Meli kubwa ya mizigo yashindwa kukwamuliwa katika Mfereji wa Suez kwa siku ya tatu

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
93
150
Shughuli ya kuondoa meli kubwa ya mizigo iliyokwama katika mfereji wa Suez nchini Misri na kuziba njia kwa vyombo vingine vya maji kupita imeingia siku ya tatu hii leo bila mafanikio yoyote.

Jitihada za kugeuza meli yenye uzito wa tani 220,000 na urefu wa mita 400 iliyopewa jina Ever Given inaendelea leo baada ya mapumziko mafupi usiku, huku shughuli hiyo ikihofiwa kuchukua wiki kadhaa ikiwa uamuzi wa kupakua makontena yote yaliyopo kwenye chombo hicho utafikiwa kabla ya kukigeuza.

1920.jpg

Kukwama kwa meli hiyo katika mfereji wa Suez kumesababisha mrundikano wa vyombo vingine vya maji zaidi ya 150 katika bahari ya Mediterania na Bahari ya Shamu vikisubiri kukwamuliwa kwa Ever Given.

Meli hiyo iliyosajiliwa nchini Panama inayoendeshwa na kampuni ya Taiwan ilipoteza mwelekeo katika mfereji huo kutokana na upepo mkali uliofikia mwendokasi wa kilometa 50 kwa saa na kuifanya kuegama upande hivyo kuziba njia kwa vyombo vingine vinavyopita katika mfereji huo.

Mfereji wa Suez hupitisha hadi meli 50 kwa siku, na takriban asilimia 12 ya safari zote za baharini hupitia katika mfereji huo. Baada ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya Abdel-Fattah al-Sisi mwaka 2015, mfereji huo uliweza kupitisha meli kubwa zaidi duniani, ikiwamo Ever Given yenye uwezo wa kubeba makontena 20,000 kwa wakati mmoja.

Kuendelea kuzuiwa kwa mfereji huo kunamaanisha kuwa bidhaa za chakula, mafuta na bidhaa za viwandani zinashidwa kupitishwa kutoka mataifa ya Ulaya kwenda Mashariki ya Mbali na kutoka Mashariki ya Mbali kwenda Ulaya. Mbali na changamoto za kiuchumi, uwepo wa meli iliyokwama baharini kunaongeza hatari ya kiusalama kutokana na kuongezeka kwa matukio ya uharamia katika nchi za Mashariki ya Kati katikati ya mzozo baina ya Iran na Marekani.

1280.jpg


PIA SOMA>>Hasara ya mabilioni ya dola baada ya mfereji wa Suez kuzibwa na meli kubwa ya mizigo

Chanzo: The Guardian
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,690
2,000
Suluhisho ni wale wa kutoka mashariki ya kati na mbali wazunguke Afrika Kusini, Afrika Magharibi halafu waende huko Ulaya ama kwa kupitia Ureno au Gibraltar kuelekea nchi zinazopakana na Mediteranean. Kinyume chake na wale wa kutoka Ulaya wapite huko huko kuwahi masoko.
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,690
2,000
Wazunguke kwa madibakuwa na huruma mdau
Inachukua wiki mbili kuzungukia kwa Madiba na imekisiwa itachukua wiki tatu kuikwamua au kuteremsha makontena yote.Angalia mwenyewe kwa meli inayotoka Uiengereza, Ufaransa au Marekani na haijaingia uchochoro wa Gibraltar si ni bora wazunguke huko kuliko kuanza kukatisha mediteranea kwa wiki 1 ndipo ufike Suez halafu wiki tatu nyengine ufike Mombasa na Mtwara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom