Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Mh waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hajamfahamu adui yake no 1. Hii inatokana na ukweli kuwa vita anayopigana inamhusisha yeye na adui asiowajua. Membe anaamini adui zake wakubwa ni Rostam na Edward.Amepotoka.

Membe napenda nikufahamishe ya kuwa, usipoangalia, yatakupata makubwa zaidi ya yale yaliyompata Harrison. Unapigana na watu hatari na wanaotumia akili nyingi sana kwenye game hili la siasa.

Katika baraza la kwanza la JK uliteuliwa kuwa deputy wa home affairs. Ulilalamika sana kwa JK. SMS ya kulalamika kwako uliyomtumia JK, iliwafikia Rostam na Edward at the same time bila wewe kufahamu. Tafakari kwanza!

Richmond haijaletwa na Rostam wala Edward nchini. Wewe unafahamu vyema jinsi JK alivyocheza dili la Richmond kishamba akishirikiana na Gire baada ya mazungumzo yao huko U.S. Baada ya mambo kuharibika ndipo Rostam na Edward wakashirikishwa. Unafahamu vizuri role aliyoicheza rostam kuhakikisha angalau dowans inazaliwa ili kumwokoa JK. Ya lowassa kujiuzulu unayafahamu vizuri sana sitaki kuyazungumzia kwa sasa.

Sitta hakuwahi kuwa rafiki wa Harrison hata siku moja. Alimtumia tu ili kutimiza malengo yake ya kumwondoa Lowassa kwenye nafasi yake. Wewe ndiye uliyekuwa ukiwachonganisha mara kwa mara JK na PM wake Lowassa. Hata nafasi ya nje uliipata kwa jungu kubwa na la ustadi wa hali ya juu ulilochezewa na vijana wawili wa usalama wa taifa kwa kumchafua Lowassa. JK akaanza kukuamini. Ulicheza vizuri karata kwani ulijua fika jinsi gani sitta alivyomchukia Rostam na Lowassa kwa yale waliyomtendea ili asiwe PM na kwa ustadi wa hali ya juu ukamshawishi Sitta alitumie bunge ili kumwadhibu Lowassa.

Mwakyembe ana ugomvi wa siku nyingi na Rostam hata kabla ya JK kuwa rais. Alitumia nafasi hiyo kumnyonga Lowassa na rafiki yake Rostam na kwa bahati mbaya akakiri ndani ya bunge kuwa kuna machafu mengi yameachwa ili kunusuru heshima ya serikali. Kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na mtu aliyepitia idara ya usalama wa taifa. Unafahamu vyema kuwa hili kosa ndilo linalomgharimu Harrison huko Appollo. Baada ya Lowassa kuangushwa, ulikumbatiana na Mwakyembe, Rais akawapongeza, mkafurahi, mkabweteka na kumwamini JK. Kosa la pili kubwa.

Kwa bahati mbaya sana ukaungana na Mwakyembe, Mengi, Sitta, na wafuasi wake kwa ajili ya kuutafuta urais tena kwa kumtumia mwanaye Ridhiwani. Hili ni kosa la tatu kubwa kwani ulichanganya kwenye kundi lako watu wasio marafiki wa JK ambao kwa hakika wata-demand umburuze JK mahakamani pindi utakapokuwa rais.

Rostam-JK-Lowassa

1. Hawa ni marafiki wakubwa ambao licha ya wawili kuwa nje ya serikali lakini wote watatu wanaendesha serikali na hawasiti 'kuwanyamazisha'' wabaya wao wanaogusa interest zao. Individually wanatofautiana ila wakiwa watatu ni wamoja. Membe naomba ufahamu hili.
2. Wewe ulimtaka Sitta awe spika kwa mara nyingine tena. JK alimtaka Sitta pia lakini katika kikao cha watatu akakubaliana na pendekezo ingawa kwa shingo upande la Anne kuwa spika.
3. JK atakuwa safe kama Lowassa akiwa rais. Hatakuwa safe endapo mmoja wenu atakuwa rais. Anafahamu hili fika.
4. Richmond itarudi bungeni kabla ya 2015. Wakati wa kujadili, wewe na Mwakyembe mko tayari kusema ukweli. Ili kuwazima, Mwakyembe 'ataondoka' then wewe waweza kufuata!.Haya yatafanywa na umoja wa hawa watatu na si individually
5. Ndani ya CC iliyopita zilipigwa kura za siri ili kumfukuza Lowassa uanachama. Kati ya wajumbe 32, 19 walimsupport Lowassa na 13 kwa JK!.Hapa wanaonekana ni wapinzani ingawa wakiwa watatu ni wamoja.
6. JK anaweza kukusikiliza na kujifanya mko pamoja naye. Lengo ni kutaka kujua what's going on in your group ili wawamalize vizuri.
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe makamu wa rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako Chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na Rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe:

Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first. Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person
Wakati wa dhahabu wa JF.
 
Nina swali kwako tofauti na hii mada jadiliwa hapa, ningeomba nikuulize kama utaamua kuindikia makala mara baada ya kuichanganua ni sawa au kama utaona vipi ianzishie uzi tu! Vipi naweza kukuuliza?
Uliza tuu chochote, mimi niko very reachable
P
 
nina swali, hivi ni kwa nini kati ya wanaotwaliwa Christians wako overrepresented? i mean, wote ni Christians je, hii ime/inatokea tu au vita against the so called "mfumo Kristo" ?

war on Christianity is real ...

Inafikirisha sana.
 
Uliza tuu chochote, mimi niko very reachable
P
Mtazamo wangu.
Tumefundishwa kuhusu Ubepari na Ujamaa! lakini tuliaminishwa kama ujamaa ni mbaya haufai huko mashuleni mwetu.

Nchi yetu ya Tanzania licha ya kuwa Katiba yetu inaita nchi kuwa ya kujamaa na kujitegemea lakini tumebahatika kupata Marais 6 mpaka sasa ambao kwa mchanganuo wangu na milengo yao ya kisiasa iko hivi.

1. Mwal Nyerere - Mjamaa
2. Mwinyi _ Mrengo wa Kibepari
3. Mkapa - Mrengo wa Kibepari
4. Kikwete- Mrengo wa Kibepari
5. JPM - Mrengo wa Kijamaa
6. Samia Mrengo wa Kibepari

Nikiwatathimini Marais wetu katika makundi haya mawili ya kibepari na Kijama naona kabisa kama waliokuwa na mrengo wa Kijamaa walikuwa na uzalendo mkubwa na Taifa lao la Tanznaia kuliko wenye mrengo wa Kibepari, wenye mrengo wa kibepari ni kama ni watu wanaotawanya mali za umma sana, wamekumbwa na kashfa nyingi za kifisadi kuanzia kule Loliondo etc.

Binafsi nikitafakari juu ya hii mirengo miwili napata shida sana kuamini kama mrengo wa kijamaa ni bora na thabiti kwa nchi za kiafrica na sababu kuu nikiangalia viongozi wetu na aina za tawala zao. Napata tabu sana kiongozi kuwa mrengo wa ujamaa na kuitwa Dikteta. naomba uchambuzi wako ata kwa kuanzishia uzi juu ya hii imani yangu.

Wasalaam
JF
 
Mh waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hajamfahamu adui yake no 1. Hii inatokana na ukweli kuwa vita anayopigana inamhusisha yeye na adui asiowajua. Membe anaamini adui zake wakubwa ni Rostam na Edward.Amepotoka.

Membe napenda nikufahamishe ya kuwa, usipoangalia, yatakupata makubwa zaidi ya yale yaliyompata Harrison. Unapigana na watu hatari na wanaotumia akili nyingi sana kwenye game hili la siasa.

Katika baraza la kwanza la JK uliteuliwa kuwa deputy wa home affairs. Ulilalamika sana kwa JK. SMS ya kulalamika kwako uliyomtumia JK, iliwafikia Rostam na Edward at the same time bila wewe kufahamu. Tafakari kwanza!

Richmond haijaletwa na Rostam wala Edward nchini. Wewe unafahamu vyema jinsi JK alivyocheza dili la Richmond kishamba akishirikiana na Gire baada ya mazungumzo yao huko U.S. Baada ya mambo kuharibika ndipo Rostam na Edward wakashirikishwa. Unafahamu vizuri role aliyoicheza rostam kuhakikisha angalau dowans inazaliwa ili kumwokoa JK. Ya lowassa kujiuzulu unayafahamu vizuri sana sitaki kuyazungumzia kwa sasa.

Sitta hakuwahi kuwa rafiki wa Harrison hata siku moja. Alimtumia tu ili kutimiza malengo yake ya kumwondoa Lowassa kwenye nafasi yake. Wewe ndiye uliyekuwa ukiwachonganisha mara kwa mara JK na PM wake Lowassa. Hata nafasi ya nje uliipata kwa jungu kubwa na la ustadi wa hali ya juu ulilochezewa na vijana wawili wa usalama wa taifa kwa kumchafua Lowassa. JK akaanza kukuamini. Ulicheza vizuri karata kwani ulijua fika jinsi gani sitta alivyomchukia Rostam na Lowassa kwa yale waliyomtendea ili asiwe PM na kwa ustadi wa hali ya juu ukamshawishi Sitta alitumie bunge ili kumwadhibu Lowassa.

Mwakyembe ana ugomvi wa siku nyingi na Rostam hata kabla ya JK kuwa rais. Alitumia nafasi hiyo kumnyonga Lowassa na rafiki yake Rostam na kwa bahati mbaya akakiri ndani ya bunge kuwa kuna machafu mengi yameachwa ili kunusuru heshima ya serikali. Kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na mtu aliyepitia idara ya usalama wa taifa. Unafahamu vyema kuwa hili kosa ndilo linalomgharimu Harrison huko Appollo. Baada ya Lowassa kuangushwa, ulikumbatiana na Mwakyembe, Rais akawapongeza, mkafurahi, mkabweteka na kumwamini JK. Kosa la pili kubwa.

Kwa bahati mbaya sana ukaungana na Mwakyembe, Mengi, Sitta, na wafuasi wake kwa ajili ya kuutafuta urais tena kwa kumtumia mwanaye Ridhiwani. Hili ni kosa la tatu kubwa kwani ulichanganya kwenye kundi lako watu wasio marafiki wa JK ambao kwa hakika wata-demand umburuze JK mahakamani pindi utakapokuwa rais.

Rostam-JK-Lowassa

1. Hawa ni marafiki wakubwa ambao licha ya wawili kuwa nje ya serikali lakini wote watatu wanaendesha serikali na hawasiti 'kuwanyamazisha'' wabaya wao wanaogusa interest zao. Individually wanatofautiana ila wakiwa watatu ni wamoja. Membe naomba ufahamu hili.
2. Wewe ulimtaka Sitta awe spika kwa mara nyingine tena. JK alimtaka Sitta pia lakini katika kikao cha watatu akakubaliana na pendekezo ingawa kwa shingo upande la Anne kuwa spika.
3. JK atakuwa safe kama Lowassa akiwa rais. Hatakuwa safe endapo mmoja wenu atakuwa rais. Anafahamu hili fika.
4. Richmond itarudi bungeni kabla ya 2015. Wakati wa kujadili, wewe na Mwakyembe mko tayari kusema ukweli. Ili kuwazima, Mwakyembe 'ataondoka' then wewe waweza kufuata!.Haya yatafanywa na umoja wa hawa watatu na si individually
5. Ndani ya CC iliyopita zilipigwa kura za siri ili kumfukuza Lowassa uanachama. Kati ya wajumbe 32, 19 walimsupport Lowassa na 13 kwa JK!.Hapa wanaonekana ni wapinzani ingawa wakiwa watatu ni wamoja.
6. JK anaweza kukusikiliza na kujifanya mko pamoja naye. Lengo ni kutaka kujua what's going on in your group ili wawamalize vizuri.
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe makamu wa rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako Chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na Rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe:

Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first. Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person
Rostam ni mtu powerful zaidi nchini, Viongozi wakubwa tunaowaona nyuma yao yupo yeye, Ana connections nzito sana kimataifa, Anatajwa kuwa miongoni mwa watu wenye utajiri mkubwa zaidi nchini,

Hata hivyo, wengi pia wanasema kuwa hapendi kelele kabisa, hupenda kufanya mambo yake kimya bila attention.

Kuna Ukweli wowote ?
Karibu
P
 
Membe alikufa kifo cha kawaida? Kwa haya yanayoendelea nchi sasa hivi, naanza kuelewa aliyenzisha hii thread alikuwa na maana gani. Mkwere mkwere mkwere....
Kwasasa Bundi katua Zanzibar!
Mume,make wa marehemu!

Hai wawili tunaweza kuwachukulia wa kawaida lakini inawezekana ni Moja ya watu waliokua wanasikilizwa sana na mwenyekiti wa sasa tena labda aliwaamini mno kuliko tunavyodhani!!

Ngoja tusubiri bundi akitua huku atatua Kwa nani!!
 
wakati mwingine unaweza kuamini kabisa kuwa TZ imefikia kama Sicily Italia enzi hizo... rejea masimulizi ya Mario Puzzo

Itafika siku hao wote watang'olewa na Haki. Haki ni kwa wote wache wale tu lakini ikifika siku watapumzika huko kula, kwao kutakwisha na Wanyonge watapata kupumua eeeh Mwenyeezi Mungu inusuru Nchi yetu na utupatie viongozi wanaoipenda Nchi yao pamoja na Sisi walala hoi amina.
Mkwere bado anarun show tu na sasa yeye ndio kashika remote, mtaangalia channel anayotaka yeye.
 
Halafu ni mdini wa kutupwa na ni katili wa kisirisiri. Kipindi chake alikuwa ana ogopa-ogopa kwa sababu CCM ilikuwa na mwagwiji wengi kama kina Mkapa na hata Membe. Na zaidi alikuwa hajajua kuwa watanzania ni mbulula kiasi gani.... Magufuli alipoingia ndiyo akaonyesha kuwa unaweza kuwafanya lolote na wanakaa kimya tu. Alipopata hii chance ndiyo ameonyesha rangi zake haswa.
 
Kwasasa Bundi katua Zanzibar!
Mume,make wa marehemu!

Hai wawili tunaweza kuwachukulia wa kawaida lakini inawezekana ni Moja ya watu waliokua wanasikilizwa sana na mwenyekiti wa sasa tena labda aliwaamini mno kuliko tunavyodhani!!

Ngoja tusubiri bundi akitua huku atatua Kwa nani!!
Huyu mama miaka 97 ni natural death, nahisi Kwa Zanzibar, Mzee Amaan ni miongoni mwa washauri wake
 
Back
Top Bottom