Nimeisikia Clouds FM Breaking News!, watu zaidi ya 200 wazama!. Mode iweke hii rasmi kama breaking news!. Imezamia pale pale pa ile boti ya MV Islanders, karibu na kisiwa cha Chumbe!.
My God!.
May the Lord Our God, Rescue Them!.
Ya jana iliokolewa ilikuwa inaelekea pemba, hii imetokea leo saa 9 ilikuwa inatoka Dar kwenda Zanzibarimepinduka bado haijazama imekuwa kama ile ya Mv Bukoba
Mungu azinusuru roho za abiria wote
Ni MV Kalama Mkuu. Ilikuwa na abiria approximately 200. Capacity yake ni 250. Inazo lifeboats za kutosha watu 300 na lifevests pia za kutosha 260. Wengi wameokolewa na habari nilizo nazo ni kuwa process ya kuokoa bado inaendelea.
Ni MV Kalama Mkuu. Ilikuwa na abiria approximately 200. Capacity yake ni 250. Inazo lifeboats za kutosha watu 300 na lifevests pia za kutosha 260. Wengi wameokolewa na habari nilizo nazo ni kuwa process ya kuokoa bado inaendelea.
twen zetu!Watakutukana huku mama,twende zetu kwetu chit chat
huu uzi uko jukwaa la siasa ina maana hii meli imezama kisiasa zaidi au?
mkuu silver, meli hiyo ndo mojawapo ya meli zilizosajiliwa na sumatra ya zanzibar, wenyewe wanaiita ZMA (znz maritime authority) na kina mamlaka kama ya sumatra huku tanganyika.Mtumeeee
Selikali hapa inapaswa kuwajibika Kuanzia Waziri hadi Takataka nyingine zinazo husika... Sumatra nanyie Muwajibike Kwanini muache Meli mbovu ziendelee kusafirisha Abiria?
Baada ya kusoma breaking news ya hapa JF, nikakimbilia TV ya taifa kuona wao wanasema nini kutudhibitishia kutokea ajali hiyo. Sasa ni zaidi ya saa nzima hawa jamaa wanaendelea na mavipindi yao yasiyo na mbele wala nyuma. AIBU.
Mataifa mengi Redio na TV za Taifa zinakuwa za kwanza kutaarifu majanga yatokeapo lakini hizi za kwetu ni za kwanza kueleza kifo cha kiongozi wa UVCCM Ndago Iramba na kuwa Chadema wanahusika.
Ukombozi ukitokea TBC ivunjwe
asitokee mjinga akaitoboa kama ilivyokuwa kwenye mv bukoba....yule mkuu wa mkoa basi tu kwa vile amekufa majuzi
inasemekana MV seagul ikitokea Dar kuelekea zanzibar imezama. kila tupato habari tutazidi kuhabarishana
Update:
Ilikua na abiria 200 na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vipo. Meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu mara kadhaa.
View attachment 59156
tunasubiri taarifa kamili mkuu....