Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Mapema Sana wakati anaapisha wateule wake wa Mwanzo Rais Samia alisema kuna tatizo kubwa la Coordinations serikalini.

Leo nimeona hili tatizo kati yake Rais na waziri wake Jennista Mhagama. Na lack of coordination Kwa ujumla kutoka IKulu kwenda chini Kwa watu Wengine.

Kama Samia alikuwa anajua haiwezekani kupandisha mishahara leo alipaswa kuwaweka wasaidizi wake mapema ili waweze 'kuwaandaa watu kisaikolojia'mapema.

Ajabu leo wafanyakazi wameaminishwa kuna 'tamko'linakuja na hata waziri Jenista Mhagama alishadadia kabisa kuwa Leo kuna 'tamko'..

Hotuba za vyama vya wafanyakazi naamini IKulu ilizipata mapema na hata arrangements za leo walishirikiana kati ya serikali na Viongozi wa wafanyakazi. Serikali ingeweza kabisa kuwaeleza mapema kuwa mishahara mwaka huu ni ngumu lakini mwakani itawezekana..

Hii ingepunguza 'expectation kubwa 'iliyokuwepo leo..na hali ya 'dissapointment' baada ya hotuba.

Nimejiuliza je Jesnista Mhagama alikuwa hajui Rais hatapandisha mishahara leo?
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi?..

Serikali ina vyombo vyake vya Ku leak taarifa kusudi..ili kupima upepo au kuwaandaa watu kisaikolojia...Leo mbona
Imekuwa tofauti?

Kama vile aliekuwa anajua kuwa mishahara haipandi Leo ni Samia peke yake...wakati kila mtu akiwemo waziri Jenista Mhagama walikuwa wana expect mishahara kupanda leo .tatizo lilikuwa wapi?

Samia ameanza kuwa 'anaogopwa'?

Kuna ukuta Kati yake na wasaidizi wake?

Kingine ilikuwaje Rais aseme hata yeye anakatwa kodi wakati haipo hivyo?
Mawaziri ,wabunge ,Ma Dc ma RC wameanza kukatwa kodi??..

Mbona kama Rais kaanza kuwa 'mkiwa'mapema? Kama wanaotakiwa kumsaidia hawamsaidii why asiwafukuze haraka?..
 
Kazi ya Urais ni ngumu Sana.

Mama anatakiwa ajipange.

Naona mama ameanza kutafuta huruma kwa watu.

Tusiruhusu mama adeke, kipindi Cha majonzi kimeisha sasa achape Kazi bila woga Wala kinyonge.

Wananchi tunamtegemea.

Ila kitendo cha leo kinaonesha nchi na serikali imeanza kuwa dhaifu Sana na mda so mrefu atashindwa kuongoza.

Mama chukua hatua mapema kabla kivuli cha Magufuli hakijawaisha wanaokuzunguka na kuacha kabisa kufanya kazi.
 
Kuna kitu hapa nimekichunguza nikahisi, naona Rais na serikali yake kwa namna fulani kama wanataka kuzima tetesi zizazozagaa kwenye mitandao halafu baadae huwa kweli, ni kama wanajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao (siri).

Sasa nahisi wameona wasome upepo kwenye mitandao wakiona watu wanaaminishwa jambo fulani (baada ya taarifa kuvuja) wao waje tofauti ili kuwapunguzia wenye ushawishi mitandaoni (twitter in particular) waonekane waropokaji na wazandiki.

Japo inawezekana kweli mpango ulikuwa ni kuongeza mishahara ndio maana mpaka kina Mhagama walikuwa wanajua hilo, inawezekana mchezo umebadilishwa ghafla hata hao kina Mhagama hawakuwa na habari.
 
Ulitaka Vyama vya wafanyakazi wapangiwe hotuba na Ikulu ama?

Halafu Kumbuka Samia na Jenista ni Wana CCM, wanajua Watanzania mnataka nini kwa sasa huku wakigikiria Uchaguzi wa 2025

Huenda tamko alilokuwa anashangilia Jenista ndio hilo la kuongezewa mshahara mwakani..

Jenista ni Waziri mzoefu tena kwenye wizara za karibu na Ikulu, sidhani kama Kuna ambacho hakuelewa ila nahisi alikuwa anasherehesha tu kama unavyojua ccm kucheza na akili za Watanzania.
 
Kuna kitu hapa nimekichunguza nikahisi, naona Rais na serikali yake kwa namna fulani kama wanataka kuzima tetesi zizazozagaa kwenye mitandao halafu baadae huwa kweli, ni kama wanajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao (siri)...
Niliwaza hivo
 
Kuna kitu hapa nimekichunguza nikahisi, naona Rais na serikali yake kwa namna fulani kama wanataka kuzima tetesi zizazozagaa kwenye mitandao halafu baadae huwa kweli, ni kama wanajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao (siri)..
Mpango kwa bajeti ipi?
 
Ulitka Vyama vya wafanyakazi wapangiwe na hotuba na Ikulu.
Tamko lao lilipaswa kuwa changamoto zao au yale yaliyo ndani ya uwezo wao

Ukisema mishahara juu wakati mtoaji mwingine inatatanisha

Kwamba wakisema lazima atatekeleza?
 
Back
Top Bottom