Membe Alikoroga CCM, kauli yake ya CHADEMA kushika dola yamponza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe Alikoroga CCM, kauli yake ya CHADEMA kushika dola yamponza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 13, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  KAULI ya hivi karibuni iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ya kuitabiria ushindi na kukitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kijiandae kushika dola mwaka 2015, imewaduza vigogo na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Membe ambaye ni mmoja wa makada wa CCM wanaotajwa kuutaka urais mwaka 2015, alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akiukaribisha msafara wa CHADEMA nyumbani kwake kijijini Rondo na kushiriki nao chakula cha pamoja.

  Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zilisema kuwa kauli ya Waziri Membe si tu kwamba imewashangaza vigogo wa CCM, bali pia imetafsiriwa kama ni mmoja wa mawaziri wanaotajwa kutaka kujiunga na CHADEMA hasa baada ya jina lake kutajwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kama mmoja wa mawaziri wanaotarajiwa kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara hivi karibuni uliofanyika mjini Sengerema, Lema aliwataja mawaziri wengine wanaotarajiwa kujiunga na CHADEMA kuwa ni pamoja na Edward Lowassa (Monduli) na Samuel Sitta (Urambo Mashariki). Lowassa na Sitta kwa nyakati tofauti walikanusha madai hayo, lakini Waziri Membe hajawahi kukanusha.

  Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Emmanuel Nzungu aliliambia gazeti hili jana kuwa kauli ya Waziri Membe ina utata mkubwa.

  "Tumezungumza kwenye vikao vyetu hapa ofisini, tumeona kuna haja ya kuleta hoja hii kwenye vikao vya juu vya chama. Hii si kauli ya utani bali ni kauli iliyopangwa na hatujui kwa sababu gani," alisema Nzungu.

  Alisema kibaya zaidi kauli hii imetolewa na Waziri Membe siku chache baada ya Lema kumtaja kuwa mmoja wa mawaziri wanaotajwa kutaka kuhamia CHADEMA.

  "Ningesoma kwenye magazeti, ningesema amewekewa maneno mdomoni, lakini nilimwona kwa macho yangu kwenye kituo cha televisheni ya ITV aikimwagia sifa CHADEMA na kuitabiria ushindi. Hii inashangaza sana na lazima kauli yake ijadiliwe kwenye vikao vya chama," alisema Nzungu.

  Kada mwingine ambaye ni mjumbe wa NEC aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema kuwa anashangazwa na ukimya wa viongozi wa juu wa CCM kwani hakuna aliyetoa kauli ya kumwonya Waziri Membe.

  "Kuna makada wa CCM waliowahi kutoa kauli ndogo tu, lakini chama kilitumia nguvu kuzijibu na kuzitolea ufafanuzi. Hii kauli ya Waziri Membe ya kuitabiria kifo CCM na kuitabiria ushindi CHADEMA si ya kupuuzwa," alisema mjumbe huyo wa NEC toka mkoani Shinyanga.

  Hivi karibuni Waziri Membe aliwakaribisha na kufanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA waliotembelea kijijini kwake.

  Katika mazungumzo yake na viongozi hao mbele ya waandishi wa habari, Waziri Membe alikitabiria chama hicho kushika dola mwaka 2015 kwa vile kina mvuto kwa Watanzania.

  Viongozi waliokaribishwa nyumbani kwa Membe ni pamoja na Lema, James Millya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa kata za Chiponda na Mnara.

  Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama na mjumbe wa NEC, aliwatahadharisha wabunge wenzake wa CCM kwamba wako hatarini kung'olewa katika majimbo yao na CHADEMA kwani chama hicho kwa sasa kimeimarika na kukubalika kwa wananchi wengi.

  "CHADEMA sasa imegundua udhaifu wao uliokuwa ukisababisha isishinde, zamani mlikuwa mkifanya kampeni mikoani, lakini kitendo cha kufika kata hadi kijiji, hii sasa ndio siasa safi.

  "Wapo wengi wanaodhani kuja huku ni kama mmekuja kuwavamia la hasha, siasa ni nguvu ya hoja, haina maana mmekuja kumshughulikia mtu, binafsi najua nguvu ya hoja ndiyo inayoleta maendeleo.

  "Pia nguvu ya hoja inasaidia kuleta maendeleo, yaani nguvu ya hoja unaweza kuita ni mgongano au msuguano wa kimawazo ambao unakumbusha uwajibikaji wa chama na serikali.

  "Mimi najua maana ya siasa, nimeishi miaka 10 nje ya nchi zenye demokrasia safi, ikiwamo Marekani, pia nimesoma miaka miwili, hivyo kuja kwenu hapa kunaweza kuchukuliwa na wabunge au Watanzania wengine mmekuja kuwaingilia, hapana.

  "Mimi naipenda siasa ya demokrasia na nailewa zaidi na ndiyo maana niliposikia mko huko nimesitisha ziara zangu jimboni na natarajia kurudi Dar es Salaam na kusafiri kwenda nje ya nchi," alisema.

  Membe alisema katika dunia hii ya tatu, vitu vyote vinabadilika yakiwamo mabadilko ya siasa na kuongeza kwamba, hali ilivyo Tanzania lazima kutakuwapo na mabadiliko ya vyama vya upinzani kushika dola.

  "Kuna nchi nyingi zilikuwa na vyama zaidi ya 500 ikiwamo Angola, lakini hadi sasa vimepungua na kufikia 310, sasa tahadhari yangu kwenu CHADEMA hivi sasa mko ‘strong' na mnashika nafasi ya pili, muanze kujiandaa kuunda serikali ingawa bado kuna vita vikali mbele.

  "Mnaweza mkajiamini mnaweza kushinda, lakini mwishowe upepo ukageuka, unajua binadamu na mnyama ni vitu vya ajabu sana, vyama vingine vinaweza kutumia rungu hilo hilo kukumaliza," alisema.

  Adha, Membe aliwaonywa viongozi kuchukua tahadhari kubwa juu ya serikali ya umoja, huku akitolea mfano nchi za Kenya na Ethiopia.

  "Hakuna serikali yoyote ya mseto au ya umoja itakayoleta maendeleo kwa wananchi na sote ni mashahidi wa nchi hizo, mfano Keneth Kaunda chama chake kilikuwa na wafuasi wengi kikashinda na watu wakashangilia, lakini wiki tatu za kwanza walikuwa katika vita vya kuunda serikali.

  "Serikali ya mseto ina madeni makubwa, maana kila chama, taasisi mtu ana watu wake wa kutaka kupewa madaraka, mwishowe mnajikuta matatizoni, epukeni misaada ya wafadhili maana waliokusaidia watakugharimu baadaye.

  "Hapa kwetu kule Zanzibar wamenusurika kwa kitu kimoja tu, CCM na CUF wameunda Serikali ya Umoja, lakini Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndicho kilichowasaidia.

  "Ile serikali ipo chini ya chama mama, chama chenye nguvu na fedha, kina miongozo, kanuni za CCM zinazotekelezeka," alisema.

  Alimweleza Lema kwamba alisikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya kumnyang'anya ubunge.

  "Lema, sikuamini baada ya maamuzi kutolewa na mahakama, lakini kama umekata rufaa nafikiri huku kutatendeka haki zaidi, bila shaka utarudi bungeni," alisema.
   
 2. d

  davidfrance82 Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Membe is my role model.......
   
 3. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  If you can't fight them, join them - George Bush
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Aliyefichwa jina ni Hamis Mgeja mwenyekiti wa CCM shinyanga na mjumbe wa NEC,ndiye huwa na Nzungu kila kukicha,sku nyingine asiogope kujitaja
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sasa walitaka aseme uongo?
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  no more comments Membe amemaliza, asante
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm ukisema ukweli unakuwa adui ndani ya chama. ccm wanachokiaminin zaidi ni uongo
   
 8. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  wa ta ji ju
   
 9. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Membe! Membe! Membe!

  Laiti angekuwa raisi wa nne.
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Making a mountain out of nothing. He expressed his views to which he is entitled. His freedom of speech should be respected.
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,109
  Trophy Points: 280
  Karibu sana na hongera kwa kusoma alama za nyakati
   
 12. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kasema kama mwanademokrasia na anaamini demokrasia kwani mwenye nguvu ya hoja na zinazokubalika na wananchi ndo anachaguliwa.

  Hongera Membe kwa ukomavu wa siasa ulionao.
   
 13. N

  Ndinimbya Senior Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huyu jamaa ni daktari anayejua mgonjwa wake(CCM) anaendeleaje ndiyo maana kayasema haya
   
 14. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndo hiyo, nasikia harufu ya ushindi. CDM ndo kila k2.
   
 15. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Hilo ndilo daraja la CDM Shinyanga hasa tukianza na jimbo la mjini
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Membe alisema kauli hiyo ilikuwa poza chadema wasimchanechane jukwaani lakini ilikuwa ni tofauti kwani makamanda walipopanda jukwaani walimchana kama kawa...
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Ameongea mambo ya msingi kabisa,na ametushauri vizuri kabisa, sasa nyinyiemu mjiandae sasa. Yan nap umenyamaza hadi muda huu! Kweli kuna watu hawagusiki kule nyinyiemu.
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mbona wote ccm wanalijua hilo!!!
   
 19. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shibuda alipotofautiana na Chadema,CCm walishangilia wakisema aachwe kwani kutoa amwazo ni
  haki ya kila raia.Sasa mbona hapa kwa Membe wanaanza kigugumizi?Ukweli mimi binafsi namkubali
  sana huyu jamaa,hata ukiona akiongea hayuko kishabiki kama wenzake bali yeye yuko kitaifa zaidi.
   
 20. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi wanayo ccm, tutafika tu
   
Loading...