Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Mkuu Paskali, najiuliza hivi ruksa ya kuikosoa/ kuishauri serikali anatolewa na waziri? Au ipo kwa mujibu wa sheria? Itafika siku atasema wewe wa gazeti la Uhuru, Mzalendo, Tbc, clouds, daily news ruksa. Wakosoaji/washauri wa kweli NO. Unataka 360 feedback halafu unatoa masharti kwamba unataka feedback nzuri tu, au pale unapojisikia. Hii si sawa ni upuuzi mtu mmoja kuamua when people should give feedback on the government performance. . Na hii tabia pia anayo mkuu mwenyewe na alitishia baadhi ya magazeti siku zao zinahesabika. Woga wa kukosolewa mbaya sana huwezi endelea kwa kusifiwa kufanya mazuri tu. Huko nikujikomba. .
Mkuu Jongwe, alichofanya Nape sio kutoa ruhusa bali kutoa tuu guarantee ya uwepo wa free Press. Hii ni kufuatia huu udikiteta uliopo hivyo media zinajikuta too supressed to the point of not being sure which is right and which is wrong ambapo the top hawata ipenda. Nidhamu ya woga.

Niliwahi kusema kuhusu the reign of terror hivyo hata media kujikuta ziko terrorized.
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.
Paskali
 
Devide ana rule, serikali yenyewe inachekelea tu vi utitiri vingi vya vyama, TV, Redio lukuki, nyingine ni kupiga mziki na majungu ya mtaani mwanzo mwisho, hence kutengeneza taifa la wasioelewa mambo ambao ni rahisi kutawaliwa maana hawana uwezo wa kuhoji.
Mkuu Fuso naunga mkono hoja.
Paskali
 
Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.



Paskali
I beg to differ!
Hakuna magazeti mawili wala tv mbili kubwa in the US
Matter of fact unapoongelea ratings basi hao CBS na ABC wanashika mkia kwenye upande wa news labda kama unaongelea reality shows na NFL

There are a number of the most elite newspapers in the US such as The Wall Street Journal, The Washington Post, NYT, LAT, Chicago Tribune, USA Today, Boston Globe, Houston Chronicle, Dallas Morning News etc

When it comes to TV you have Fox News, MSNBC, CNN, CBS, CSpan, ABC, Bloomberg, PBS, And even Weather Channel
 
Wanabodi,

Declaration of Interest: Mwanzisha Mada ni Mwandishi wa Habari Mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii kwa miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu kama Mwandishi/Mtangazaji was Kujitemea kupitia kampuni ya PPR.

Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.

Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Stong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni ma Iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.

Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media?, jee tunao hao strong journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza? .

Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.

Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.

UK pia wana Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.

Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.

Paskali
Serikali yetu ikiamua kusikiliza itasikiliza yeyote awe strong au weakling. Hawana kanuni. Ila kwa sasa wameamua hawataki kusikiliza mkosoaji yeyote. Maneno ya Nape ni debe tupu, hakuna ukweli wowote.
 
inawezekana zikawa zipo ila hazifanyi kazi ipasavyo ama mazingira hayaruhusu hata hivo media nyingi hazipo kwa ajili ya jamii husika au kuwaelimisha zaidi wananchi na kuishauri serikali hapa tz bali kwa manufaa na biashara zao wenyewe.tofauti na vyombo vikubwa duniani jinsi wanaripoti na kufanya kazi ukifatilia kwa makini mfano mzuri ni BBC then huwezi linganisha na media zetu kama TBC na nyinginezo mkuu.
 
Shida sio strong media wala weak media shida ni wanahabari mnanunulika sana. hamna strong journalists. ndio mana hata mkikosoa mnaonekana mmenunulika. Mswada wa habari utawaweka sawa. Hilo tu mkijirekebisha ndo mtaweza kukosoa serikali.
 
Kwanza si kweli kwamba Pascal ni mwandishi nguli wa habari, ni juzi tu tulikua na mkutano wa wahariri na Ali Mohamed wa Jicho pevu akasema kuwa pasipo Investigative Reporting hakuna uandishi wa habari. Na ndipo aliposema categorically kuwa media houses in Tanzania are Public Relations firms. This is exactly what the likes of Pascal Mayalla are, katuambia juzi alifanya invetigation ya mgomo wa madaktari, iko api hiyo report, eti wallikataa kuchapisha, ( zooo), haya walikataa wakina nani? Ripoti ya Mohamed Ali wa Jicho pevu kuhusu mauaji ya wakenya na state agencies, ime ripotiwa na Aljazeera. Huyu PR uchwala ndio huyo juzi anatuambia habari ya sisi kumuonea wivu Makonda, can you imagine? Njaa Njaa Njaa, vipindi vyake vya mashirikia ya umma, kuwapamba nakuwasifia ndio yeye anaviita uandishi wa habari? juzi kaambiwa yeye ni njaa mkuuu hakukosea anawajueni. Wakati wa Mswada wa Habari mlimiskie pale kwa Chilala akijamba cheche kusema eti muswada unamakosa kidogo, mchumia njaa hata siku moja hawezi kuwa shujaa. Acha wakina Kubenea waongee wewe, shut up and put up with the food you are putting on the table, acha wanaume wongelee ukombozi wa nchi hii, wewe mwenzetu endelea kuchekacheka kwenye tv
Mkuu umetema povu si siri
 
kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.

Paskali


Mhimili wa nne wa vyombo vya habari unaitwa the Fourth Estate, sio the Fourth Protocol, hebu usitie aibu zaidi waandishi wenzako ambao tayari mna sifa mbaya mno.

Mtu unasema ni mwandishi mstaafu halafu hapo hapo unadai kwa sasa unafanya kazi ya uandishi kwenye kampuni ya PPR. Sasa umestaafu kuandika nini, nyimbo za kizazi kipya? Uwezo wa kujieleza ni finyu kiasi cha kutisha.

Halafu UK hakuna "gazeti moja kubwa... Daily Telegraph." Kamba! Hilo sio kubwa na haliko peke yake. La kwanza ni Daily Mail, linauza kopi 10,636,000 kwa kila tolea, likifuatiwa na Daily Mirror, kopi 6,847,000. Daily Telegraph lako linafuatia kwa mbali mno na kopi 3,923,000. Usituandikie andikie vitu bila kufanya the simplest of research effort bana, unaamka usingizi unaenda kututype-pia mavitu kutoka kichwani mwako tu, vipi wewe Paskali wewe?

Na ukae ukijua interms of latesy ratings NBC ni kubwa kupita hizo ABC na CBS zako unazozijua wewe. Usituambie "kuna TV kubwa mbili Marekani... ABC na CBS." Double check your stuff before coming up here kuandika vitu vinavyosomwa na Watanzania tumetapakaa dunia nzima tuna ma exposure ya kila aina na ma gadget ya kufuatilia ukweli na uongo wa mataarifa within seconds.

"Fake News" yako nyingine uliyotupiga nayo hapa ni kwamba eti USA kuna magazeti makubwa mawili NY Times and Washington Post. Kamba kubwa.

Here is the latest circulation breakdown:

1. USA TODAY 2,301,917
2. NY TIMES 2,101,611
3. WALL STREET JOURNAL 1,337,376
4. LA TIMES 467,309
5. NEW YORK POST 424,721
6. CHICAGO TRIBUNE 384, 962

Hilo Washington Post lako halipo hata kwenye discussion linashindwa hata na ki tabloid cha NY Post. OK? Kwa hiyo acha kamba!

Unauliza kama Tanzania tuna mwandishi ambae akisema serikali itasikia, itabalidika. Hebu wewe nitajie mwandishi mmoja duniani ambae yeye akisema serikali yao inabadilika!

I mean, hauandiki kwa audience ya peasants and fish mongers wa kijijini kwenu Msakanyoka hapa! Poor crummy journalists we have! Daaaaah!
 
Mkuu Tony Antony, kwanza asante kukubali kuwa hizo strong media zipo na hao strong brave journalists pia wapo tatizo ni tumbo. Unaweza kunifafanulia unamanisha nini? .
Paskali
wengi wa waandishi wa habari wapo pale kwa maslahi ya mkubwa fulani ili vibarua vyao visiingie mchanga ni wachache sana wanathubutu kusema ukweli...mfano mzuri clouds kwa ujumla tuwe wa kweli tu wale watu sometimes wanaonyesha kubalance mambo lakini si kweli wana balance mambo ukiangalia kwa undani wameegemea upande mmoja ambao ndio unao waingizia zaidi pesa.....na huo upande unaufahamu upande wetu sisi ccm/serikali hiyo ipo wazi.....nikupe mfano mwingine kipindi cha dk 45 cha itv kinapoteza mvuto siku hadi siku,kwanini??kwakuwa akija wa upande ule ana minywa lakini akija wa upande wetu slope anabebwa kwa hoja mfu,hafifu......sidhani kama unanielewa yote hii inatokana na wale watu kuogopa vibarua vyao/matumbo yao kesho yatakuweje wakikaza ma kusimamia haki au kuweka uzalendo mbele kwanza???
 
Zile thread za Ndugu yako Bashite zimekuvunjia heshima sana Paskali
Mkuu Kalou, ni kweli, nyuzi za kumtetea ndugu yangu na homeboy wangu Bashite zimenivunjia sana heshima, ila faraja yangu ni mabandiko yangu yote kumhusu Bashite yalikuwa targeted na directional yaani ni mishale iliyolengwa kwenda kuhit specific targets, hivyo wale wote wenye akili za ki bashite bashite wameona mishale tuu ikiruka hewani kutokana na uoni wao hafifu hawakufanikiwa kuweza kuona hiyo mishale ililenga wapi au imeangukia wapi, hivyo kufikiri imepotelea hewani.

Paskali
 
Tatizo njaa wabahabari wengi bado wananjaa na wengine wanajitoa mhanga ili waonekane na wateuliwe kuwa ma dc au ded
Mkuu Bandu Bandu, japo njaa kweli ni tatizo kwa wana habari wengi ila sio wote. Si kweli ni wanahabari wote huandika kwa kujikomba ili wateuliwe, kuna wanahabari kibao nawafahamu ambao wanaandika just for the sake ya kuitumikia jamii na sio kujikomba kutafuta uteuzi.

Najitolea mfano mimi mwenyewe. Waandishi watafuta uteuzi kitu cha kwanza ni kujiunga na CCM na kuwa wanachama. Pili ni kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kupitia CCM au kuandika kwa kuegemea CCM, kuipendelea CCM au kujikomba komba kwa CCM.

Mimi sijawahi kujiunga na chama chochote, sijawahi kugombea nafasi yoyote ya uongozi hata class monitor, sijawahi kuipendekeza kwa yoyote kupalilia uteuzi.

Nikiwa Tambaza O-Level nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben na tulikuwa marafiki hadi kutembeleana. Nikiwa US alinipeleka kumsalimia Ben kwenye room yake kwenye hotel aliyofikia hivyo lengo lingekuwa uteuzi ningeisha lobby kitambo.

Nikiwa UDSM nimesoma na Riz 1 pale FoL na tunafahamiana. Kama ni ku lobby ningemfuata tu Riz anipeleke kwa Mshua.

Kila nikitembelea Chato nafikia kwa Magufuli hivyo kama ni lobbying ningeisha lobby kitambo! .

Wako Waandishi wengi tuu kama mimi ambao tunaifanya kazi hii ya uandishi kwa mapenzi na uzalendo tuu wa kuitumikia jamii na sio kwa lengo la kutafuta uteuzi ndio maana bado tuko kwenye fani hii ya kimasikini wakati we have all the opportunities elsewhere.

Paskali
 
Tatizo kubwa sana, tasnia ya habari kwa miaka mingi sana imevamiwa Na watu wasio Na sifa wala uweledi juu ya taaluma hiyo na kuonekana kama ni kazi ya kuendeshwa na vipaji vya watu kuongea ama kutangaza ama kutunga habari..watu wengi wamegeuza chaka lao...hizi media maarufu kabisa tz...wengi wa wahusika hawana taaluma hiyo. So to expect strong media rooms with this kind of fake journalist ni taabu...pia nchi zetu Na vyombo vyetu vya habari havisapoti habaritafiti or chunguzi bali ni vya matukio zaidi...Jeri Muro alijaribu hili...yakiyomkuta anajua mwenyewe....
 
Unachokizungumza kuhusu TBC ni mambo ambayo tungetarajia iyatende kwa umma, lakini imegeuka ni chombo cha chama fulani na serekali na sio umma. Waandishi wa habari nao ugumu wa maisha umewageuza mateka wa tumbo.
Mkuu Tindo kuhusu TBC ni kweli kwa sababu mimi niliwahi kuwepo pale, paperwork za TBC ni Public Broadcasting Station na sio government media. Ila kufuatia Mkurugenzi haombi kazi bali huteuliwa na rais, mtu ukiteuliwa haiwezekani tena ukakosa shukrani kwa aliyekuteua ukaruhusu akosolewe, hivyo kujikuta you're forced to pay lip services.

Ili kui transform TBC toka government media into public broadcasting station nafasi ya Mkurugenzi Mkuu lazima itangazwe wenye sifa waombe, wafanyiwe usaili kwa kueleza utafanya nini, hata kama mwisho wa siku Dr. Ayub Rioba ndio atashinda kwa sifa uwezo na vigezo, then atatimiza majukumu yake as a deserving DG na sio sasa kwa hisani ya Mteuzi! .

Kwa skilled manpower ya TBC na vifaa, wana best brains na best equipments hakuna media inaweza kushindana nayo. Japo kwa vifaa Azam wako juu kuliko TBC ila vichwa viko TBC tatizo ni motivation tuu. Azam wako Dar tuu, TBC wako Tanzania mzima.

Hili la waandishi mateka wa tumbo, japo ni kweli lakini sio wote.

Paskali
 
tulikuwa tunakutegemea wewe ila na wewe ukamezwa maana ulivyokuwa unamtetea bashite utadhani ulikuwa nae uko koromije.......................

inshort ni hakuna ata mmoja wote njaa na uwoga vimewajaa
Mkuu themanhimself176, hilo la utetezi wa Bashite, you just missed the point, nilitarget wasomi wa level fulani ya uelewa, but very unfortunately it was above kiwango chako cha uelewa. Pole.
Hii ya kusema hakuna hata mmoja wote ni njaa tuu, ni too general, sio kuwatendea haki wazuri wachache.

Paskali
 
85% ni wapiga pesa kama wewe nadhani. Kuna strong walaji wanaowatumikia wenye pesa kuwapamba kwenye media kwa malengo binafsi na si ya kitaifa
 
Ukitaka strong media tumchukue /lisu/lema/zito/lijualikali/halima mdee/ tuwapeleka journalism institute ndipo tathnia ya habari itabadilika
Mkuu Mc Cain, tukifanya hivyo tutakuwa tumetengeneza only one side of the coin kujenga waandishi mahiri wenye uthubutu. Swali linabaki ukiisha wapata waandishi wenye uthubutu, jee watatumia media ya nani yenye uthubutu huo wa kuikosoa serikali?.

Kama ni waandishi wenye uthubutu tupo tena tuko wengi tuu, tatizo tutautumia uthubutu huo kupitia media gani na ya nani? , TBC ya Magufuli? , ITV ya Mengi? , Star TV ya Diallo? , Channel Ten ya Rustam? ,Clouds ya Ruge?, etc.

Niliwahi kuishauri Chadema adui wake mkubwa anayeifanya isiingie ikulu sio CCM bali wananchi ambao ndio wanaoichagua CCM, hivyo wasipowafikia hao wananchi kwa wingi, ni kutwanga maji kwenye kinu.
Nikasema hawawezi kuitegemea mikutano tuu ya hadhara na kuitegemea media za wengine lazima wawe na media yake vinginevyo ikulu wataendelea kuisikia tuu.
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!
Paskali
 
Dictatorial govt kama Zimbabwe huwa HAZIKUBALI KUKOSOLEWA KAMWE...
•KUKOSOA HUWA NI JINAI KWA KWA MABAVU YA WATAWALA...

Naamini hakuna mtu wala serikali ambayo haitaki kukosolewa, ila tatizo kubwa kwa media ni negativity, na negativity wao wanasema ndiyo kukosoa.
Positive criticism ndiyo kukosoa maana nia ya kukosoa ni kujenga SI kubomoa.
Hivyo mwandishi wa habari au chombo cha habari kikihubiri chuki na ubinafsi hiyo SIYO kukosoa
 
Back
Top Bottom