Mdogo mdogo dini zitakosa wafuasi

Ndugu kama unaona unakwazika na kutoa ktk kanisa lako, acha kwenda au kutoa ila usiaminishe wengine upumbavu wako.

Kumbuka kuna majengo ya makanisa kama vile ya Catholic na Lutheran (sio vile vikanisa/vioski vya watu binafsi) unasali au kupata huduma mbalimbali yalijengwa kwa michango ya watu kama mie na wewe kwa kujitolea. Sasa kama unaona kuchanga ni mateso kwako acha na ishi utakavyo hulazimishwi.
 
Kanisa moja nilitembelea kulikuwa na changizo wengi walitoa ahadi za mapesa na wengine wakatoa live wengi tuliwapigia makofi na kushangilia kw jinsi ahadi zilivyokuwa zilkitolewa ndg mmoja akatoka mbele akasema yeye atajitolea kufunga na kuomba ili watu wote walitoa ahadi wafikie malengo yao I'll kazi ya Mungu isikwame mchungaji akasema hapa hakuna maombi Wala Nini hapa ukisimama ni hela ama ahadi ya hela tu...! Ajabu yule mtu hakupigiwa makofi Wala kushangilia! Ndiko tulikofika
 
Mungu ni mwema niko na afya na mwenye nguvu, nakusalimuni nyote popote mlipo, amani iwe nanyi.

Naona mdogo mdogo watu wameanza kustuka kuhusu hizi dini, kwamba michango imekuwa mzigo makanisani, mpaka mtu unaogopa kwenda km huna hela,

Sadaka tu vikapu kibao, na amini si muda mrefu kutoka sasa itachukua watu watakuwa wameelewa kwamba dini zilikuja kwa makusudio Fulani kwa faida za watu au kikundi Fulani.

Wale wote ambao walisha shtukia dili za hawa watu nakuombeni tuendeleee kuuambia ulimwengu juu ya dini, kwamba dini ni biashara km biashara zingine tu

Dini sio Mungu na Mungu sio dini,

Dini ilikuwa ni mawazo ya watu tu kuhusu Mungu.

Chukueni hatua
Neno lenyewe LA WAFUWASI linatokana na maneno WAFU +WAASI Kwa mujibu wa biblia wanajulikana kama CHUKIZO LA UHARIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU
 
Punguzeni michango ili kila mmoja aweze kuja na kukisikilizeni
Sio issue ya Michango, ni wewe na Mungu wako. Kama Michango ni zaidi ya Mungu wako utaacha kuenda na kama Mungu wako ni juu ya michango hutaona shida wala aibu.

Ni kweli taratibuuuuu za dini wakati mwingine zinakwaza lakini hazitakiwi kuondoa focus yako kwa Mungu kwa maana dini sio mpango wa Mungu bali ni taratibuuu za wanadamu kumtafuta Mungu.

Ukikuta dini inakwaza upendo wako kwa Mungu wako I question your sprituality. Ni kupambana nao maana dini ni mfumo tuu na unaweza kuwa kikwazo kwako kumtafuta Mungu.
 
Kanisa moja nilitembelea kulikuwa na changizo wengi walitoa ahadi za mapesa na wengine wakatoa live wengi tuliwapigia makofi na kushangilia kw jinsi ahadi zilivyokuwa zilkitolewa ndg mmoja akatoka mbele akasema yeye atajitolea kufunga na kuomba ili watu wote walitoa ahadi wafikie malengo yao I'll kazi ya Mungu isikwame mchungaji akasema hapa hakuna maombi Wala Nini hapa ukisimama ni hela ama ahadi ya hela tu...! Ajabu yule mtu hakupigiwa makofi Wala kushangilia! Ndiko tulikofika
Aisee alaaniwe huyo mchungaji wenu
 
Punguzeni michango ili kila mmoja aweze kuja na kukisikilizeni
Kama kwel unamtafuta Mungu aliye mkuu michango sio tatizo Mungu huwa anaonekana sana katka utoaj kwa sababu yeye Mungu mwenyew natural yake n utoaj huwez kubalikiwa kama sio mtoaj tatizo watu weng wanaenda makanisani sio kwa ajil ya kumtafuta Mungu ndio wakisikia michango wanaona sio sawa
 
Ni kweli mimi nina miaka kadhaa sikanyagi nyumba yoyote ya IBADA kwa ajili ya maudhi ya Viongozi wa dini ndani nyumba hizo za ibada haiwezekani leo sadaka itolewe wazi wazi huku waumini wakipiga makofi au Furaha, Yani ni Panakera kabisa Ukiwa na Hela nyumba za Ibada ni rafiki ila Fulia sasa hapafai kabisa
 
Kanisa moja nilitembelea kulikuwa na changizo wengi walitoa ahadi za mapesa na wengine wakatoa live wengi tuliwapigia makofi na kushangilia kw jinsi ahadi zilivyokuwa zilkitolewa ndg mmoja akatoka mbele akasema yeye atajitolea kufunga na kuomba ili watu wote walitoa ahadi wafikie malengo yao I'll kazi ya Mungu isikwame mchungaji akasema hapa hakuna maombi Wala Nini hapa ukisimama ni hela ama ahadi ya hela tu...! Ajabu yule mtu hakupigiwa makofi Wala kushangilia! Ndiko tulikofika
Nimeogopa sana!
 
mtoa mada ungekuwa ulaya ungekuwa mbali sana,

watu dini tumeletewa lakini tulivo bize hadi WARABU NA WAZUNGU wanashangaa,

juzi kati nlikutana na binti wa Ki-Dutch tulikuwa tunabadilisha mawazo nikamuuliza huko kwao dini wanaichukuliaje?

akadai kwao wanajali kazi zaidi kwanza, swala la kwenda church inabaki ni imani kwa mtu, uende usiende hakuna anayekuuliza,

ila ameshangaa sana hapa TZ watu walivo makini na dini kuliko kazi,
 
Uislaam tu ndio unapata nguvu duniani Kote, ulaya na marekani watu wanajifunza na kuelewa ni dini isiyo na Shaka.
Japo inapigwa vita ila ndo kimbilio la wengi
na ndo dini pekee iliyo smart...haina mashaka.
 
Kanisa moja nilitembelea kulikuwa na changizo wengi walitoa ahadi za mapesa na wengine wakatoa live wengi tuliwapigia makofi na kushangilia kw jinsi ahadi zilivyokuwa zilkitolewa ndg mmoja akatoka mbele akasema yeye atajitolea kufunga na kuomba ili watu wote walitoa ahadi wafikie malengo yao I'll kazi ya Mungu isikwame mchungaji akasema hapa hakuna maombi Wala Nini hapa ukisimama ni hela ama ahadi ya hela tu...! Ajabu yule mtu hakupigiwa makofi Wala kushangilia! Ndiko tulikofika
Alikuwa amevurugwa tu huyo.
 
Kuna msemo wanasema kutoa ni moyo sio utajiri. Sidhani kama unapangiwa kutoa sadaka. Wewe just chenji buku, weka shilingi mia mia na hamsini hamsini, then ikifika muda wa sadaka unaweka tu bila kuuliza
 
Back
Top Bottom