Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,317
Wanabodi,

Declaration of Interest: mwanzisha mada ni mwandishi wa habari mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii as active media kwa zaidi ya miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu as passive media kama mwandishi/mtangazaji was kujitemea kupitia kampuni ya PPR.

Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama. Hii mihimili mitatu anatakiwa kufanya kazi kwa check and balance with each other. Ila pia kuna mihimili wa nne usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol or The Fourth Estate.

Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na independent stong media instutions zinazoweza kuwa critical, na tuwe na waandishi mahiri ambao ni independent strong journalists ambao ni ma iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.

Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media institutions?, jee tunao hao strong independent journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza?. Kwenye electronic media zetu, jee kuna vipindi vyovyote critical kama Hard Talk?, Larry King or hata Jicho Pevu kama kwa jirani zetu Kenya?. What is wrong with our media and our journalists?.

Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong independent journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.

Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wakati wa enzi ya kashfa ya Watergate walikuwa na magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.

UK pia walikuwa na Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.

Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.

Kazi kubwa ya ukosoaji wa constructive criticism ni ukosoaji wenye lengo la kujenga na sio ukosoaji wa kuzodoa, kudhalilisha na kubagaza, ukosoaji huu ufanywe kwa lugha ya staha na sio lugha ya maudhi, matukano au kebehi.

Media tukitimiza wajibu wetu ipasavyo, tutamsaidia sana rais Magufuli na serikali yetu kwa kuionyeshea madudu ya watendaji wake, hivyo kumrahishia kazi rais wetu, achukue hatua stahiki, na sio kusubiria hadi mambo yameharibika na wale jamaa zetu wampelekee rais taarifa zao, ndipo hatua zichukuliwe.

Paskali
 
Pamoja na mapungufu mengine yaliyopo, njanjaa zenu ni tatizo kubwa sana.

Waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari mmeshindwa kutambua kabisa watawala hawana urafiki wa kudumu na media bali wanachoangalia ni maslahi yao kupitia media namna gani yanalindwa.

Hata hivyo,kuna waandishi wachache wanaostahili pongezi kwa kusimamia maslahi ya Taifa.
 
Nape huyo huyo alikomalia sheria mbovu ya huduma za habari ipitishwe, halafu leo anaibukia jukwaani akisema tuikosoe serikali! Huu ni mtego.
Wanahabari walipaswa kupambana sheria ile isipite, maana ni hatari mno kuikosoa serikali kwa sheria ile, narudia tena, ni hatari sana.
 
stong=strong
nirudi kwenye mada mimi nadhani hizo media zipo hao watu wapo tatizo moja tuu linakuja jee hao watu wapo tayari kujitenga na tumbo???wapo tayari kusimama upande wetu na sio upande wao kwa maslahi mapana ya nchi yetu??nikitendo cha kujitathmini na kuamua uelekeo wa kufuata....
 
Pascal Mayalla ni nini kinatangulia kati ya kuwa na waandishi wa habari mahiri au vyombo vya habari huru. Jee inawezekana kukawa na vyombo vya habari huru lakini vikakosa waandishi wa habari mahiri? Au pia inawezekana kukawa na lundo la waandishi mahiri lakini kusiwe na vyombo huru vya habari?

Kama kwetu yote mawili yanakosekana, basi tuna safari ndefu sana kufika huko kwenye kukosoa unakokusema!!
 
GENTAMYCINE,
Mkuu Genta, hii too generalization kuwa huku sio kuwatendea haki pure journalists waliokuwepo na waliopo! . Sio kweli waandishi wetu wote kabisa wanafanya uandishi wa PR tuu na kukimbizana na those little brown envelopes!. Kuna media kama Gazeti la Citizen/ Mwananchi/Jamhuri/Mwahalisi/Mawio na Raia Mwema.

Tulikuwa na waandishi mashujaa kama Stan Katabalo.

NB. Naomba ku declare kuunga mkono waandishi kushikishwa bahasha halali za uwezeshaji.Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!
Paskali
 
Back
Top Bottom