Meli ya MV Skagit yazama

Meli ya MV Skagit yazama

Wat did you expect? kwani waliohusika na uzembe wa kuzama kwa meli mwaka jana walifanywa nini? nchi hii bwana, uzenbe uzembe uzembe tu.....kama imewahi kuripotiwa kuwa meli hiyo ni mbovu je ilikuwa imetengenezwa? ilisimamishwa lini na kufunguliwa lini? nani aliyeidhinisha ianze safari? service ilifanyiwa lini mara ya mwisho?wapi? kwenye gereji bubu? hah what do you expect?
Subiri mtaona mengi katika nchi ambayo kuanzia baba, watoto na watumwa wao wa ndani wote ni wasanii!!!!!
 
Tanzania kama taifa tunachezea makali ya wembe,ukitukata hakuna wa kumlaumu!!!!!!
 
Innalilahi wa Ina ilaihi Rajiun,Hakika kwake tutarejea. Kumbe ndio ile ilizimika Nungwi? Hii balaa jamani!
 
Mh jana niliona taarifa ya habari kuwa ilivutwa sasa kama ilianza tena safari leo, watakuwa wamefanya makusudi kabisa .

Tajiri na wahusika wa meli hii ni wazi watakuwa na kesi ya kujibu ya mauaji ya makusudi.

labda kama sio TZ.......hapa ata Waziri anaeusika alitakiwa kuja kutoa maelezo kwa nini asijiuzulu ikiwa izi ajari zinafuatana..
 
Nimesikia pia, na inasemekana ilikuwa na abiria zaidi ya hao. Hakuna nchi ya ajabu kama Tanzania, tuna laana ya kuchagua chama chenye laana, ajali hizi zinatokea hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kuzuia ajali hizi, na kwa hakika chini ya serikali hii tutakufa kama njugu kama tusipojisalimisha chini ya mwenyenzi MUNGU.

Siyo chama ni uongozi hafifu!! Mimi siyo CCM (actually mimi ni CDM), lakini kwenye issue kama hii unapolaumu chama wakati unajua wazi kuwa ni uongozi, unawapa excuse wahusika. Hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa kuadhibu wale waliosababisha vifo vilivyosababishwa na meli ya mwisho iliyozama. Sana sana serikali badala ya kufanya uchunguzi madhubuti na kueleza ukweli walikuwa busy wanajaribu kuficha kiasi cha abiria walipotea kwenye mkasa ule. Hadi sasa hakuna mahali popote nimeshaona namba kamili ya watu waliopotea. Kwani CCM imeanza kuongoza kipindi hiki tu? Mbona kwenye uongozi uliopita mikasa hii ilikuwa haipo kwa frequency hii? Same as corruption! Same as road accidents! Imezidi kwa sababu wahusika hawaogopi kuadhibiwa. Jiulize, kule Loliondo ni watu wangapi walipoteza maisha kwa sababu serikali ili-sanction kile kikombe cha babu? This is **** resulting from crappy leadership NOT the party. Tusikubali kuwaacha viongozi bila lawama wakati tunajua kuwa ubovu uko kwao.
 
KUMBE MELI YENYEWE ILIKUA MBOVU MBOVU TOKEA ZAMANI.... Soma hiyo iliyotokea tarehe 12/05/2012:

Mv. Seagull yazima moto ikiwa safarini kuelekea Pemba


Written by Mrfroasty (Ufundi) // 13/05/2012 // Habari // 5 Comments

Salma Said,
ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.

Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.

Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.

“Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele” alisema Masoud.

Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.
Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.
Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.

Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.

wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.

“Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.

Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.


Mimi sishangai kwa Tanzania kuendelea kutumia meli mbovu kwani viongozi wetu hawatujali. Magari mangapi yako barabarani yanabeba abiria lakini ni mabovu. Mungu tusaidie ifike 2015 tuondokane na CCM janga la Taifa.
 
Nilisikia ktk TV, kabla ya tukio hili, kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa hadhari khs hali ya hewa ya leo, lkn cha ajabu hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia vyombo vya majini kusafiri au kwenda kufanya shughuli nyingine baharini, km uvuvi.
Milango ya saa sita na nusu mchana wa leo, palitokea a freak storm, upepo usio wa kawaida kabisa ulioambatana na vumbi hapa jijini Dar es salaam.
Ilibidi nikimbilie dirishani katika jengo la ghorofa ya kwanza hapa jijini ili nitazame kulikoni, maana muungurumo ulikuwa mkubwa.

Hii ni pamoja na ukweli kuwa toka asubuhi ya leo pamekuwepo na upepo usio wa kawaida.
Pale bandarini kwa hali hii chombo kisingeruhusiwa kuondoka.

Sasa sijui kama kuonya usafir wa baharini nani anchukua jukumu na kubeba lawama, liondolewe kwenye muungano!
 
Picha ziko wapi?

IMG_2429.jpg IMG_2429.jpg
 
IMG_stun4.jpg IMG_stun4.jpg Image captured from above by a friend aliyekuwa kwenye ndege ndogo
Uki-zoom utaona watu in circles na maboya

sad event
 

Attachments

  • IMG_stun3.jpg
    IMG_stun3.jpg
    51.6 KB · Views: 179
mara mv seagul mara mv karama....ni meli ipi hasa imezama?

Ni MV Kalama Mkuu. Ilikuwa na abiria approximately 200. Capacity yake ni 250. Inazo lifeboats za kutosha watu 300 na lifevests pia za kutosha 260. Wengi wameokolewa na habari nilizo nazo ni kuwa process ya kuokoa bado inaendelea.
 
Mkuu kwa nini unasema hii ni breaking news wakati huna taarifa kamili???? Subiri ukishakuwa na taarifa kamili ndo uanzishe uzi.

mbona unamind issue ndogo we unachotaka ni habari au?? kukosoa watu tu kwa issue za msingi acha gubu.
 
Kwa taarifa tu ni kuwa bado wako baharini, hawajaokolewa.
Meli iliyoenda kuwachukua/kuwaokoa (kilimanjaro) haijarejea..mawasiliano ni hafifu
 
Back
Top Bottom