Hivi
Madame B na wewe upo hapa bize kuchangia hii mada ya michirizi na sio kumshauri huyo binti asepe?
Kama kuna kitu kwa mwenza wako na hukipendi kwanza jiulize swali hili;
Je, Kinaweza kubadilika? (Can I change it?)
Kama kinabadilika msaidie kukibadili na sio kumtupia yeye lawama. Kama kanenepa kidogo, amka naye asubuhi nenda naye mazoezi. Kama ni katabia kapya, kabla hakajakomaa kuwa active kumsaidia kukiacha. Kamwe usimpe mwenza wako mzigo wa, "Usipo..basi nita..." Mtu yeyote anayetumia sentensi hiyo ujue siku nyingi sana alishafanya maamuzi na keshachukua hamsini zake.
Kama hakiwezi kubadilika ujiulize, je, kinaathiri upendo wangu kwake? (Is it a deal breaker to me?) Kama ndiyo basi mweleze wazi na usepe. Kama siyo deal breaker kwako basi muombe Mungu akupe busara na hekima ya kukivumilia na kumchukulia mwenza wako kwa upendo ule ule.
Wewe dada Vero usimtese mdogo wako kisa sijui kamsomesha wala sijui alikuwa mwanaume wake wa kwanza. Mapenzi sio masharti.
Lakini ushauri mwingine kwa vijana wote walioko kwenye mahusiano na wanaotarajia kuingia kwenye mahusiano. Someni 1 Wakorintho 13:1-8. Hapo ndipo utapata maana halisi ya upendo. Hapo utaweza kujipima mwenyewe na kumpima mwenza wako. Hakuna kipimo kingine kizuri cha upendo kama hiyo mistari.
Kila la kheri.