Mdogo mdogo dini zitakosa wafuasi

Mdogo mdogo dini zitakosa wafuasi

Ni kweli mungu mmoja ila binaadamu wana rangi tofauti weusi na weupe,mungu mmoja ila hali za maisha za watu ni tofauti wengine masikini wengine matajiri.
Wewe ndo unasema ila dini zinaamini ktk miungu wengi, ingalikuwa wanaoamini kwa Mungu mmoja wasingalitofautiana kiimani
 
Nashindwa kuelewa kwanini watu walipie sadaka mahubiri ya siasa na majungu makanisani
Mkuu ktk chama chochote michango ni kawaida kwa ajili ya uendeshaji wa baadhi ya mambo ya chama husika

Tatizo hawa wenzetu hiyo michango ambayo wameipa jina LA sadaka wanaichangisha vibaya
 
Kama tofauti zimewekwa na Muumba hizo hazina shida mfano kuzaliwa wapi ama wa kabila gani hakuna aliyeomba ama kuamua yeye ila haya yanayopangwa na binadamu mwenzetu kwa ajiri ya masrahi yake kwanza ni kuleta mifarakano na yanatakiwa kupigwa chini iwezekanavyo. Mie nikifa ni mali ya Mungu yeye ndo atajua hatma yangu na si dini zetu. Matendo na wema wangu ndo vitakavyoniokoa siku ya kihama
Mkuu ulikuwa unashangaa ni vp kuwe na tofauti za mambo yenye kuhusu mungu wakati mungu ni mmoja tu! ndipo nami nikakutolea mifano mengine ambayo inatofautisha binaadamu ila mwisho wa siku mungu ni yule yule mmoja hakuna mungu wa weusi wala weupe.

Na hivyo hauoni kuwa huku kutofautiana bado haifanyi kuwa yote yanayoelezwa ni mambo tu yaliyotungwa na watu na hakuna yaliyo ya ukweli?
 
Km unayo tofauti nawe yaseme,
Hoja yangu si kuhusu mimi nina maelezo mengine au sina,ila nimeuliza hayo uliyoyaeleza yenye kuhusu mungu umeyatoa wapi? maana anaweza akaja mwengine na maelezo tofauti na yako je,tumsikiliza nani?
 
Si lazima uyafuate mkuu

Kwan hata hivyo kunawasioamini uwepo wa Mungu

Kwa wale wanaoamini wanaweza kuyafuata kwa hiari wala hawatashikiwa bunduki na kukamatwa na MTU,
Si suala la kushikiwa bunduki ila matokeo ya kufanya au kutokufanya hivyo ni yepi?
 
Wewe ndo unasema ila dini zinaamini ktk miungu wengi, ingalikuwa wanaoamini kwa Mungu mmoja wasingalitofautiana kiimani
Kwanini wasingetofautiana?

Kwani unajua imekuaje hadi wanatofautiana? mfano leo kunaweza kuwa na maelezo tofauti kuhusu mtu fulani,lakini hali hiyo haifanyi kuwa hayo maelezo yote ni uongo.

Hivyo kuna sababu zilizofanya kukawa na hizo tofauti ila maelezo ya kweli lazima yawepo.
 
Back
Top Bottom