Kwanini Gaza yote, kwanini sasa?

Kungarochi

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
271
572
Mgogoro wa Israel na Palestina umedumu kwa zaidi ya miaka 70 sasa.

Mara zote umekuwa ukisababisha machafuko makubwa yanayogharimu maisha ya watu, mamia kwa maelfu.

Safari hii kama safari nyingine huko nyuma, hali imechafuka tena, na maelfu ya watu wanaendelea kuuawa.

Bila shaka utakuwa umesikia sababu kadhaa za asili ya mgogoro huu; dini, siasa nk.

Lakini tofauti na mara zote machafuko yanapotokea, safari hii kuna sababu nyingine imeongezeka ambayo ni ya kiuchumi.

Kuna kitu kinaitwa mfereji wa Suez, yaani ni kama mto wa kutengeneza, unaounganisha bahari mbili za Sham na Mediterranea.

Bahari hizi ndiyo kiungo kikuyu kati ya bara la Ulaya na Mashariki ya Kati.

Mfereji huu ulijengwa na wakoloni wa kiingereza kati ya 1859 hadi 1869 ili kurahisisha usafiri wa majini kutoka Asia kwenda Ulaya.

Mwaka 1956 baada ya uhuru, Misri ikautafisha mfereji huu na kuufanya kuwa mali ya Misri.

Mfereji huu ni muhimu sana katika uchumi wa dunia kwa ujumla kwani unachangia asilimia 12 ya pato la dunia.

Asilimia 10 ya mafuta yanayosafirishwa duniani yanapita kwenye mfereji huu.

Mwaka 2022, Misri iliingiza kiasi cha Dola bilioni 22 kama ushuru wa kuitumia mfereji huu.

Kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji, mfereji huu kwa sasa unaonekana mdogo.

Kwanza hauruhusu meli mbili kupishana njiani, ni hadi moja ifike upande wa pili ndiyo nyingine ije, na safari moja inachukua hadi saa sita.

Kiuchumi hii inagharimu muda na pesa. Mbaya zaidi mwaka 2021.meli moja ilipata hitilafu na kuziba njia.

Ikasababisha meli nyingine zilizunguke bara la Afrika (angalia ramani ya pili) ili kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Siku moja tu ya kadhia kama hii husabanisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 9.6.

Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisema kadhia ile ilileta madhara makubwa sana kwenye jeshi la nchi hiyo.

Kutokana na hilo, mataifa makubwa ya Marekani, Uingereza na Ufaransa yameamua kujenga mfereji mwingine unaoitwa Ben Gurion kupitia nchi ya Israel.

Lakini mfereji huu ili utokee bahari ya Sham, inabidi upite Gaza.

Kwa hiyo Israel na washirika wake wanataka kuichukua Gaza moja kwa moja ili wapate kutekeleza mpango huu.

#ZakaZaKazi.
 
Mkuu ungekuwa na chanzo unge ambatanisha na hii habari ingekuwa vizuri sana ili tuchimbe zaidi kuhusu hii Siri.
Mkuu, Mbona wahusika na vita hiyo wameweka mambo bayana? Israel ametamka analipiza kisasi kujibu shambulio la kushtukiza la tar.7/10/2023. HAMAS(kwa mgongo wa Palestina) anasema anaikomboa ardhi yake lakini pia ameingiza humo mambo ya Udini na chuki binafsi(Hayuko straight forward).
Hayo mengine tunayoweka sisi yanatoka wapi na chanzo kipi? Hakuna siri; Vita ni vita baina ya Israel na HAMAS. Ni bahati mbaya tu kwamba hao HAMAS wapo hapo Nchini Palestina kwa kukaribishwa/Kibali/kuruhusiwa na Mpalestina. Lakini lengo la Israel liko wazi : Kuifuta HAMAS kwenye uso wa dunia - full stop. Ninaamini Myahudi amejiwekea Logical Framework Analysis kwa mpango huo.
 
Back
Top Bottom