Mdude Nyangali CHADEMA azuiwa kusafiri nje ya nchi na DCI. DCI kapata wapi mamlaka ya kuzuia mtu asisafiri?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,722
10,226
Hivi huu Ujinga bado upo? Au ndo 4R kwa kiwango cha standard gauge ? my foot !...Kumbe tuna wafungwa wanaotembea? DCI vipi kulikoni?

Au una kwazwa sana na watu wenye maoni Huru? Nimetaarifiwa kuwa umeweka zuio mdude Chadema asitoke nje ya Nchi eti?

Kwa hiyo anakifungo kwa Mujibu wa Ofisi yako? Au hujui wala kuheshimu haki za kikatiba za watu? Kosa gani analo tuhumiwa nalo?

Tuambie na toka wazi useme ni wananchi wangapi hiyo Mahakama yako ya mfukoni imewawekea Mazuio? Mwachieni Mdude Nyagali siyo Muhalifu.

Screenshot_20240129-102845_Lite.jpg
 
🦎 Hata Makonda amezuiliwa,😌ni mfungwa anayetembea😌.

Sasa kama Ruto hataki apitie huko je, bado mtasingizia ati ni 'ujinga bado upo'.

Kunywa Uji.
 
Kuna sheria nyingi za mkoloni kwenye vitabu vyetu na bado mpaka leo zinatumika, juzi hapa katika msamaha wa Rais, kuna hiki kifungu hapa

1706513788140.png
 
"Saa nane na dakika ishirini asubuhi"
Sijui maana yake nini. CHADEMA na CCM wanafanana sana
 
Hivi huu Ujinga bado upo? Au ndo 4R kwa kiwango cha standard gauge ? my foot !...Kumbe tuna wafungwa wanaotembea? DCI vipi kulikoni?

Au una kwazwa sana na watu wenye maoni Huru? Nimetaarifiwa kuwa umeweka zuio mdude Chadema asitoke nje ya Nchi eti?

Kwa hiyo anakifungo kwa Mujibu wa Ofisi yako? Au hujui wala kuheshimu haki za kikatiba za watu? Kosa gani analo tuhumiwa nalo?

Tuambie na toka wazi useme ni wananchi wangapi hiyo Mahakama yako ya mfukoni imewawekea Mazuio? Mwachieni Mdude Nyagali siyo Muhalifu.

Anatoroka kwenda wapi na huu ni msimu wa kilimo anatakiwa awe shambani na wanakijiji wenzake akizalisha mali.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mambo mengine ni upumbavu, huyo Mdude ana kitu gani cha maana cha kufanya huko nje ya nchi hadi wamzuie?
Tuwaulize hao waliomzuia,kwasababu nikama hawako serious na mambo ya msingi.wanaangaika na upuuzi tu.
 
Tuwaulize hao waliomzuia,kwasababu nikama hawako serious na mambo ya msingi.wanaangaika na upuuzi tu.
Pengine hata hakuna mtu aliyemzuia, serikali isimzuie Lissu mtu anayeweza kupangilia hoja zake na akaeleweka na kuungwa mkono na watu wenye akili ije imzuie mdude mpiga kelele? Usiwaamini sana hawa watu wa mitandaoni.
 
Mambo mengine ni upumbavu, huyo Mdude ana kitu gani cha maana cha kufanya huko nje ya nchi hadi wamzuie?
Serikali inakichonga wenyewe kinyago ambacho baadaye kitakuja kuwatisha wao wenyewe.

Huyu Mdude ajiongeze kidogo tu akale maisha Canada.

Mlionaye karibu mpelekeeni huu ujumbe wangu bahati haiji mara mbili.
 
Back
Top Bottom