Meli ya MV Skagit yazama

Meli ya MV Skagit yazama

Viongozi wote na polisi, majeshi yote na ambulances wamekusanyika mjini Zanzibar kuna hatari ya ajali za kugongana katika mji
 
meli za bakhressa na vyombo vyengine pamoja na vikosi vya Km km wanaelekea eneo la tukio kwa uokozi
 
Nimesikia pia, na inasemekana ilikuwa na abiria zaidi ya hao. Hakuna nchi ya ajabu kama Tanzania, tuna laana ya kuchagua chama chenye laana, ajali hizi zinatokea hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kuzuia ajali hizi, na kwa hakika chini ya serikali hii tutakufa kama njugu kama tusipojisalimisha chini ya mwenyenzi MUNGU.
 
halafu utashangaa kesho vyombo vya habai vinatumia picha ile ile ya mwaka jana halafu ya meli iliozama huko brazil
 
Ya jana ni kweli ilizima majini lakini abiria waliokolewa na ya leo ni nyingine boti kadhaa zikiwemo aina ya kilimanjaro zimeelekea eneo la tukio kuokoa watakaojaaliwa kuokolewa. Kweli tuwaombee.
 
Jamaa nafikiri mmekosea, ni MV SKAGIT na sio Seagull, ingawa zote ni kampuni moja!

By the way PASCO MV SPICE ISLANDER imezama katika mkondo wa nungwi na SKAGIT imezama mbele kidogo na chumbe island, 2 different location kabisaaa!!
 
Nimesikia pia, na inasemekana ilikuwa na abiria zaidi ya hao. Hakuna nchi ya ajabu kama Tanzania, tuna laana ya kuchagua chama chenye laana, ajali hizi zinatokea hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kuzuia ajali hizi, na kwa hakika chini ya serikali hii tutakufa kama njugu kama tusipojisalimisha chini ya mwenyenzi MUNGU.

Kweli kabisa mkuu jana kwenye vyombo vya habari kuna mojawapo inasemekana ilizimika maeneo ya ilipozama spice !
 
[h=6]Habari za hivi punde ni Meli ya Seagul ikiwa na abiria 200 imezama katika kisiwa cha Chumbe. Jitihada za uokoaji zinaendelea.[/h]
 
Nilisikia ktk TV, kabla ya tukio hili, kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa hadhari khs hali ya hewa ya leo, lkn cha ajabu hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia vyombo vya majini kusafiri au kwenda kufanya shughuli nyingine baharini, km uvuvi.
 
Jamani mwenyezi mungu atuepushie mbali balaa hili abiria watoke salama. Hivi serikali zetu zitajifunza lini? Matukio ya watu kuzama yamekuwa yanatokea mara kwa mara katika maziwa na bahari yetu lakini hakuna anayedhibiti hali hiyo. Hawa sumatra kazi yao nini hasa km wanaruhusu boti mbovu kutembea au boti imejaza watu na mizigo kupita kiasi?
 
Updates from Clouds sasa hivi: Imezama eneo la Chombe karibu na Serena hotel, imepigwa na wimbi kubwa. Ilikuwa inatoka Dar kwenda Zenji, idadi ya abiria bado ni kitendawili.

Ila kiukweli hii meli huwa ina overload sana, mwaka jana nilijichanganya nikaipanda, nilijuta na nikaapa kuwa sitaipanda tena, maana ni zoa zoa, sidhani kama wana-control ya idadi ya watu na mizigo!
 
Rushwa wanazopokea Sumatra kutoka kwa mafisadi ndizo zinazo angamiza roho za wasafiri wa majini na nchi kavu
 
halafu utashangaa kesho vyombo vya habai vinatumia picha ile ile ya mwaka jana halafu ya meli iliozama huko brazil
Waandishi wa kibongo wavivu sana.
Mechi inachezwa Dar ambako ndio makao makuu ya vyombo vingi vya habari, na mechi hiyo imezalisha magoli matano au zaidi. Cha ajabu katika taarifa tena ya TV station mtu anawapa simulizi tu na kuonesha mchezo wa mwaka juzi tena usiohusisha timu zilizocheza leo. Ripoti inakamilika hata half time bado.
Wanakera sana hawa wazee wa vibahasha.
 
Baada ya kusoma breaking news ya hapa JF, nikakimbilia TV ya taifa kuona wao wanasema nini kutudhibitishia kutokea ajali hiyo. Sasa ni zaidi ya saa nzima hawa jamaa wanaendelea na mavipindi yao yasiyo na mbele wala nyuma. AIBU.
Mataifa mengi Redio na TV za Taifa zinakuwa za kwanza kutaarifu majanga yatokeapo lakini hizi za kwetu ni za kwanza kueleza kifo cha kiongozi wa UVCCM Ndago Iramba na kuwa Chadema wanahusika.
Ukombozi ukitokea TBC ivunjwe
 
Back
Top Bottom