Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Kupandishwa mshahara ni kuongezeka kwa take home pay ambayo inaweza kuongezwa kwa kupunguziwa kodi. Je wafanyakazi hawajapunguziwa kodi Ingawa kidogo?
Nyongeza ya mshahara ina positive effect kwenye pension ndugu.Nyongeza ni muhimu kuliko posho
 
One similarity between samia and magufuli, wote walipata urais kama zari hawakujiandaa.
 
In USA millions died on the road to democracy..it is also the same to UK, Germany, Russia etc..
USA hakuna demokrasia kule weusi kila siku wanapigwa shaba na police

UK nchi la kifalme hakuna demokrasia napo

Russia napo hakuna demokrasia kabisaaa Putin anaitawala Russia kwa mabavu na mpinzani wake kisiasa kamfunga hahahaaaa

Tanzania well Magufuli alikuwa ni Rais aliyependa maendeleo alifanya vingi na hapa anayepinga ni mpumbavu tu nchi haiwezi kuendelea kwa watu kulalamika lalamika wapige kazi tu

Rais samia Sina shida nae hizi ni siku chache mno watu kumpima uongozi wake ameshaonesha ana nia njema na Tanzania twendeni nae naye anataka kutengeneza legacy yake kitu ambacho ni jambo jema kwake
 
Actually iko hivi...
Kutoka Kwa Ben hadi JK walipunguza kabisa
Centralized government...
Wafanyakazi wachache hasa walimu
Na serikali kuu ndo walikuwa wanapata nyongeza ya kila mwaka kuanzia July..

Wakati Wengine hasa wa mashirika waliweka
Utaratibu wao.. mostly ilikuwa kila January..

Magufuli akaja kubadili nowadays watumishi wa mashirika hawana tofauti na walimu.
Mfano shirika kama NHIF wanapeleka makusanyo yote serikalini na wakipanga bajeti yeyote hata ya kuongeza Tu allowances
Inabidi waombe kibali na waombe hiyo bajeti serikali kuuu.... Shida imeanzia hapa...

Mfano we ni mstaafu wa NHIF baada ya miaka miwili kuanzia sasa bado na wewe unasubiri serikali kuu iweze kua approve increment zako zote za miaka 6 iliyopita ili uweze kustaafu ..ingawa NHIf wala haina shida ya pesa kukurekebishia... Magufuli alitoa hizo power Kwa taaasisi na mashirika ya serikali kujiendesha...so hata mfanyakazi wa TRA .
Na yeye Jana alikuwa anasubiria 'tamko'..

Kikwete aliweka utaratibu wa nyongeza za kimya kimya bila matamko...unless shirika au taasisi inaitegemea serikali 100 Percent..

Siku hizi kila shirika au taasisi kila kitu hadi
Wapewe go ahead..

Now Samia nna uhakika hata hajui how deep
Hii kitu ilivyo...
Kama ni hali ya uchumi why isingetoka go ahead Kwa taasisi na mashirika ambayo yako healthy kurekebisha hata hizo increment kwanza?..

Samia naamini Jana alizungumzia zaidi serikali kuu...

Mkuu sasahivi Hayo Mashirika yanapeleka Mapato yao yooote Hazina/Serikali kuu...
Sasa wanabaki 0!
Lengo serikali kupitia Kapu kuu ili Wagawe kwa taasisi nyingine!na Maendelo kwa Kila sekta zipo sekta ambazo hazizalishi!
 
USA hakuna demokrasia kule weusi kila siku wanapigwa shaba na police

UK nchi la kifalme hakuna demokrasia napo

Russia napo hakuna demokrasia kabisaaa Putin anaitawala Russia kwa mabavu na mpinzani wake kisiasa kamfunga hahahaaaa

Tanzania well Magufuli alikuwa ni Rais aliyependa maendeleo alifanya vingi na hapa anayepinga ni mpumbavu tu nchi haiwezi kuendelea kwa watu kulalamika lalamika wapige kazi tu

Rais samia Sina shida nae hizi ni siku chache mno watu kumpima uongozi wake ameshaonesha ana nia njema na Tanzania twendeni nae naye anataka kutengeneza legacy yake kitu ambacho ni jambo jema kwake
Watanzania wengi sio watu wa kufanya analysis kiwango kama hivi.

Heko mkuu
 
Mkuu hongera sana kwa maada hii na uchambuzi wako murua. Baada ya hotuba ile nami nilikuwa najiaandaa kutoka na uzi kama huu lakini nimeona mengi niliyofikiria umeyagusia hivyo mimi nitaongezea mawli niliyokuwa nimefikira yakiwemo hayo uliyoyajadili mkuu.

Kuna makosa naona yamefanywa na waandaaji wa hotuba ya rais. Rais hakuwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza isipokuwa alialikwa katika tukio la kitaifa na kimataifa lililokuwa linafanyika Mwanza. Kuanza kuwashukuru wanamwanza kwa kuichagua CCM na kuelezea miradi mbali mbali inayotekelezwa na itakayo tekelezwa Mwanza ilikuwa ni kukengeuka na kutoka nje ya lengo la shughuli tena wakati huo ameshawavuruga watu kwa kushindwa kukidhi matumaini makubwa waliyokuwa nayo ya kuongezewa mishahra.

Hiki kipengele hakikupaswa kuwepo katika kabisa hotuba ya Mei Mosi. Hayo yote aliyoyazungumza hayakuwa matarajio na mategemeo ya hadhira yake hivyo ilikuwa ni kuwachosha tu.

Jambo jingine ni mpangilio wa matukio au maelezo katika hotuba ya rais. Suala la mishahara ambalo ndilo lilikuwa hoja kuu iliyoyegemewa na kila mfanyakazi pale uwanjani na nchi nzima halikupaswa kuzungumzwa katikati ya hotuba kwakuwa ni wazi lilikuwa linakwenda kuwanyong'nyeza na kuwakera wasikilizaji wake hivyo lingewekwa mwishoni kisha baada ya hapo ashukuru na kuondoka. Baada ya taarifa ya kutoongezwa mishahara kila mmoja hakuona tena umuhimu wa kumsikiliza rais. Hili ni kosa lililovuruga usikivu wa hadhira.

Kingine ni kama ulivyosema kulikuwa na matarajio makubwa sana yaliyopita kiasi kuwa kutatangazwa ongezeko la mishahara. Sasa kwakuwa viongozi wa juu walikuwa wanajua walipaswa kuwaaandaa watu kulipokea hivyo. Hii ingefika mpaka kwa waandaa mabango yasomeke KAZI IENDELEE badala ya MISHAHARA JUU.

Kingine ambacho kingeweza fanyika pamoja na kuwa ni kigumu ilikuwa ni kwa mama kukwepa tukio lile na kumtuma makamu wake. Hii ni kwasababu inaonesha wazi alishafanya vikao na viongozi wa wafanyakazi na akawapa matumaini makubwa sana. Kila mtu jana alijua kikwazo cha kupanda mishahara alikuwa ni mwendazake. Hivyo ili kulinda angalau hadhi yake mama angetafuta sababu mapeema zaidi ya kutokuwepo jana huo msala umuangukie makamu. Hii ni kwasababu watu walikuwa na matumaini makubwa kuwa yeye ndiye mkombozi wa mkwamo wa kupanda kwa mishahara sasa wataanza kumuona hana tofauti na mwendazake ingawa mama alitumia lugha laini tofauti na mwendazake.
Mapema Sana wakati anaapisha wateule wake wa Mwanzo Rais Samia alisema kuna tatizo kubwa la Coordinations serikalini...

Leo nimeona hili tatizo kati yake Rais na waziri wake Jennista Mhagama...
Na lack of coordination Kwa ujumla kutoka IKulu kwenda chini Kwa watu Wengine ..

Kama Samia alikuwa anajua haiwezekani kupandisha mishahara leo alipaswa kuwaweka wasaidizi wake mapema ili waweze 'kuwaandaa watu kisaikolojia'mapema...

Ajabu leo wafanyakazi wameaminishwa kuna 'tamko'linakuja na hata waziri Jenista Mhagama alishadadia kabisa kuwa Leo kuna 'tamko'..

Hotuba za vyama vya wafanyakazi naamini IKulu ilizipata mapema na hata arrangements za leo walishirikiana kati ya serikali na Viongozi wa wafanyakazi..
Serikali ingeweza kabisa kuwaeleza mapema kuwa mishahara mwaka huu ni ngumu lakini mwakani itawezekana..

Hii ingepunguza 'expectation kubwa 'iliyokuwepo leo..na hali ya 'dissapointment' baada ya hotuba...

Nimejiuliza je Jesnista Mhagama alikuwa hajui Rais hatapandisha mishahara leo?
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi?..

Serikali ina vyombo vyake vya Ku leak taarifa kusudi..ili kupima upepo au kuwaandaa watu kisaikolojia...Leo mbona
Imekuwa tofauti?

Kama vile aliekuwa anajua kuwa mishahara haipandi Leo ni Samia peke yake...wakati kila mtu akiwemo waziri Jenista Mhagama walikuwa wana expect mishahara kupanda leo .tatizo lilikuwa wapi??

Samia ameanza kuwa 'anaogopwa'?

Kuna ukuta Kati yake na wasaidizi wake?

Kingine ilikuwaje Rais aseme hata yeye anakatwa kodi wakati haipo hivyo?
Mawaziri ,wabunge ,Ma Dc ma RC wameanza kukatwa kodi??..

Mbona kama Rais kaanza kuwa 'mkiwa'mapema? Kama wanaotakiwa kumsaidia hawamsaidii why asiwafukuze haraka?..
 
We acha mchezo, kwani katiba ndiyo imesababisha tusipate tamko? Watu tunataka nyongeza ya mishahara bwashee, hakuna anayekula katiba.
Ukiona chat inaongelea katiba juwa huyo ni mfuasi wa chadema. Wamekaririshwa hivyo.Katiba ya chadema ilichakachuliwa kipengele cha ukome. LISSU anajua lakini hawezi fungua domo lake
 
Ukiona chat inaongelea katiba juwa huyo ni mfuasi wa chadema. Wamekaririshwa hivyo.Katiba ya chadema ilichakachuliwa kipengele cha ukome. LISSU anajua lakini hawezi fungua domo lake

Hitaji la Katiba Mpya Tanzania sio hitaji la chama ama kundi fulani la watu. Ni hitaji la Watanzania wote.

Just take a moment and reflect on Warioba's commission work. Consider their data collection, collation analysis and their reports. Add on work of the special constitutional assembly.

Hizo kazi zote na yaliyotokana nayo tukisema yalikuwa ni mahitaji ya CHADEMA peke yake ama kundi fulani nchi mwetu tunakuwa hatutendi haki kwa akili zetu.

Ima hukuwa na ufahamu wa kufuatilia mchakato uliozalisha vitini na bango kitita pamoja na ripoti za Tume ya Warioba usione haya kuuliza wakubwa zako.
 
Umechachawa Mkuu au unachanganya madesa? Soma unielewe kabla hujakurupuka...
Usiwe mjinga kiasi hicho. Dicteta aliwapumbaza kwa Ujinga wenu akiwahadaa kuwa uchumi umekua na anatumia Pesa za ndani kujenga miradi wakati linakopa kwa wazungu.
Hotuba ya Mh Samia imesema uchumi umeshuka wew Kibwetele uwe makini usikurupuke tuu kuandika.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Tatizo watu mlikuwa mna yenu mliyotaka kuyasikia kwa mama, kuondolewa 6% ya heslb, PAYE kupunguzwa kwa 1% hilo si neno? Acheni ujinga wenu Rais hawez kumridhisha kila mtu ila angalau ameleta mwanga kuliko marehemu JIWE.

hiyo 6% isikie tu kwa jirani kama ingeendelea hivyo ungekukuta unastaafu utumishi wa umma na deni la heslb unalo
Kuna jamaa alilipa deni lake lote kupitia mwajiri wake kabla hata ya marekebisho ya Sheria yaliyoleta retention ya 6%. Lakini cha ajabu wamemdai retention amount mara 5 ya kiasi wanachodai hajakilipa wakati amewapelekea copy za salary slips zikionyesha alivyoanza na kumaliza kukatwa na mapengo waliyoyafanyia doubt. Bado wanasisitiza awasiliane na mwajiri wake. Angekuwa sio mtunza kumbukumbu mzuri ingekula kwake.
 
Tatizo letu watanzania ni kuropoka ovyo.tumepewa na tumeruhusiwa kusema lolote ili mradi tusivunje sheria.sasa hakumaanishi useme au uandike bila ya kuyapima.Sasa huyu mleta mada kapewa uhuru kamili wa kuandika anachokiona badala yake ETI anamshauri Mama Mh.Rais nini cha kufanya.

Mh.Rais wa awamu ya sita ni mkweli na muwazi.Tubadilike tumedanganywa miaka 6,na wote tulifyata mkia.tunasema kwa woga na kunonengezana.vyuma vimekaza.sasa tumejaaliwa Rais Mkweli na Muwazi tunaanza tabia zetu za kujifanya tunajua sana.keshatuahidi mwakani mambo ya mishahara yatarekebishwa hamtaki.tumedanganywa miaka 6 mmenyamaza kama waliopakwa super glue midomoni,mwaka mmoja tu mnalalama.

Acheni hizo.Kama huna cha kuandika bora unyamaze.Wananchi takriban wote Tanzania nzima wamefurahishwa na hotuba ya Mh.Rais Leo.Mama keep it up.UGANDA WANAKUTAKA PALE MAKERERE UNIVERSITY UKAWANOE KUHUSU UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI.WANAOMBA KUPATA KIONGOZI KAMA WEWE.
Umeandika nini hapa mkuu.

Mimi sitaki kutukana Ila unataka nitukane.
 
Back
Top Bottom