Membe Alikoroga CCM, kauli yake ya CHADEMA kushika dola yamponza

Amesoma alama za nyakati huyo anatengeneza kushoto na kulia wakimzibua huko kwake anasepa anaenda kulia kwenye chama cha ukombozi hakika waliomuona ITV watakubaliana kwamba alimaanisha aliyoyasema

Ni kweli mkuu.Unajua kuna siku nilishambuliwa hapa kwa kuwa nilisema Membe ni miongoni mwa mawaziri wachache wanaotumia Taaluma zao kiweledi.Ni jasiri,ana misimamo na anajua anachokifanya ingawa nina ugomvi nae kwenye sula la kufanyia overhaul sera yetu ya mambo ya nje.Ngoja nitatoa mawazo yangu yatakayowasukuma kuchukua hatua kwa kutoa maoni yangu kwa Wizara kivuliya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa........
 
Ben said:
Jokakuu,

Kizuri kisemwe.Siyo kwa sababu mtu yupo chama kingine ndiyo iwe Nongwa

Leo tunashuhudia wana-CCM wakichangia upinzani.Je hawa nao ni wanafiki? Tuwe wakweli.Ndiyo maana nasema tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila maandalizi.Leo tunaangalia watu badala ya kuangalia hoja.Mashambulizi ya kisiasa yanaelekezwa kwa watu badala ya kushambulia hoja.

Colin Powell aliyekuwa waziri wa mambo ya nje kutoka Republican alimu-endorse Obama(democrats) badala ya Mgombea wake john Maccain.Haikuleta kelele kwa sababu ya ukomavu wa kisiasa

Pia Membe hata kama ni mwanamtandao aliyesababisha madhara kwa Taifa haifanyi ukweli atakaousema uwe haramu siku zote.Hebu tujenge demokrasia ya kweli na tuwe genuine siku zote.

Nahofia sana hulka yetu watanzania kuzoea wanasiasa wanaopiga siasa za u-simba na u-yanga.Wanasiasa hawa ndiyo wanaosababisha machafuko inapofikia hatua chama cha upinzani kinaposhinda uchaguzi.Wanalisha watu propaganda kwamba chadema haiwezi kuingia ikulu mwaka 2015.Wanaandaa mazingira ya uchakachuaji na hujuma kwa gharama yoyote.Membe ameonyesha njia.Wengine wafuate

Chadema tukaze buti.Narudia tena:Membe jenga chama chako ikishindikana karibu Chadema.

Ben,

..tatizo langu ni kwamba uliandika kana kwamba Membe amekuwa msafi siku zote.

..ungeweka angalizo kwamba pamoja na hiyo lunch aliyowapatia CDM, Membe ana historia ya kuwa miongoni mwa wahusika wakuu ktk kundi la wanamtandao ambao wameivuruga CCM pamoja na siasa za nchi.

..zaidi wizara ya mambo ya nje ndiyo inahusika ktk kuandaa safari za nje zisizo na tija za Raisi Kikwete. safari hizo zimeisababishia nchi hasara ya mabilioni ya fedha.

..vilevile hivi ukomavu wa kisiasa wa Benard Membe unapimwa kwa hili tukio moja tu, wakati kuna mlolongo wa rekodi na matukio kwamba huyu ni mmoja kati ya mawaziri wazembe wa JK??
 
na mashaka na maneno ya membe kama yalikuwa yanatoka moyoni au ndio kujipendekeza aonekane ni mwanademokrasia? subiri atakavyoshambuliwa kwenye kikao cha ndani cha nec sijui nani atatujuza? Halafu nimegundua humu jamvin hata hao wanasiasa na viongozi wa dini wamo humu sema hatuwajui? JF kiboko cha maneno watanzania woote wangekuwa na access ya hili jamvi.
 
Ben,

..tatizo langu ni kwamba uliandika kana kwamba Membe amekuwa msafi siku zote.

..ungeweka angalizo kwamba pamoja na hiyo lunch aliyowapatia CDM, Membe ana historia ya kuwa miongoni mwa wahusika wakuu ktk kundi la wanamtandao ambao wameivuruga CCM pamoja na siasa za nchi.

..zaidi wizara ya mambo ya nje ndiyo inahusika ktk kuandaa safari za nje zisizo na tija za Raisi Kikwete. safari hizo zimeisababishia nchi hasara ya mabilioni ya fedha.

..vilevile hivi ukomavu wa kisiasa wa Benard Membe unapimwa kwa hili tukio moja tu, wakati kuna mlolongo wa rekodi na matukio kwamba huyu ni mmoja kati ya mawaziri wazembe wa JK??

Ukomavu wa Membe haupimwi kwa Tukio hili moja tu.

Membe ni Waziri anayemudu potfolio yake kwa weledi (tukiachana na hoja ya reform kwenye foreign policy).

Uwezo wa Membe kidiplomasia ni mkubwa.Bila shaka hata katika Medani za kimataifa anayemng'arisha JK ni Membe.JK anaonekana kuaminiwa na kuwa na nguvu nje ya Tanzania kwa kuwa ana waziri ambaye ni powerful wa mambo ya nje.Mawaziri wa JK na watumishi wengine wangekuwa powerful hivi JK angekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hali yake ilivyo mbaya hivi sasa.Uwezo wa JK no doubt ni mdogo.Anahitaji booster.Hata Obama legacy yake nje inabebwa na Joe Biden(mtaalamu wa mambo ya nje) na Hilary Clinton(Secretary,Foreign Affairs)

Suala la Ziara za Nje linatokana na mfumo wetu mbovu ambao kimsingi linajikita katika vipaumbele vyetu ambavyo vina-lean moja kwa moja kwenye sera zetu za nje(hili Membe ana hisa ya lawama kwa kiwango flani,i agree with you).

But tukiwa wakweli mioyoni mwetu ni kwamba Membe kwenye siasa za kimataifa anatumia taaluma yake vizuri na kutekeleza kanuni zake kwa weledi.Natambua kuna tuhuma nzito zimeandalia na mahasimu wake kisiasa tena kwa kuhusisha wanasiasa vijana wasomi ili kummaliza kisiasa kwa matakwa binafsi ya watu

Watu hao wakimalizana na Membe ndani ya CCM wanaelekeza makombora hayo kwa viongozi wa juu wa chama cha CHADEMA. Siasa za aina hii hazitalisaidia Taifa zaidi ya kuliangamiza.Huko baadae hali hii itazaa uasi wa kutisha
 
Bernad-Membe.jpg

• Lema amtaka ajiuzulu ikiwa ataonyeshwa mkanda

na Happiness Mnale Tanzania Daima

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amejikoroga akikana kauli yake ya kukitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukitaka kijiandae kushika dola mwaka 2015.
Membe alitoa kauli hiyo ya kuisifu CHADEMA, nyumbani kwake hivi karibuni alipomkaribisha mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho (Godbless Lema) na James ole Millya, mbele ya waandishi wa habari.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Membe alisema kuwa wakati taarifa hiyo inatolewa na vyombo vya habari, alikuwa safarini London, hivyo kusikitika kuwa viliripoti uongo.
Wakati Membe akikana kauli yake, Lema alisisitiza kuwa hana sababu ya kubisha kwani kauli hiyo aliitoa na hivyo kumuuliza kama atakuwa tayari kujiuzulu endapo ataonyeshwa mkanda uliorekodiwa siku hiyo.
“Alizungumza mambo mengi kuhusu CHADEMA tena kwa nia njema kabisa na hasa kaulimbiu yetu ya ‘people’s power’, kuwa inahamasisha watu hasa wakati huu ambao CCM ina mivutano akidai itatuletea mafanikio, sasa haihitaji kujitetea kwa hilo bali aseme kama atajiuzulu akionyeshwa mkanda huo,” alisema Lema.
Membe katika utetezi wake, alisema kuwa wakati wa mazungumzo yake na makada hao wa CHADEMA hakuwahi kutoa kauli hiyo kwa vile yeye si mtabiri na kwamba haamini kama uzushi huo ulienezwa na chama hicho bali yuko mtu aliyetunga jambo hilo.
“Mimi nafahamu watabiri ambao ni Nabii Joshua wa Nigeria na marehemu Sheikh Yahaya Hussein wa Magomeni hivyo anayetaka utabiri aende huko, naona kuna mkono wa mtu katika hilo.
“Mimi ni mwana CCM mpaka naenda kaburini, jambo hilo liliwekwa makusudi ili kunifitinisha na wenzangu pamoja na CHADEMA, siwezi kuacha kuwa mkarimu kwa kukaribisha watu nyumbani kwangu,” alisema Membe.
Alifafanua kuwa upinzani sio uadui na nchi zote zilizojaribu kuona upinzani kuwa uadui haziko salama, hazina amani na haziendelei, hivyo Tanzania haiwezi kuwa katika upande huo.
“Maadui wa vyama vyetu ni sisi wenyewe tulio ndani ya vyama kama unaleta ubaguzi, hujakomaa kisiasa, maadui wako ndani ya CCM na wanajitafuna wenyewe, wapo wengine wanashabikia jambo hilo tena ni wana CCM wenzangu,” alisema.
Akizungumzia hatua yake ya kulazimika kwenda Lindi katika kipindi cha ziara ya CHADEMA, alisema kuwa alienda kwa ajili ya Mwenge na kujibu hoja za chama hicho ili kufukia mashimo.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya CCM ambazo bado hazijathibitishwa na Tanzania Daima, ni kwamba Membe ametishwa kuhusu kauli zake hizo akidaiwa kuhatarisha uhai wa chama chake.
Wakati huohuo, Membe alizungumzia kuhusu fedha za gharama za usafiri wa Rais zilizodaiwa kupotea, akisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi mosi mwaka huu wakati yeye, naibu wake, Katibu Mkuu, naibu katibu na mhasibu mkuu na msaidizi wake wakiwa hawapo.
Membe alifafanua kuwa waliokuwepo walifanya mchakato huo japo hakuna fedha zilizoibwa na kwamba zote zilizofanyiwa mchakato zilikuwa sh bilioni mbili ambazo zimeshaingia katika wizara yake.
Alisema kuwa gharama halisi ilikuwa bilioni 3.5 na fedha hizo zilikuwa za safari ya Geneva, Addis Ababa na Arusha lakini zilizofanyiwa mchakato ni sh bilioni mbili.
“Hakuna tuliyemuita mwizi, wala kumshutumu, fedha hizo hakuna hata senti moja iliyoibwa ziliingia katika akaunti ya wizara tuliziona na tukazihesabu,” alisema. Membe aliongeza kuwa wameamua kuunda kamati ya uchunguzi kama taratibu zilifuatwa kiutawala, jambo hilo halihusiani na wizara moja, na ama mwanya huo uliotokea ili kuona makosa yalifanyika wapi.
Kamati hiyo inaundwa na mkaguzi mkuu wa ndani, usalama wa taifa, wakaguzi wa ndani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo uchunguzi utakapokamilika, watatangaza.

Chanzo Tanzania daima

Ukomavu wa Membe haupimwi kwa Tukio hili moja tu.

Membe ni Waziri anayemudu potfolio yake kwa weledi (tukiachana na hoja ya reform kwenye foreign policy).

Uwezo wa Membe kidiplomasia ni mkubwa.Bila shaka hata katika Medani za kimataifa anayemng'arisha JK ni Membe.JK anaonekana kuaminiwa na kuwa na nguvu nje ya Tanzania kwa kuwa ana waziri ambaye ni powerful wa mambo ya nje.Mawaziri wa JK na watumishi wengine wangekuwa powerful hivi JK angekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hali yake ilivyo mbaya hivi sasa.Uwezo wa JK no doubt ni mdogo.Anahitaji booster.Hata Obama legacy yake nje inabebwa na Joe Biden(mtaalamu wa mambo ya nje) na Hilary Clinton(Secretary,Foreign Affairs)

Suala la Ziara za Nje linatokana na mfumo wetu mbovu ambao kimsingi linajikita katika vipaumbele vyetu ambavyo vina-lean moja kwa moja kwenye sera zetu za nje(hili Membe ana hisa ya lawama kwa kiwango flani,i agree with you).

But tukiwa wakweli mioyoni mwetu ni kwamba Membe kwenye siasa za kimataifa anatumia taaluma yake vizuri na kutekeleza kanuni zake kwa weledi.Natambua kuna tuhuma nzito zimeandalia na mahasimu wake kisiasa tena kwa kuhusisha wanasiasa vijana wasomi ili kummaliza kisiasa kwa matakwa binafsi ya watu

Watu hao wakimalizana na Membe ndani ya CCM wanaelekeza makombora hayo kwa viongozi wa juu wa chama cha CHADEMA. Siasa za aina hii hazitalisaidia Taifa zaidi ya kuliangamiza.Huko baadae hali hii itazaa uasi wa kutisha​

  • Ben,

    ..how can u endorse mwana CCM tena kinara wa kundi la wanamtandao?

    ..wewe unalichukuliaje kundi la wanamtandao na jinsi walivyovuruga siasa za nchi yetu na kuingia madarakani wakitumia fedha chafu?

    ..zaidi, wizara ya mambo ya nje, chini ya uongozi wa Benard Membe, wanatumia bilioni 3.5 kwa safari za Geneva,Addis,na Arusha. hivi unafahamu kwamba fedha hizo zingeweza kujenga vyuo vya Veta 2 au shule za sekondari fully equiped 4?? sasa pesa za kutumbua kwenye safari wanazo lakini kulipa ada ya AU hawataki.

    ..kwa mtizamo wangu, maoni yako yanathibitisha ule msemo wa " ukipenda chongo huita kengeza ."
 
Ukiniambia kama Membe anaweza kuwa mkuu wa nchi hilo nitalipinga.ukiniambia katika mawaziri katika serikali hii ni yupi angalao mwenye uwezo nitasema Membe.....mambo mengine ya mtandao and rhetorics aside!
 
Back
Top Bottom