MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,214
- 43,740
Wakuu leo nimeona niandike uzoefu wangu mdogo kwenye hii biashara ya duka la nguo. Huenda ikamsaidia mtu fulani humu atakayesoma uzi. Kwanza kabisa hii biashara sikuwahi kuota ipo siku nitaifanya kwa sababu nilikuwa siielewi na pia kuiogopa kwa sababu marafiki zangu walikuwa wakianzisha na ndani ya muda mfupi usiozidi mwaka hufunga biashara. Ilipofika zamu yangu nikajikuta nimeanza bila kupenda. Yafuatayo ni mambo niliyojifunza;-
1. Pamoja na kwamba duka la nguo ni muhimu liwe la kuvutia ila tafadhali sana usipoteze pesa zako nyingi kwenye decorations. Weka pesa nyingi kwenye kununua mzigo. Kama mtaji wako ni 10m basi 9m iwe stock na 1m au chini ya hapo iwe decorations na kuweka duka sawa kimpangilio.
2. Kama ilivyo kwa biashara nyingine jitahidi sana uwepo muda mwingi dukani.
3. Kwa kuanzia anza na nguo aina mbalimbali kidogokidogo kama samples. Hii itakusaidia kitu gani kinapendwa zaidi na wateja ili uweke nguvu hapo. Kwa mfano mimi nilianza karibu na kila aina ya nguo za kiume na za kike ila nikaishia kupiga chini karibu kila kitu na kubakiwa items zisizozidi aina 5 tu dukani. Kuna wengine huanza na kila kitu ila baadae mtu anabakiwa labda na suruali za kiume tu.
4. Sio lazima ukimbizane na trends. Kuna nguo ambazo ni timeless yaani inaweza ikauzwa hata mwaka 2040. Kwa mfano suruali za jeans plain kiume na kike huwa hazipitwi na wakati kirahisi. Hata plain tshirts hazipitwi na wakati. Kuwa tu smart kwenda na fashion haraka wakati ndo zimeanza kuvuma.
5. Biashara ya nguo ina ushindani mkali sana kwahiyo ili uwe salama na ukue jitahidi kuchukua faida uongeze kwenye mtaji. Vinginevyo hiyo faida ndogo inaweza potea.
6. Weka bei reasonable za kutomuumiza mteja na kutojiumiza wewe. Kwa sasa nimeona watu wengi wanajiumiza kwa kuweka bei ndogo kiasi kwamba akija kutoa gharama zake anajikuta kaanza kula mtaji. Hii inasababishwa na kutazama wengine badala ya kujitazama yeye. Usiige mkinga anayeagiza kontena zima na kuweka faida ya Tsh 500 kila suruali ukadhani utaweza.
7. Kila siku jifunze kuhusu biashara yako ikiwemo kutafuta machimbo ya bei nafuu zaidi. Hujafunga ndoa na supplier wako kwahiyo ukipata chimbo la bei rahisi nenda.
8. KUWA MWAMINIFU KWAKO WEWE BINAFSI, WATEJA, SUPPLIERS, WASAFIRISHAJI na wote wanaohusika na biashara yako. Ukiwa mwaminifu utaanza kupata mizigo ya malikauli ikakusaidia.