Mdogo mdogo dini zitakosa wafuasi

Mdogo mdogo dini zitakosa wafuasi

mtoa mada ungekuwa ulaya ungekuwa mbali sana,

watu dini tumeletewa lakini tulivo bize hadi WARABU NA WAZUNGU wanashangaa,

juzi kati nlikutana na binti wa Ki-Dutch tulikuwa tunabadilisha mawazo nikamuuliza huko kwao dini wanaichukuliaje?

akadai kwao wanajali kazi zaidi kwanza, swala la kwenda church inabaki ni imani kwa mtu, uende usiende hakuna anayekuuliza,

ila ameshangaa sana hapa TZ watu walivo makini na dini kuliko kazi,
Duh! hiyo sio mchezo kabisa,vp na kwa waarabu nao wanaichukuliaje dini waliyotuletea?
 
Ni kweli mimi nina miaka kadhaa sikanyagi nyumba yoyote ya IBADA kwa ajili ya maudhi ya Viongozi wa dini ndani nyumba hizo za ibada haiwezekani leo sadaka itolewe wazi wazi huku waumini wakipiga makofi au Furaha, Yani ni Panakera kabisa Ukiwa na Hela nyumba za Ibada ni rafiki ila Fulia sasa hapafai kabisa
Labda kama unasali ktk vile vikanisa vya watu binafsi ie kwa 'mlima wa baridi' , 'kanisa la ulazima na ufukuaji', 'kanisa la kikobe' nk
 
We fikiria Mungu mmoja ila eti kuna aliowapa mamlaka ya kuoa mke mmoja tu na wengine zaidi ya mmoja, sasa ni kweli Mungu wetu ana upendeleo ama ni janja tu za watu fulani na masrahi yao?

Tena fikiria, Mungu mmoja lakini dini ziwe tofauti, yaani muumba awe mmoja lakini eti huku kuna Mtume na kule yupo Yesu ila Mungu ni mmoja ...so what?

Inashangaza zaidi kumbe hata Mtume/Yesu ni zaidi ya mmoja kwani hata wafuasi wao kila mtu ana Yesu/Mtume wake, wanabaguana kama nini lakini utasikia wote ni wa Mtume/Yesu.

Hivi hii mizengwe ni kwa faida ya nani, hivi kweli Mungu anahusika kwenye haya ama ni mipango tu ya makundi fulani?

Ninachokijua mie ni kwamba kila mtu kuna kitu anachokiamini toka akizaliwa, dini inaweza kufa lakini imani ya mtu kwamba yupo Mungu hiyo itasalia daima milele
 
Mkuu kwanza dini zinafanya watu wawe wavivu,

Km unaambiwa usiyasumbukie ya dunia yatajisumbukia yenyewe maana yake nn

Unaambiwa Mali na fedha za dunia uzihesabu km mavi, utapata wapi muda wa kuhangaika kuzitafuta?

Unaambiwa usihangaike na kesho itajihangaikia yenyewe
Mbona sijaelewa hapo,kama dini inafanya watu kuwa wavivu na kukosa muda wa kutafuta hela je,hiyo michango huwa wanachanga mawe?

Maana kama wamekosa muda wa kutafuta hela na huziona kama mavi,wangewezaje kupata hela za michango?
 
huwezi kumthibitisha Mungu kwa kumshika, kikubwa unatakiwa utambue na uamini moyoni mwako kwamba, kuna nguvu iliyo nje ya uwezo wako, nguvu ya asili ambayo ni MUNGU mwenyewe
Haya maelezo wewe umeyatoa wapi,vp mwengine nae akiwa na maelezo tofauti na haya?
 
Dini haitakufanya wewe umwone Mungu, sahau

Ili siku moja ufike kwa Mungu watakiwa ufanye hata:
1. Uamini akilini mwako kwamba kuna nguvu iliyo nje ya uwezo wako

2. Hakikisha unachukia na kuachana na uovu wote maishani mwako

3. Tenda haki, simamia haki, tetea haki kwa nguvu zako zote maishani mwako

4. Wapende binadamu wte bila ya kuwabagua na uwe tayari kuwasaidia pahala unapojiweza

5 na mwisho, ipende kazi na uifanye kwa bidii kuhakikisha unaifanya dunia hii kuwa makao ya wanadamu, kupitia kazi ya mikono yako Mungu atakubariki
Na usipofanya hayo inakuaje mkuu?
 
We fikiria Mungu mmoja ila eti kuna aliowapa mamlaka ya kuoa mke mmoja tu na wengine zaidi ya mmoja, sasa ni kweli Mungu wetu ana upendeleo ama ni janja tu za watu fulani na masrahi yao?

Tena fikiria, Mungu mmoja lakini dini ziwe tofauti, yaani muumba awe mmoja lakini eti huku kuna Mtume na kule yupo Yesu ila Mungu ni mmoja ...so what?

Inashangaza zaidi kumbe hata Mtume/Yesu ni zaidi ya mmoja kwani hata wafuasi wao kila mtu ana Yesu/Mtume wake, wanabaguana kama nini lakini utasikia wote ni wa Mtume/Yesu.

Hivi hii mizengwe ni kwa faida ya nani, hivi kweli Mungu anahusika kwenye haya ama ni mipango tu ya makundi fulani?

Ninachokijua mie ni kwamba kila mtu kuna kitu anachokiamini toka akizaliwa, dini inaweza kufa lakini imani ya mtu kwamba yupo Mungu hiyo itasalia daima milele
Ni kweli mungu mmoja ila binaadamu wana rangi tofauti weusi na weupe,mungu mmoja ila hali za maisha za watu ni tofauti wengine masikini wengine matajiri.
 
Kuna jamaa kafungua kanisa la walevi hap dom anajiita nabii Tito huko church watu wanachapa bia tuu
 
Uislaam tu ndio unapata nguvu duniani Kote, ulaya na marekani watu wanajifunza na kuelewa ni dini isiyo na Shaka.
Hao wazungu wakishajichanganya humo baadae utaona watakavyoanza kuingiza madudu yao humo
 
Ni kweli mungu mmoja ila binaadamu wana rangi tofauti weusi na weupe,mungu mmoja ila hali za maisha za watu ni tofauti wengine masikini wengine matajiri.
Kama tofauti zimewekwa na Muumba hizo hazina shida mfano kuzaliwa wapi ama wa kabila gani hakuna aliyeomba ama kuamua yeye ila haya yanayopangwa na binadamu mwenzetu kwa ajiri ya masrahi yake kwanza ni kuleta mifarakano na yanatakiwa kupigwa chini iwezekanavyo. Mie nikifa ni mali ya Mungu yeye ndo atajua hatma yangu na si dini zetu. Matendo na wema wangu ndo vitakavyoniokoa siku ya kihama
 
Mungu ni mwema niko na afya na mwenye nguvu, nakusalimuni nyote popote mlipo, amani iwe nanyi.

Naona mdogo mdogo watu wameanza kustuka kuhusu hizi dini, kwamba michango imekuwa mzigo makanisani, mpaka mtu unaogopa kwenda km huna hela,

Sadaka tu vikapu kibao, na amini si muda mrefu kutoka sasa itachukua watu watakuwa wameelewa kwamba dini zilikuja kwa makusudio Fulani kwa faida za watu au kikundi Fulani.

Wale wote ambao walisha shtukia dili za hawa watu nakuombeni tuendeleee kuuambia ulimwengu juu ya dini, kwamba dini ni biashara km biashara zingine tu

Dini sio Mungu na Mungu sio dini,

Dini ilikuwa ni mawazo ya watu tu kuhusu Mungu.

Chukueni hatua
Nashindwa kuelewa kwanini watu walipie sadaka mahubiri ya siasa na majungu makanisani
 
Wewe utachuja n.a. kupauka,dini zitasimama
Hivi Leo Mungu akiondoa kifo na aruhusu kila kitu binadamu anachokihitaji akipate wakati wwte, hivi kuna binadam yeyote atakayeenda nyumba ya ibada kuomba? Akienda ataomba nini?
 
Na usipofanya hayo inakuaje mkuu?
Si lazima uyafuate mkuu

Kwan hata hivyo kunawasioamini uwepo wa Mungu

Kwa wale wanaoamini wanaweza kuyafuata kwa hiari wala hawatashikiwa bunduki na kukamatwa na MTU,
 
Back
Top Bottom