Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,679
- 119,314
Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo: Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, kama unatolewa in good faith, kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, ukosoaji huu ukatoa ushauri wa the right thing to do, huitwa "constructive criticism" ambao ni ukosoaji mzuri, very healthy katika ujenzi wa taifa lolote la kidemokrasia linaloheshimu uhuru, haki na kufuata utawala wa sheria.
Serikali yoyote yenye nia ya dhati ujenzi wa taifa lake kwa kufuata misingi ya katiba nzuri na kuheshimu misingi ya haki binaadamu na utawala wa sheria!, inakuwa makini sana na hoja zozote zinazohusu katiba. Zikitokea kelele zozote zinazohusu ukiukwaji wa katiba au uminyaji wa demokrasia, serikali makini huzichukulia hoja hizi very serious, serikali yoyote inayopuuzia hoja za ukiukwaji wa haki zilizotolewa na katiba, then serikali hiyo ni ya ki imla, au ni ya kidikiteta!, na rais yoyote anayekiuka katiba aliyoapa kuilinda, huyo ni dikiteta.
Serikali nyingi za mataifa, zinazo heshimu katiba, na kufuata mfumo wa kidemokrasia na utawala wa sheria, zina mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Mihimili hii inatakiwa kuwa sawa kwa kufanya kazi kwa uhuru na kujitegemea bila kuingiliwa na Mhimili mwingine (independent) na wakati huo huo kila mhimili ukiwa ni mlinzi na mdhibiti wa mhimili mwenzake, (check and balance) ili mihimili mmoja usizidishe mamlaka yake na kuingilia mihimili mingine.
Kitendo cha rais wa nchi ambaye ni Mkuu wa mhimili mmoja wa dola, kutoa amri kwa mihimili mingine, ni kuingilia haki, uhuru na mamlaka za mihimili mingine, hivyo kukiuka ile kanuni ya "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances".
Nimehamasika Kuanzisha uzi huu, kufuatia mjadala wa amri ya rais Magufuli kuzuia safari za nje, kwa watumishi wa umma ambao pia imewakumba watumishi wa mhimili wa Bunge na watumishi wa muhimili wa Mahakama!.
Rais wa nchi ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa dola ambao ni serikali, mkuu wa mhimili wa Bunge ni Spika na mkuu wa mhimili wa Mahakama ni Jaji Mkuu!. Kitendo cha rais wa nchi kutoa amri ya mihimili yote kuomba ruhusa ya kusafiri nje kwa watumishi wa bunge na mahakama bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi ni kuingilia uhuru ,haki na madaraka ya mihimili mingine ambayo rais hana mamlaka hayo, huku ni kwenda kinyume cha utawala bora!, ambako mimi nakuita ni sehemu tuu ya udikiteta wa Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli!, kitendo cha watu wanaojua the principle of separation of powers, na checks and balance, hawakupaswa kulinyamazia hili!.
Rais wa nchi, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge, ni watu wenye hadhi sawa as wakuu wa mihimili, lolote likitokea kwa rais, hao wanashika wadhifa wa urais kwa mujibu wa katiba, hivyo kitendo cha kumfanya Jaji Mkuu na Spika wa Bunge kuomba kibali cha kutimoza wajibu wao kwa Katibu Mkuu Kiongozi, sio tuu kinakiuka kanuni hii ya sepaations of powers, pekee, bali kinawadhalilisha, na kuwafanya washindwe kufanya checks na kumbalance rais anapovuka mipaka ya mamlaka yake!, kwa mwendo huu Magufuli anao anza nao, huko mbele nani atathubutu kumcheck au kumbalance?.
Kwa vile katazo la rais kuzuia safari za nje bila kibali, limetolewa kwa nia njema kabisa ili kuzuia safari za nje zisizo na tija na manufaa kwa taifa, ili kutunza hadhi na heshma ya mihimili ya dola, rais kama mkuu wa mhimili mmoja wa serikali, alipaswa kuwaita wale wakuu wa ile mihimili mingine, Spika na Jaji Mkuu, na kuwaelezea nia yake njema katika kuthibiti safari za ulaji, ili spika na yeye atoe amri kama hiyo kwa wabunge na watumishi wa bunge kuomba kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge, na watumishi wa mahakama, kuomba kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama na ile amri ya rais iwahusu watumishi wa serikali kuu tuu na serikali za mitaa wakala na idara za serikali. Wabunge wapate vibali ofisi ya bunge na majaji na watumishi wa mahakama wapate vibali kwa Jaji Mkuu ili kuepusha kuingiliana majukumu kati ya mihimili hii!.
Watanzania tunapaswa kuwa waangalifu sana na hatua kama hizi na hili jambo sio la kulinyamazia hata kidogo, linabidi kukemewa kwa nguvu zote, kwa sababu madikiteta wengine wote duniani huanza hivi hivi kwa kulisupress Bunge, kisha atakuja kuisupress Mahakama, kisha ata supress the media na mitandao ya kijamii, na kumalizia na kuwa target individuals watakaonekana kuwa very vocal, or threat, kwa kuwatisha kama ilivyofanyika kwa Dr. Ulimboka, Kubenea na Kibanda, au msije kushanga, watu wakaja ku vanish into thin air, hata unywele usionekane!.
Kazi hii "doctrine of separation of powers", jukumu la mhimili wa serikali ni kuliwezesha bunge na mahakama kutimiza majukumu yake kwa kuipatia tuu pesa za uendeshaji na maendeleo, kwa mtindo wa "eyes on, hands off ", anachofanya rais Magufuli kwa mihimili hii ni "ayes on, hands on" kwa kutia mkono wake hadi jikoni, chumbani hadi kuchungulia uvunguni kwa wengine ambako huku ni kuuingilia.
Naomba kuwasilisha.
Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali

Mkuu Mahesabu hapa umeongea jambo la maana sana!, angalia nilivyowajibu hawa watu!.kuna mihimili mitatu
1. bunge
2. mahakama
3. serikali
Pesa za kuendesha ShUGHULI zao zinatoka HAZINA .
Kuna wizara mahsusi zinazosimamia Mihimili hiyo. Unapojitahidi kutenganisha pia jitahidi kuhusianisha utafikia tamati nzuri
Kwa ufahamu wako serekali ni nani????
Mtumishi wa watu na waserikali kunatofauti?
Ungesema ni kiongozi wa kisiasa hapo sawa!!

kama sio mtumishi wa serikali mbona analipwa mshahara na serikali,,, we bwege kweli
najiuliza waziri mkuu au waziri ni mtumishi wa watu au?pia najiuliza mbunge wa kuteuliwa na rais ni mtumishi wa watu pia?halafu nikiangalia kwenye payroll ya serikali nauona mshahara wa mbunge...mfumo wetu unanichanginyi
Wabunge ni watumishi wa umma.
Zuio la Rais Magufuli linahusu watumishi wa umma.
Sio kila anayelipwa na fedha za umma ni mtumishi wa serikali au mtumishi wa Umma, hata vyama vya siasa, watumishi wa vyama vya siasa, kikiwemo Chadema, wanalipwa kwa fedha za umma kupitia ruzuku, lakini hawa sio watumishi wa umma.sawa but analipwa na nani,