Haya mambo ni makubwa, Tuanze kuunganisha dots
Makundi ndani ya CCM (Wanamtandao)
- Lilikuwa likitengenezwa na akina JK, EL, RA S6,.... n.k
Makundi mengine madogo madogo ambayo hayakuwa na nguvu kama lamtandao mf. la Prof. Mwandyosa, Kagoda n.k
Baada ya kuzidiana kete wakati wa kugawana vyeo mtandao ukaparanganyika :
- Mafisadi (wanaotuhumiwa kulihujumu taifa, kwasababu hawa ndio wanaofanya maamuzi serikalini kwa maslahi yao)
Hapa tuna JK, EL, RA, EC na wapambe wadogo wadogo
- Wanaojipambanua kuwa ni makamanda dhidi ya mafisadi(Hawa ni kwa sababu wapo nje ya maamuzi makubwa hivyo kukosa mgao, hawapo tayari kuona upinzani ukiwa na nguvu hata pale inapoonekana wanazungumza lugha moja)
Hapa tunakutana na S6,Dr. Mwakyembe, A.Kilango,O. Sendeka.
NB: Wale waliokuwa wanaliamini kundi hili kuwa ni la wazalendo kama akina Uncle Fred, waliamua kukimbia Chama moja kwa moja pale walipohisi unafiki unanukia kwenye kundi hili. Big up Uncle Fred
Baada ya kupakana matope sana na kukamiana, kundi la mafisadi linaonekana kushindwa nguvu ya hoja, kundi la wanaojiambanua limefanikiwa kuimba ukosi(chorus) ya wananchi wengi , hivyo kupata nguvu ya hoja.
Swali, nini hatima ya kila moja wa hao former wanamtandao?
Ili mafisadi wabaki salama, lazima mwezao awe rais, iwe ni key member wao au mpambe wao. VInginevyo ni jela au kuhama nchi, ingawa kuna Interpol (sijui kama watajificha). Kufanya hivyo lazima watumie mbinu yoyote ile kuwamaliza nguvu wao wanoimba chorus ya wananchi,maana kama wakisimama kugombea Urais au mpambe wao akasimama, basi itawaweka katika hali tete.
Hii ni hatari, maana sasa tunashuhudia mambo yanayoendelea sasa,...anyway ni speculations may be. Ila mi naiita kuunganisha nukta/matukio.
Hii ya Nape na Malisa ni mchezo wa hawa Mafisadi kufanya watu waamini miongoni mwao kuna mfarakano, nidhahiri tunaamini kuwa Nape ni JK, Malisa ni EL. Baadae waje kumuweka mtu ambaye tutafikiri ni Neutral kumbe ni mpambe,...hahaha, hawa jamaa ni game makers kweli, yaani hata hawa Malisa na Nape hawajijui kuwa wanatumiwa na mtu/ watu wamoja.
Ila tu wamesahau kuwa Watanzania wamehamisha mawazo yao kwao, sasa hivi wanacheza nyimbo za CDM, na hapo ndipo patachimbika kama wakijaribu kuwagusa wapiganaji wetu, sisi hatutumii vikao vya siri kuwashughulikia, tunatumia nguvu ya umma,
Umma tukiwakataa, hata mtumie jeshi zima hamtaweza, sana sana jeshi hilo hilo litatusaidia kichinichini na baadae waziwazi.
Ushauri: Kwa wana CCM ambao bado wanao uzalendo kwa nchi hii, mjue madereva wenu wa chama ni ma criminal, wanafanya mambo ambayo yatasababisha kupotea kwa amani, Jiungeni na wazalendo wa kweli ambao ni umma, ukiongozwa na CDM.