Mkuu Luse, not necessarily, japo ukosoaji unahitaji kufanywa na manguli wenye weledi wa hali ya juu mfano Ukisema Tumpinge Magufuli ni Dikiteta kwa sababu tuu amezuia mikutano ya kisiasa, utaitwa mchochezi. Lakini ukisema kuwa Magufuli ni Dikiteta, ukaonyesha vifungu vya katiba vilivyotoa haki ya kukutana, ukaonyesha jinsi Magufuli alivyovunja Katiba, ukaonyesha mipaka ya mamlaka ya rais kuwa hana mamlaka ya kwenye kinyume cha katiba, kisha ukauliza alipopiga marufuku mikutano ya siasa alitumia mamlaka gani na kumalizia kuelekeza hatua za kumchukulia rais pale anapovunja katiba, amini usiamini Magufuli angeifuta kauli yake na media ingekuwa very safe, ndio maana sisi wengine tulisupport UKUTA but conditionally.Most media ambazo ziliikosoa serikali either zilifungiwa, kutishiwa au kuundiwa kesi
Mkuu Mkaruka TBC ni public media not government media ndio maana ina bodi yake independently hivyo inaweza kuikosoa serikali kama ilivyo BBC.
Sijazungumzia neutrality, nimesema public media inatanguliza mbele maslahi ya umma, kazi ya serikali ni kuutumikia umma, hivyo serikali ikikosea TBC ilipaswa kuwa na uwezo wa kuikosoa.
Paskali
Nashukuru sana kwa kunipa heshima ya kunijibu. Kwanza nashukuru umetupa track yako ya u media, ambayo imenisaidia ku confirm kuwa ni kweli wewe si muandishi wa habari. Kuwa host wa kipindi kinacholeta magwiji sio kuwa muandishi wa habari. Ni sawasawa na kumuita Zembwela Muandishi wa habari, kama tulivyomuuliza makonda, tuletee track yako ya uandishi wa habari, investigative na public interest, Maxence hajawahi kujiita muandishi wa habari, pamoja na kuwa na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuwakutanisha watu kuzungumzia habari. Zile habari sio zake, ni sawa na wewe, kiti moto hakikuwa investigative work yako, wale madiwani wa ccm wanaotoka kibaha na wazalendo wengine walikua wanatulietea scops tu, sio wewe. Pili nashukuru pia kuwa miaka yako 27 ya kukaa studio, not even press room, haitoshi kukuita muandishi wa habari. Ni sawa na kutuambia kuwa kwa kuwa unakaa karibu na mahakama basi wewe ni mwanasheria. Ndio maana karani wa mahakama aliyekaa mahakamani miaka 30 haitwi mwanasheria. Swala la Makonda haliweze kuwa your piece of literature, ni swala linalohusu integrity ya Taifa la Tanzania na kitu kinachoitwa Good Governance, sio mambo ya opinion zako, ulitakiwa ujue hata hilo kabla hujaingiza ujikombi wako, kwenye mambo serious. Once again, usipende kujikwaza sana na kujifanya mjuaji, neno linasema, ajikwezaye atashushwa, kwanini kama huna point lazima tu uongee, jitambue kuwa wewe sio opinion leader kwenye sekta ya media, kwanza sidhani hata kama unazo qualification zaidi tu ya ujanja ujana fulani, kama we bingwa weka vyeti vyako hapa tuone kama walau diploma ya uandishi, sana sana pengine una certificate ya Royal bahati kama una ya TSJ. (over) nakusubiri!
Unlee otherwise tundu lisu atakuwa anawasumbua mahakamani kila sikuWanabodi,
Declaration of Interest: Mwanzisha Mada ni Mwandishi wa Habari Mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii kwa miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu kama Mwandishi/Mtangazaji was Kujitemea kupitia kampuni ya PPR.
Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.
Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Stong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni ma Iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.
Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media?, jee tunao hao strong journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza? .
Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.
Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.
UK pia wana Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.
Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.
Paskali
Mawio mediaMost media ambazo ziliikosoa serikali either zilifungiwa, kutishiwa au kuundiwa kesi
Ukitaka strong media tumchukue /lisu/lema/zito/lijualikali/halima mdee/ tuwapeleka journalism institute ndipo tathnia ya habari itabadilikaWanabodi,
Declaration of Interest: Mwanzisha Mada ni Mwandishi wa Habari Mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii kwa miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu kama Mwandishi/Mtangazaji was Kujitemea kupitia kampuni ya PPR.
Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.
Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Stong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni ma Iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.
Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media?, jee tunao hao strong journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza? .
Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.
Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.
UK pia wana Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.
Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.
Paskali
Exactly.Waandishi wengi ni njaa kali na elimu za kuunga unga.
TBC inapoitete serikari na chama kilichopo madarakani si ndiyo hivyo kuwatetea wananchi? Serikali ni nini? wapo kwa ajili gani? so kama TBC haiweza kusimamia misingi ya upinzani kwa kuwa upinzani unaipinga serikali na serikali inafanya kazi ya kuwatumikia wananchi... iacheni TBC ifanye kazi yake ya kuelimisha umma.Unachokizungumza kuhusu TBC ni mambo ambayo tungetarajia iyatende kwa umma, lakini imegeuka ni chombo cha chama fulani na serekali na sio umma. Waandishi wa habari nao ugumu wa maisha umewageuza mateka wa tumbo.
Umesema sahihi sana.Naomba nichangie kwenye ili la utitiri wa vyombo vya habari.
Ingawa uwepo wa vyombo vingi vya habari unatoa fursa za ajira kwa wananchi wenzetu.Lakini ni wakati wa kuangalia sheria ya uanzishwaji wa vyombo hivi.Sasa hivi imekua kama "fasheni" kila mkoa kuwa na either kituo cha radio/tv. Lakini hazina impact yoyote katika kukuza maendeleo/maadili na uchumi wa sehemu husika!!
Hii inatoka either na ubora na umahiri wa wanahabari hawa.
Mkuu Tony Antony, kwanza asante kukubali kuwa hizo strong media zipo na hao strong brave journalists pia wapo tatizo ni tumbo. Unaweza kunifafanulia unamanisha nini? .stong=strong
nirudi kwenye mada mimi nadhani hizo media zipo hao watu wapo tatizo moja tuu linakuja jee hao watu wapo tayari kujitenga na tumbo???wapo tayari kusimama upande wetu na sio upande wao kwa maslahi mapana ya nchi yetu??nikitendo cha kujitathmini na kuamua uelekeo wa kufuata....
Naunga mkono hoja ila hizo serikali za kidomokrsia zina udikiteta wake. Kitu ambacho ni kweli kuhusu serikali zote za kidikiteta zina kiuka haki za binaadamu na ku suppress the media, hakuna freedom of expression. Tanzania bado hatujafika huko na hata Zimbabwe sio udikiteta bali ni African Democracy. Kama hoja ni ile ya Mugabe kung'ang'ania madaraka, tumependekeza Magufuli apewe muda zaidi
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Paskali
Mkuu Nimeguswa sana bandiko lako hili, this is very inspirational words. Mwanzo nilipanga to work out of media 2015 baada ya uchaguzi ikatokea mayai yangu yote nikayaweka kwenye kukapu kimoja, hivyo yakapasuka yote! .
Sasa nitawalk out 2020, hivyo in between najiandaa kuondoka kwa kuacha kitu. Kuna wakati nilijaribu kupitia JF, lakini nilipigwa sana madongo nika abandon.
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
Kwa sasa nazifanyia kazi some of these 10 TV Programs ideas kabla sijaagana rasmi na media.
rams.
3.1 Prog. 1-KWA MASLAHI YA TAIFA- TV Political Hard Talk Show- 30min
3.2 Prog. 2-SIRI YA MAFANIKIO – Profile Program-30 min
3.3 Prog. 3- TANZANIA NA MAENDELEO- Descriptive Program 30 min
3.4 Prog. 4- KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA- Feature Program
3.5 Prog. 5- KIPINDI MAALUM- Documentary in any specific Topic-30 min
3.6 Prog. 6- PPR NEWS EXTRA- 5 Minutes News extra "Habari Zaidi ya Habari na PPR.
3.7 Prog.7- IJUE KATIBA, SHERIA NA HAKI ZAKO-30 Minutes kuhusu Katiba, sheria na haki.
3.8 Prog.8- ITS ALL ABOUT POWERS THAT MATTERS -30 Minutes TV Program about power be it Supernatural, Devine, Psychic, Meditation,Mind Over Matter etc.
3.9 Prog. 9- TULIPOTOKA, TULIPO NA TUNAPOKWENDWA -30 Minutes Program about Trends za issues za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.
3.10 Prog.10- HIFADHI YA JAMII NI HAKI YAKO- 30 Minutes Program kuhusu hifadhi ya Jamii ni haki kwa wote sio privilege to some or favors.
Paskali
Mkuu Bujibuji kiukweli hili tukio la kifo cha Daudi Mwangosi kiliniumiza sana hadi niliamua kuachana kabisa na hii fani ya uandishi ila kitu kikishakuwa kwenye damu kukiacha ni vigumu sana.Hii nchi ambayo Polisi wanamuua mwandishi wa Habari kwa kumpiga Bomu hadharani, Vipi mwandishi akikamatwa kwa uficho jiulize atafanywa nini?
Mkuu Mdukuzi, mimi sio case study bali ni mwanzisha mada tuu.nikikuchukulia wewe kama case study am obliged to say NO big NO
Mkuu Kitumbotala, moja ya sifa kubwa ya strong media, ni zile media zinazojiendesha kwa funds kutoka vyanzo vingine ambazo hazitegemei matangazo. Clouds media sio tuu inategemea matangazo bali inajua kuzipanga vizuri na kuzicheza vizuri karata zake na mkono unaokulisha, ila kiukweli Clouds TV inafanya kazi nzuri zaidi ya ukosoaji kuliko TV nyingine yoyote kupitia kipindi chake cha 360 degreesKama Strong media zenyewe ni Clouds Fm ndio iikosoe serikali basi tumeumia
Makala zangu kuhusu wivu wenu dhidi ya mafanikio ya Makonda ni baadhi tuu ya my pieces of literature, kama huna uwezo wa kusoma "in between the lines, you just have completely missed the point.
Pole.
Paskali
Mkuu Prishaz, japo kuna kaukweli katika hili, ila pia kuna waandishi wa aina 3.Waandishi wengi ni njaa kali na elimu za kuunga unga.