Rayvanny wa jamiiForums
Senior Member
- Apr 7, 2023
- 132
- 350
Ni ukweli usiopingika kwamba Kampuni ya kalyanda ni kampuni iliyotapeli maelfu ya watanzania mtandaoni, lakini licha ya kufanya uhalififu huu mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali.
Hivi inaamana kwamba hawa wezi wa kalyanda wameshindwa kufahamika au hawatambuliki jibu ni hapana sasa kwanini wahusika wa utapeli mpaka leo hawachukuliwi hatua za kisheria?
Wakati Kampuni hii ili tangazwa mpaka kwenye vyombo vya habari ikiwemo ITV na sura za wahalifu hawa zikiwa zinaonekana sasa kwanini hawachukuliwi hatua za kisheria au kukamatwa kwao mpaka sasa inamaana jeshi la polisi linawaogopa?
(pichani ni ITV wakitangaza kampuni ya kalyanda)
(pichani ni baadhi ya sura za matapeli wa kalyanda walio waibia maelfu ya watanzania)
Kampuni hii pia ya kalyanda ilisajiliwa mpaka (BRELA) lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa
Vipi mdau unamaoni gani kuhusiana na hili suala?
#nyumayapazia