa jamaa..) mhh what about Loliondo..??

Au kuuzwa maana yake ni nini..?
 
Mkuu kwani hao mafisadi walioingia sasa Mungu alikuwa likizo..!!!!, tuache kumsingizia Mungu..., ni binadamu ambae ataondoa huu wizi kwa njia ya Kura (au vinginevyo) na kuhakikisha kwamba Tume ya Uchaguzi inafanya kazi yake..

Au umesahau ya Kaisari muachie Kaisari....!!!!, watu wanahongwa na Tshirt alafu unadhani Mungu atampiga radi Fisadi..., (kwa mawazo haya tutaendelea hivi mpaka siku tunaamka na kugundua kwamba hata sisi wananchi tumeshauzwa na ni watumwa wa mtu fulani) 🙁

Kwahiyo kama wanahongwa tufanyeje tukae tukilia kwamba watu wanahongwa? Atleast mm nimechukua hatua ya kuwapiga radi ya mungu hao mafisadi wewe mwenzangu unafanya nini?
 
Mkuu mbona ipo wazi kabisa hii zile mali ambazo Mzee wetu alisema tuzikalie mpaka tutakapopata akili (tunazigawa kama pipi); sehemu nzuri na zenye rutuba wanapewa watu kwa jina la uwekezaji (na wananchi inabidi waende mbali zaidi kuwapisha hawa jamaa..) mhh what about Loliondo..??

Au kuuzwa maana yake ni nini..?

Sasa nyie si muwe wawekezaji kwenye hayo maeneo ikiwemo loliondo?

Ungekuja hapa unasema sisi tulitaka kununua wakakataa tungekuwa pamoja mkuu
 
Sasa nyie si muwe wawekezaji kwenye hayo maeneo ikiwemo loliondo?

Ungekuja hapa unasema sisi tulitaka kununua wakakataa tungekuwa pamoja mkuu

Mimi na Mzee wangu visionary Mwalimu Nyerere tuliona kwamba hii mali ibaki kuwa ya jamii na sio mtu binafsi..... Au haujaona kelele zangu za chura mkuu cheki hapo; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/181622-turudi-kwenye-ujamaa-at-least-kwenye-kilimo.html#post2636546

Au wewe unaona mambo yanavyokwenda sasa ni poa tu ??
 
Masikini mwandosya inaonekana ugonjwa wake.., ni kutokana na mchezo mchafu wa siasa.
 
Kwahiyo kama wanahongwa tufanyeje tukae tukilia kwamba watu wanahongwa? Atleast mm nimechukua hatua ya kuwapiga radi ya mungu hao mafisadi wewe mwenzangu unafanya nini?

Point yangu ni kwamba hivi vita sio vya mtu mmoja wala sio vya kutegemea miujiza..., hio radi unaipa muda gani ujue kama inafanya au haifanyi kazi na unajuaje hizo akili alizokupa Mungu sio radi kwamba wewe uzitumie...?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
....Hatukukutana barabarani.

Naona like-Minded factions za ndani ya CCM zitakapoona hili dirisha ndogo na la pekee kutokea na wakawa wa kwanza kukishawishi CHADEMA na kujiunga mle bila ajizi na kukubali tu kujichukulia viti vya kwaida tu ndani ya chama, ni kundi hilo la kwanza ndilo litakalokua salama na kuibuka washindi mwisho wa siku.

Turufu za siasa chafu nchini iko mikononi mwao CHADEMA hadi miaka kesho kutwa huko.

wakati mwingine unaweza kuamini kabisa kuwa TZ imefikia kama Sicily Italia enzi hizo... rejea masimulizi ya Mario Puzzo
 
.......... Again, don't drag our beloved President into this suicidal plot because we know our preseident more than what you think we know.........

........ They have confirmed that these are dirty people who cannot be trusted with any junior position in the service of this country. .......!

Mbopo, I surmise that you know better than that. I also presume that you are being cynical and a bit satirical in your posting.

Otherwise, I would be utterly dismayed by your understanding. Not that it matters much, anyway.
 
Point yangu ni kwamba hivi vita sio vya mtu mmoja wala sio vya kutegemea miujiza..., hio radi unaipa muda gani ujue kama inafanya au haifanyi kazi na unajuaje hizo akili alizokupa Mungu sio radi kwamba wewe uzitumie...?

Tuko pamoja mkuu...nyumba nzuri lazima iwe na designer kuanzia architecture; structural engineer mpaka mafundi (Manual) wa zege; mabomba; umeme na rangi. Tatizo lako unawaamini tu hao waweka zege; umeme; maji na wapaka rangi lakini ma designer kwasababu hujawahi kuwaona site huamini kama wapo hata kama unaambiwa wapo; hii ni kwa logic tu tulizokuzwa nazo....

Sasa nikikwambia kuwa mimi ndiyo architecture mwenyewe wa mambo yote katika ulimwengu wa roho utaamini? Kama huniamini mimi angalau jenga imani kwa kuoanisha maneno yangu na kinachoendelea kutokea...kitakachotokea in the future zaidi ya hapo sina chakukusaidia zaidi ya kukopa ID ya mtu; kama huamini acha!
 
Mkuu sasa wewe architecture ulikuwa wapi wakati hili jengo la sasa linajengwa...!!? na lile la Kesho ambalo linajengwa sasa hivi....!!?? au ulipitiwa usingizi basi anza kufanya kazi ili Jengo la Kesho liwe bora kuliko la leo..
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu Hutaki Unaacha, umesomeka hadi hapo.

Taarifa hizo zikiunganishwa na zile tayari kibindoni, mambo si ndio hayo????????? ... an ultimate and MOST shivering permanent sln is on the way from the West-Coast an shall strike very hard indeed; smarshing a number of CCM underworld warlords.

Whereas it is known of EL's disguise into the new sacred quarters today for the worst on his back, RA's is latest move is a desparation of the highest order just as much as the current tenants at the beach-house. And the clues continue anyway.

And the sun shall be seen from the East again.

Mh waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hajamfahamu adui yake no 1. Hii inatokana na ukweli kuwa vita anayopigana inamhusisha yeye na adui asiowajua. Membe anaamini adui zake wakubwa ni Rostam na Edward.Amepotoka.

Membe napenda nikufahamishe ya kuwa, usipoangalia, yatakupata makubwa zaidi ya yale yaliyompata Harrison. Unapigana na watu hatari na wanaotumia akili nyingi sana kwenye game hili la siasa.

Katika baraza la kwanza la JK uliteuliwa kuwa deputy wa home affairs. Ulilalamika sana kwa JK. SMS ya kulalamika kwako uliyomtumia JK, iliwafikia Rostam na Edward at the same time bila wewe kufahamu. Tafakari kwanza!

Richmond haijaletwa na Rostam wala Edward nchini. Wewe unafahamu vyema jinsi JK alivyocheza dili la Richmond kishamba akishirikiana na Gire baada ya mazungumzo yao huko U.S. Baada ya mambo kuharibika ndipo rostam na edward wakashirikishwa. Unafahamu vizuri role aliyoicheza rostam kuhakikisha angalau dowans inazaliwa ili kumwokoa JK.Ya lowassa kujiuzulu unayafahamu vizuri sana sitaki kuyazungumzia kwa sasa.

Sitta hakuwahi kuwa rafiki wa Harrison hata siku moja. Alimtumia tu ili kutimiza malengo yake ya kumwondoa Lowassa kwenye nafasi yake. Wewe ndiye uliyekuwa ukiwachonganisha mara kwa mara JK na PM wake Lowassa. Hata nafasi ya nje uliipata kwa jungu kubwa na la ustadi wa hali ya juu ulilochezewa na vijana wawili wa usalama wa taifa kwa kumchafua Lowassa. JK akaanza kukuamini.Ulicheza vizuri karata kwani ulijua fika jinsi gani sitta alivyomchukia rostam na Lowassa kwa yale waliyomtendea ili asiwe PM na kwa ustadi wa hali ya juu ukamshawishi sitta alitumie bunge ili kumwadhibu lowassa.

Mwakyembe ana ugomvi wa siku nyingi na rostam hata kabla ya JK kuwa rais. Alitumia nafasi hiyo kumnyonga Lowassa na rafiki yake Rostam na kwa bahati mbaya akakiri ndani ya bunge kuwa kuna machafu mengi yameachwa ili kunusuru heshima ya serikali. Kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na mtu aliyepitia idara ya usalama wa taifa. Unafahamu vyema kuwa hili kosa ndilo linalomgharimu Harrison huko Appollo. Baada ya Lowassa kuangushwa, ulikumbatiana na Mwakyembe, Rais akawapongeza, mkafurahi, mkabweteka na kumwamini JK. Kosa la pili kubwa.

Kwa bahati mbaya sana ukaungana na Mwakyembe, Mengi, Sitta, na wafuasi wake kwa ajili ya kuutafuta urais tena kwa kumtumia mwanaye Ridhiwani. Hili ni kosa la tatu kubwa kwani ulichanganya kwenye kundi lako watu wasio marafiki wa JK ambao kwa hakika wata-demand umburuze JK mahakamani pindi utakapokuwa rais.

Rostam-JK-lowassa

1. Hawa ni marafiki wakubwa ambao licha ya wawili kuwa nje ya serikali lakini wote watatu wanaendesha serikali na hawasiti 'kuwanyamazisha'' wabaya wao wanaogusa interest zao.Individually wanatofautiana ila wakiwa watatu ni wamoja.Membe naomba ufahamu hili.
2. Wewe ulimtaka sitta awe spika kwa mara nyingine tena. JK alimtaka sitta pia lakini katika kikao cha watatu akakubaliana na pendekezo ingawa kwa shingo upande la Anne kuwa spika.
3. JK atakuwa safe kama lowassa akiwa rais.Hatakuwa safe endapo mmoja wenu atakuwa rais.Anafahamu hili fika.
4. Richmond itarudi bungeni kabla ya 2015.Wakati wa kujadili, wewe na mwakyembe mko tayari kusema ukweli.Ili kuwazima, mwakyembe 'ataondoka' then wewe waweza kufuata!.Haya yatafanywa na umoja wa hawa watatu na si individually
5. Ndani ya CC iliyopita zilipigwa kura za siri ili kumfukuza Lowassa uanachama.Kati ya wajumbe 32, 19 walimsupport lowassa na 13 kwa JK!.Hapa wanaonekana ni wapinzani ingawa wakiwa watatu ni wamoja.
6. JK anaweza kukusikiliza na kujifanya mko pamoja naye. Lengo ni kutaka kujua what's going on in your group ili wawamalize vizuri.
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe makamu wa rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe
:

Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first. Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu sasa wewe architecture ulikuwa wapi wakati hili jengo la sasa linajengwa...!!? na lile la Kesho ambalo linajengwa sasa hivi....!!?? au ulipitiwa usingizi basi anza kufanya kazi ili Jengo la Kesho liwe bora kuliko la leo..

Nilikuwa sijazaliwa!
 
duh!! Nimechanganyikiwa sielewi kinachoendelea kumbe nchi hii yetu ya AMANI NA UTULIVU imekuwa hivi ya fujo, uonevu na mauaji ya kutisha yanayofanywa na wanaoitwa viongozi wa chama na serikali!!!!!!!!! Kweli Tanzania ni zaidi uijuavyo!!!!
 
Back
Top Bottom