Mdogo wangu aikosa ndoa kisa michirizi

Mdogo wangu aikosa ndoa kisa michirizi

Hakuna muaoji hapo jamaa anjua fika hiyo michirizi hamuwezi kuiondoa anasimamia hapohapo. Mwambieni kuna dawa ya kuondoa gharama yake iwe kubwa itakayo mkost akiwapa basi anania ya dhati. Vinginevyo ashauliza anajua haiondoki hatotuma pesa yoyote asilani.
 
Kwani ameshakosa kuolewa?
Uzi mzima ni lalamiko kwamba mdogo mtu kakosa kuolewa na huyo mtu shallow.

Hujui kusoma ama vipi?

Hata ambaye hajaufungua kasomabkichwa tu kaona hili.

Wewe umewezaje kusoma kichwa na kuninukuu na kutoona hili?
 
Akizaa atasema hamtaki kisa K inapwaya, amwache aende, love got no reason
 
Huyo sio muoaji labda ni gea ya kutaka kumpiga chini kiaina, kasha tafuna now anatafuta gia ya kutokea
 
SI NASKIAGA KUWA HIYO MICHIRIZI NI MAUTAMU AKA MAHANJUMATI???
 
Michirizi kisingizio, kawasitiri kuwaeleza ukweli, itakua kastuka mnasagana maana haiwezekani ukague mwanamke mwezio makalio, kiuno mapaja
 
mimi nakula balaa nina kilo mia sina hata mchirizi mmoja .kuna kitu alipaka wewe ongea nae tu vizuri
Siyo mkorogo michirizi ni asli ya mwili wa mtu mwingine hananumene wa kutisha lakini ananmichirizi,wala siyo mafuta wala mkorogo usikariri!
 
Ndo athari za kuzini kabla ya ndoa hizo, jamaa keshagegeda kakinai!!
Wala hakuna uhusiano wowote.mtu kukinai kupo tu,ata akioa kama ataamua kukinai atakinai na ni bora amekinai kabla ya ndoa kuliko kuingia kwenye ndoa ndo amkinai mwenzake kwasababu kama hatakua na uwezo wakumuacha atamnyanyasa.Kwaiyo hizo ni akili za mtu mwenyewe.
 
Bora kajionesha mapema, huyo si mume bali ni mwanaume hila, hafai kuwa mume.mwambie aachane nae mapema na akilazimisha kwenye hyo ndoa ataishi kama mtumwa.
 
Wakuu habari za w,keend,

Wakuu naombeni ushauri juu ya huyu mdogo wangu,

Mdogo wangu ana mchumba wake ambae alishafanya proses zote za ndoa, ilibaki kumsubiri dogo amalize chuo wafunge ndoa.

Sasa tatizo limekuja mdogo wangu baada ya kumaliza chuo, amejiachia sana yaani kanenepa alafu kawa na michilizi kiunoni mpaka kwenye makalio na inavyoelekea inaendelea kumtoka maana anaviashiria kama inaendelea kumtoka hadi mapajani.

Sasa baada ya jamaa kumuona hivyo mchumba wake anamwambia jitahidi hiyo mistari ikutoke hangaika kama ni gharama nitalipia lakini hiyo mistari siitaki kuiona mbona wakati unasoma ulikua modo huna hiyo mistari kama ikishindwa kutoka mimi na wewe basi, mimi hiyo mistari inanitisha.

Dogo kanisimulia nikazani utani, kumbe jamaa yupo serious. Sijakaa vizuri huyu jamaa ambae ni shemu wangu akaniibukia mpaka Tanga. Anasema nipo serious na hii inshu jitahidi ukae na mdogo wako umsaidie apake dawa gani ili kuondoa hiyo mistari alafu ni mingi.

Wakuu dogo week ijayo anakuja kwangu nimsaidie maana mimi ndo dadaake mkubwa, alafu harusi ilipangwa mwezi wa na nane na jamaa kama hivyo haelewi somo.

Msaada please kuinusuru ndoa ya mdogo wetu.
Shkamoo madame Velo[emoji12]
 
Kuna daawa ya mchiriz ila hata mi binafusi sipendi mchiriz wakati mwingine inaxidi na inakera
 
1: Atumie mafuta ya parachute......
2: asijiachie achie bado binti akizaa si atakua pundamilia kabisa?
3: hakuna muoaji hapo huyo ni mtmbaji tu
 
Back
Top Bottom