Membe Alikoroga CCM, kauli yake ya CHADEMA kushika dola yamponza


Membe aikoroga CCM
• Kauli yake ya kuitabiria ushindi CHADEMA yaibua hofu

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima


KAULI ya hivi karibuni iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ya kuitabiria ushindi na kukitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kijiandae kushika dola mwaka 2015, imewaduza vigogo na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Membe ambaye ni mmoja wa makada wa CCM wanaotajwa kuutaka urais mwaka 2015, alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akiukaribisha msafara wa CHADEMA nyumbani kwake kijijini Rondo na kushiriki nao chakula cha pamoja.

Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zilisema kuwa kauli ya Waziri Membe si tu kwamba imewashangaza vigogo wa CCM, bali pia imetafsiriwa kama ni mmoja wa mawaziri wanaotajwa kutaka kujiunga na CHADEMA hasa baada ya jina lake kutajwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kama mmoja wa mawaziri wanaotarajiwa kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara hivi karibuni uliofanyika mjini Sengerema, Lema aliwataja mawaziri wengine wanaotarajiwa kujiunga na CHADEMA kuwa ni pamoja na Edward Lowassa (Monduli) na Samuel Sitta (Urambo Mashariki). Lowassa na Sitta kwa nyakati tofauti walikanusha madai hayo, lakini Waziri Membe hajawahi kukanusha.

Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Emmanuel Nzungu aliliambia gazeti hili jana kuwa kauli ya Waziri Membe ina utata mkubwa.
"Tumezungumza kwenye vikao vyetu hapa ofisini, tumeona kuna haja ya kuleta hoja hii kwenye vikao vya juu vya chama. Hii si kauli ya utani bali ni kauli iliyopangwa na hatujui kwa sababu gani," alisema Nzungu.

Alisema kibaya zaidi kauli hii imetolewa na Waziri Membe siku chache baada ya Lema kumtaja kuwa mmoja wa mawaziri wanaotajwa kutaka kuhamia CHADEMA.

"Ningesoma kwenye magazeti, ningesema amewekewa maneno mdomoni, lakini nilimwona kwa macho yangu kwenye kituo cha televisheni ya ITV aikimwagia sifa CHADEMA na kuitabiria ushindi. Hii inashangaza sana na lazima kauli yake ijadiliwe kwenye vikao vya chama," alisema Nzungu.

Kada mwingine ambaye ni mjumbe wa NEC aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema kuwa anashangazwa na ukimya wa viongozi wa juu wa CCM kwani hakuna aliyetoa kauli ya kumwonya Waziri Membe.

"Kuna makada wa CCM waliowahi kutoa kauli ndogo tu, lakini chama kilitumia nguvu kuzijibu na kuzitolea ufafanuzi. Hii kauli ya Waziri Membe ya kuitabiria kifo CCM na kuitabiria ushindi CHADEMA si ya kupuuzwa," alisema mjumbe huyo wa NEC toka mkoani Shinyanga.

Hivi karibuni Waziri Membe aliwakaribisha na kufanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA waliotembelea kijijini kwake.

Katika mazungumzo yake na viongozi hao mbele ya waandishi wa habari, Waziri Membe alikitabiria chama hicho kushika dola mwaka 2015 kwa vile kina mvuto kwa Watanzania.

Viongozi waliokaribishwa nyumbani kwa Membe ni pamoja na Lema, James Millya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa kata za Chiponda na Mnara.
Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama na mjumbe wa NEC, aliwatahadharisha wabunge wenzake wa CCM kwamba wako hatarini kung'olewa katika majimbo yao na CHADEMA kwani chama hicho kwa sasa kimeimarika na kukubalika kwa wananchi wengi.

"CHADEMA sasa imegundua udhaifu wao uliokuwa ukisababisha isishinde, zamani mlikuwa mkifanya kampeni mikoani, lakini kitendo cha kufika kata hadi kijiji, hii sasa ndio siasa safi.

"Wapo wengi wanaodhani kuja huku ni kama mmekuja kuwavamia la hasha, siasa ni nguvu ya hoja, haina maana mmekuja kumshughulikia mtu, binafsi najua nguvu ya hoja ndiyo inayoleta maendeleo.

"Pia nguvu ya hoja inasaidia kuleta maendeleo, yaani nguvu ya hoja unaweza kuita ni mgongano au msuguano wa kimawazo ambao unakumbusha uwajibikaji wa chama na serikali.

"Mimi najua maana ya siasa, nimeishi miaka 10 nje ya nchi zenye demokrasia safi, ikiwamo Marekani, pia nimesoma miaka miwili, hivyo kuja kwenu hapa kunaweza kuchukuliwa na wabunge au Watanzania wengine mmekuja kuwaingilia, hapana.

"Mimi naipenda siasa ya demokrasia na nailewa zaidi na ndiyo maana niliposikia mko huko nimesitisha ziara zangu jimboni na natarajia kurudi Dar es Salaam na kusafiri kwenda nje ya nchi," alisema.

Membe alisema katika dunia hii ya tatu, vitu vyote vinabadilika yakiwamo mabadilko ya siasa na kuongeza kwamba, hali ilivyo Tanzania lazima kutakuwapo na mabadiliko ya vyama vya upinzani kushika dola.

"Kuna nchi nyingi zilikuwa na vyama zaidi ya 500 ikiwamo Angola, lakini hadi sasa vimepungua na kufikia 310, sasa tahadhari yangu kwenu CHADEMA hivi sasa mko ‘strong' na mnashika nafasi ya pili, muanze kujiandaa kuunda serikali ingawa bado kuna vita vikali mbele.

"Mnaweza mkajiamini mnaweza kushinda, lakini mwishowe upepo ukageuka, unajua binadamu na mnyama ni vitu vya ajabu sana, vyama vingine vinaweza kutumia rungu hilo hilo kukumaliza," alisema.
Adha, Membe aliwaonywa viongozi kuchukua tahadhari kubwa juu ya serikali ya umoja, huku akitolea mfano nchi za Kenya na Ethiopia.

"Hakuna serikali yoyote ya mseto au ya umoja itakayoleta maendeleo kwa wananchi na sote ni mashahidi wa nchi hizo, mfano Keneth Kaunda chama chake kilikuwa na wafuasi wengi kikashinda na watu wakashangilia, lakini wiki tatu za kwanza walikuwa katika vita vya kuunda serikali.

"Serikali ya mseto ina madeni makubwa, maana kila chama, taasisi mtu ana watu wake wa kutaka kupewa madaraka, mwishowe mnajikuta matatizoni, epukeni misaada ya wafadhili maana waliokusaidia watakugharimu baadaye.

"Hapa kwetu kule Zanzibar wamenusurika kwa kitu kimoja tu, CCM na CUF wameunda Serikali ya Umoja, lakini Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndicho kilichowasaidia.

"Ile serikali ipo chini ya chama mama, chama chenye nguvu na fedha, kina miongozo, kanuni za CCM zinazotekelezeka," alisema.

Alimweleza Lema kwamba alisikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya kumnyang'anya ubunge.
"Lema, sikuamini baada ya maamuzi kutolewa na mahakama, lakini kama umekata rufaa nafikiri huku kutatendeka haki zaidi, bila shaka utarudi bungeni," alisema.

 
Watu wengine bwana, mtu katoa maoni yake lakini mtu mwingine anatokwa na povu sijui anataka kumfunga nani karne hii ya 21!
 
Namsubiri Nape ashuke na kajli ya chama chetu kitukufu juu ya Membe ndo nitasema.
 
CCM bana wako Paranoid kweli..sasa mtu asiongee anachokiamini

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Membe ni mwanasiasa wa ukweli ameona mbali kama mwewe .Nape anaona karibu kama kuku
 
Hamna la kushangaza kwenye hili. Hapa Membe yuko very smart, anatengeneza Plan B yake. Kama Plan A ikifail, ambayo ni JK na CCM wasipompitisha kugombea Uraisi basi ataingia plan B kujiunga na CDM.
Hii aliifanya hata JK mwenyewe 2005, JK alitishia kuhamia CDM akitoswa na CC, Ben akaogopa, ingawa Ben alikuwa hamtaki JK alikuwa anamtaka Salim, lakini ripoti ya TISS ilionesha JK ndo anapendwa na akihama chama naweza kumeguka.

Its same strategy.

asa,nani anampenda membe awe rais wake?
 
Kasema kama mwanademokrasia na anaamini demokrasia kwani mwenye nguvu ya hoja na zinazokubalika na wananchi ndo anachaguliwa.

Hongera Membe kwa ukomavu wa siasa ulionao.

Kama anamaanisha alichokisema basi ameonyesha ukomavu wa kisiasa. Kama mtakumbuka katika uchaguzi uliomuweka Obama madarakani waziri wa zamani wa mambo ya nje ambaye alikuwa republican (Collin Powel) aliweka bayana kuwa anamsupport Obama. Aliweka national interest mbele ya political party interests.
 
Kama anamaanisha alichokisema basi ameonyesha ukomavu wa kisiasa. Kama mtakumbuka katika uchaguzi uliomuweka Obama madarakani waziri wa zamani wa mambo ya nje ambaye alikuwa republican (Collin Powel) aliweka bayana kuwa anamsupport Obama. Aliweka national interest mbele ya political party interests.

Uko sawa mkuu,inahitaji tuangalie sera na hoja za wagombea zaidi ya vyama vya siasa kama ilivyo leo.Ila kwa Tz inatakiwa mabadiliko kwanza then hilo ndo lifuatiye, hii ni kwa sababu bado kimtazamo wa demokrasia uko chini.
 
Katika hali ya kawaida tu na katika mazingira yetu ya kisiasa (kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila maandalizi ya kutosha) yanyopandikiza hisia za kwamba siasa ni Uadui, Bernard Membe ameonyesha ukomavu na ujasiri wa hali ya juu kisiasa kwa kukuwapokea viongozi wa CHADEMA na kutoa maoni yaliyotafsiriwa kama endorsement kwa CHADEMA 2015.Huu ni ukweli ambao mawaziri na makada ndani ya chama chako hawathubutu kuusema

Jambo hili linaweza kukutia matatani ndani ya chama chako kama ilivyo kawaida.Ni viongozi wachache kwenye vyama vya siasa wenye uwezo wa kufanya jambo kama hili.Umewafundisha wenzako kwamba siasa ni itikadi,siasa ni umoja na siasa ni upendo.Jaribu kujenga chama chako,kirekebishe ili kiwe na mawazo ya kidemokrasia kama ya kwako na wengine wachache ikishindikana karibu chadema

Sikushangazwa na hatua yako hii kwani umeishi na kufanya kazi katika nchi zilizokoma kidemokrasia.Pengine taaluma yako ya uhusiano wa kimataifa na Diplomasia ilichangia(hilo halituhusu). Endelea kuikiimarisha chama chako ili kuwe na mchuano mzuri 2015.

What the requires at this very moment is complete overhaul or if you like, restructuring. You can play proper party democracy if the Chama Cha Mapinduzi realises the need to purge itself of the excesses that have undermined it and, through that process, bring back those genuine, committed, credible and patriotic Tanzanians who founded the Party but were hounded out by no ordinary design of their own.

As it is now, the CCM has no discipline, no orientation, there is no grassroots linkage, some kind of disconnect between the party and the people. This culture of substitution of candidates at all levels of elections undermined the level playing field which any electoral process should boast of. The kind of malpractices within the party has created political enmity, internal divisions, cleavages and bad blood among the members and leaders of the party.

The political infrastructure are weak, people of proven integrity have been shown the way out. The way to recover the party from this self-imposed affliction is to seek genuine reconciliation of all aggrieved persons, irrespective of status, to properly reposition the party.

As it stands today, CCM is the problem of Tanzania.There is need for attitudinal change, proper re-orientation and restructuring. There are many credible people out there who wish to return to CCM fold but the present reality is not motivating them to do so.

Jenga chama chako ikishindikana karibu CHADEMA !!!
 
Hakuna kitu hapo cha kumpongeza Membe maana ule ni unafiki tu, kwan kuna tofauti gani kati ya membe na shibuda? Inamana unataka kutuaminisha kuwa hata na Shibuda naye ni shujaa maana vitendo vinafanana na Membe, kama yy ni gamba inabidi afanye yale yanayokubaliana na wenzake , tatizo wana CDM wengi huwa tinatukuza mambo ya kijinga kama haya alfu yakitugeukia na ss tunaanza kulalama, tabia za undimilakuwili kama huu ndio ulinifanya niondoe iman na viongzoi wangu wa CDM kama Zitto kabwe, Shibuda, Yule makamu wa Bavicha, koz sipendi unafiki na wanafiki na ni lazima tuwe tunawasema hadharan pasipo kuogopa ili nao wajijue.
UNAFIKI NDIO ULIMPONZA YUDA KUMSALITI YESU.
 
He did nice and he has a great thinker for that CHADEMA will win 2015

mkuu kumpongeza Membe ni sawa na kumpongeza shibuda, maana hata shibuda naye alisema kile anaachoamini ni ukweli na hakujali kupishana na chama chake, ni lazima uwe pumpkin head kumpongeza Membe , shibuda, Jmakamba,kigwangallah, kilango malecella, sendeka kwani ol of them are lie on de sem line.

Wanafiki@yahoo.com
 
Ben,

..ungesubiri kidogo kabla ya kutoa pongezi hizi. kumbuka kwamba Membe ni CCM mwanamtandao, na tunajua jinsi kundi hilo lilivyoleta siasa chafu ndani ya CCM na taifa kwa ujumla.
 
Ben,

..ungesubiri kidogo kabla ya kutoa pongezi hizi. kumbuka kwamba Membe ni CCM mwanamtandao, na tunajua jinsi kundi hilo lilivyoleta siasa chafu ndani ya CCM na taifa kwa ujumla.

Kwa maoni yako haya napata moyo kwamba ss tz tuna utajiri wa wasomi wanajoua nn maana politics.
Tanx broda.
 
Hakuna kitu hapo cha kumpongeza Membe maana ule ni unafiki tu, kwan kuna tofauti gani kati ya membe na shibuda? Inamana unataka kutuaminisha kuwa hata na Shibuda naye ni shujaa maana vitendo vinafanana na Membe, kama yy ni gamba inabidi afanye yale yanayokubaliana na wenzake , tatizo wana CDM wengi huwa tinatukuza mambo ya kijinga kama haya alfu yakitugeukia na ss tunaanza kulalama, tabia za undimilakuwili kama huu ndio ulinifanya niondoe iman na viongzoi wangu wa CDM kama Zitto kabwe, Shibuda, Yule makamu wa Bavicha, koz sipendi unafiki na wanafiki na ni lazima tuwe tunawasema hadharan pasipo kuogopa ili nao wajijue.
UNAFIKI NDIO ULIMPONZA YUDA KUMSALITI YESU.

Speak for yourself.......

Unatukuza wewe mwenyewe

Suala la Shibuda na la Membe ni Tofauti.Tusichanganye mambo.Shibuda katangaza atagombea Urais na meneja kampeni wake ni JK anayetoka CCM.CCM na CHADEMA ni vyama vyenye itikadi tofauti.Mgombea urais wa chadema atanadi ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ambayo maudhui yake na msingi wake kisera ni tofauti kabisa na ya CCM (anakotoka meneja kampeni na ni rais anayemaliza muda wake).Huu ni utani wa gharama.....Tafakari na utofautishe mambo haya mawili

Ben,

..ungesubiri kidogo kabla ya kutoa pongezi hizi. kumbuka kwamba Membe ni CCM mwanamtandao, na tunajua jinsi kundi hilo lilivyoleta siasa chafu ndani ya CCM na taifa kwa ujumla.

Jokakuu,

Kizuri kisemwe.Siyo kwa sababu mtu yupo chama kingine ndiyo iwe Nongwa

Leo tunashuhudia wana-CCM wakichangia upinzani.Je hawa nao ni wanafiki? Tuwe wakweli.Ndiyo maana nasema tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila maandalizi.Leo tunaangalia watu badala ya kuangalia hoja.Mashambulizi ya kisiasa yanaelekezwa kwa watu badala ya kushambulia hoja.

Colin Powell aliyekuwa waziri wa mambo ya nje kutoka Republican alimu-endorse Obama(democrats) badala ya Mgombea wake john Maccain.Haikuleta kelele kwa sababu ya ukomavu wa kisiasa

Pia Membe hata kama ni mwanamtandao aliyesababisha madhara kwa Taifa haifanyi ukweli atakaousema uwe haramu siku zote.Hebu tujenge demokrasia ya kweli na tuwe genuine siku zote.

Nahofia sana hulka yetu watanzania kuzoea wanasiasa wanaopiga siasa za u-simba na u-yanga.Wanasiasa hawa ndiyo wanaosababisha machafuko inapofikia hatua chama cha upinzani kinaposhinda uchaguzi.Wanalisha watu propaganda kwamba chadema haiwezi kuingia ikulu mwaka 2015.Wanaandaa mazingira ya uchakachuaji na hujuma kwa gharama yoyote.Membe ameonyesha njia.Wengine wafuate

Chadema tukaze buti.Narudia tena:Membe jenga chama chako ikishindikana karibu Chadema.......
 
Amesoma alama za nyakati huyo anatengeneza kushoto na kulia wakimzibua huko kwake anasepa anaenda kulia kwenye chama cha ukombozi hakika waliomuona ITV watakubaliana kwamba alimaanisha aliyoyasema
 
Back
Top Bottom