Meli ya MV Skagit yazama

Jamani mwenyezi mungu atuepushie mbali balaa hili abiria watoke salama. Hivi serikali zetu zitajifunza lini? Matukio ya watu kuzama yamekuwa yanatokea mara kwa mara katika maziwa na bahari yetu lakini hakuna anayedhibiti hali hiyo. Hawa sumatra kazi yao nini hasa km wanaruhusu boti mbovu kutembea au boti imejaza watu na mizigo kupita kiasi?

Mkuu taratibu najua katika hali kama hii watu huhamaki na matokeo yake unaweza kuelekeza SHUTUMA kusiko. SUMATRA jurisdication yao mwisho ni Chumbe (kama wapendavyo kusema wa-ZNZ).

SUMATRA hairuhusiwi ku-operate ZNZ. ZNZ kuna chombo kingine kabisa kinaitwa ZMT(?)
 
KUMBE MELI YENYEWE ILIKUA MBOVU MBOVU TOKEA ZAMANI.... Soma hiyo iliyotokea tarehe 12/05/2012:

Mv. Seagull yazima moto ikiwa safarini kuelekea Pemba


Written by Mrfroasty (Ufundi) // 13/05/2012 // Habari // 5 Comments

Salma Said,
ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.

Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.

Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.

“Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele” alisema Masoud.

Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.
Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.
Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.

Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.

wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.

“Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.

Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.

Watanzania tunazidi kufa kwa uzembe wa wamiliki wa vyombo vya usafiri.huu ni uroho wa kutaka kuingiza tu hesabu bila kufanya service/matengenezo ya vyombo vya usafiri.hata mabasi hali kadhalika.na huko kwingine kuna thred ya kupasuka kwa kioo cha ndege.kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
 
Hizi sababu huwa hazibadiliki kila mara, wahusika kwanini wasiadhibiwe ipasavyo, ili iwe funzo kwa wengine?!

kila yakitokea majanga tunachekea viongozi wetu huku watanzania wenzetu wanapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu tungekomaa na wazembe serikali wajiuzulu wangekuwa careful, wewe subiri utaanza kusikia wanaanza kutoa rambirambi, maelezo chungu nzima,ila kesho mlio dar au zanzibar mngekusanyika ofisini kwa waziri mhusika mkitaka ajiuzulu haraka wangekoma!
 
Sijawahi serikali inayoua wananchi wake kama hii ya kwetu kwa kuruhusu mimeli mibovu iwe ndo machinjio ya watoto na kinamama kila kukicha
 
Eee Mwenyezi Mungu uturehemu sisi waja wako, hii laana itupishie mbali.... nchi hii imelaaniwa kwa laana kuu!
 
Leo kweli kulikuwa na upepo mkali mida ya saa tano tano, cause nguo zangu ziliwahi kukauka, labda bahari ilitibuka kweli, but kama ni hivyo, hali ya hewa ilionekana haieleweki, si wangezuia meli zisiondoke, but ngoja tutajua ukweli halisi later!
kuna upepo mkali xana leo Pwani ya Dar. kuna uwezekano mkubwa bahari ni chafu.

ni hisia tu. mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Oh! my God watanzania tumemkosea nini Mungu mbona sisi kila siku jama? sijui wakumlaumu mi nani maana ni too much
 
Sijawahi kuona serikali inayoua wananchi wake kama hii ya kwetu kwa kuruhusu mimeli mibovu iwe ndo machinjio ya watoto na kinamama kila kukicha
 
Sijawahi serikali inayoua wananchi wake kama hii ya kwetu kwa kuruhusu mimeli mibovu iwe ndo machinjio ya watoto na kinamama kila kukicha

Mkuu umenena vema lakini umeharibu hapo kwa red. Usiwe biased kiasi hicho, au una uhakika wanaume hawamo?
 
Leo kweli kulikuwa na upepo mkali mida ya saa tano tano, cause nguo zangu ziliwahi kukauka, labda bahari ilitibuka kweli, but kama ni hivyo, hali ya hewa ilionekana haieleweki, si wangezuia meli zisiondoke, but ngoja tutajua ukweli halisi later!

watu wanajadili vitu vya maana kama ubovu wa meli we unatangaza eti nguo zimekauka nani ana nguo?
 
Leo kweli kulikuwa na upepo mkali mida ya saa tano tano, cause nguo zangu ziliwahi kukauka, labda bahari ilitibuka kweli, but kama ni hivyo, hali ya hewa ilionekana haieleweki, si wangezuia meli zisiondoke, but ngoja tutajua ukweli halisi later!

watu wanajadili vitu vya maana kama ubovu wa meli we unatangaza eti nguo zimekauka nani ana nguo? au kama bahari imechafuka basi dunia nzima watu wangezama na maboti
 
watu wanajadili vitu vya maana kama ubovu wa meli we unatangaza eti nguo zimekauka nani ana nguo?
Yeye kakwambia kua kulikua na upepo mkali, sasa tujadili ubovu wa meli kwani sababu ya kuzama ishajulikana? hujawai kusikia meli mpya ikazama kutokana na sababu nyingine? subiri tujue chanzo ndo uanze kulaumu hapa
 
Back
Top Bottom