MDAHALO: Tundu Lissu vs Job Ndugai kama ilivyoonyeshwa na Star TV

Nimekwambia as psychoanalytic nimemjaji kutokana na argument zake, sasa ww unataka solid evidence gani? Na kwa nyongeza nmegundua tatzo lingne kwako nalo ni purisphobisias ambalo linatokana na low iq ambapo mtu anakuwa mzto kuelewa
Mkuu, hata siku moja usitoe conclusion kwenye forum kama hii based on a single observation. Kuna wengi ambao ni south pole (left-hand) na ni watu muhimu na mashuhuri kabisa hapa ulimwenguni. Labda nikukumbushe tu, Barack Obama na Bill Clinton wote ni left-handed; lakini nadhani si wapuuzi kama ulivyotoa conclusion hapo mwanzoni. Inabidi uombe samahani watu wote ambao ni left handed, otherwise naku-report kwa abusive language.

Lisu na ndugai wanauhusiano toka lini mkuu? unaposema na mwenzake una maana gani?

umeongea kama mtu ambaye hakwenda shule unachoponda ndicho ulichofanya hapa una chuki na LISU wewe hacha makundi

una anzisha vita ndani ya chama kwa manufaa ya nani?

Jamani mbona mnapenda kupindisha hoja unnecessary? Mtu mwenye chuki na mwingine atamsifia? Hivi wewe ukiwa safarini, unaesafiri nae sio mwenzio? Katika mazingira yale Ndugai alikuwa Mwenzie Lissu kwani walikuwa na sifa moja, wazungumzaji wakuu wa mdahalo ule. Tuache siasa za jazba na kuingiza chuki binafsi na personal attacks. Palipo na hoja, hoja itumike kujibu.

Inshort nliipenda saaana lkn NDUGAI alikuwa kejeli nyingi jambo ambalo halikuwa zuri na shutuma za moja kwa moja.Mf alisema CHADEMA ndio wanaofanya vurugu ukumbin jambo ambalo ata mwenyekit wa Mdahalo alipinga,kingine ni kusema wanavaa magwanda kama Mgambo ayo si mambo mazuri na hasa wanapojadili mambo yenye manufaa kwa taifa

Wadau kwa wale tulioshuhudia mdahalo huu ni kuwa kwa kiwango kikubwa haukukidhi kile watz wengi wangetegemea kupata.Hii imetokan na muongozaji kuwa dhaifu kidogo pale wasemaji walipokuwa wanakwenda nje ya mada.mfano hakumkatisha Ndugai pale alipoanza mashambulizi binafsi badala yake akamwacha kuendelea kuropoka.vilevile Ndugai hakujibu maswali mengi aliyoulizwa na hilo mungozaji hakujali!La mwisho nimepata wasiwasi mkubwa kuwa kama hulka ya chuki iliyooneshwa na Ndugai kiasi kusema CDM wanavaa magwanda kama mgambo kuitisha serikali au wanataka serikali na bunge vishindwe kutawala-ni vipi atatoa haki kwa CDM?Kifupi mdahalo umefichua kile kilicho ndani ya mioyo ya viongozi wa bunge.Me nafikiri spika na naibu wake+wenyeviti waendelee na uongozi wa bunge kwa upendeleo kama walivyopanga ila wajue hilo ndio kaburi la CCM wanafurnish kwa kuwa Public inaona na kujudge yanayotokea.Hata wanaposema wananchi wataamua ni kweli kwa jinsi wanavyozima hoja zenye maslahi ya wananchi kibabe-tutaamua.VIVA CDM+NCCR no retreat-ALUTA CONTINUA.

LISSU aponda wabunge wa ccm kwa kuishukuru serikali wakati wa kuchangia hoja,wanatumia muda mwaingi kuwashukuru wake zake zao,watoto,rais na waziri mkuu.pia kuunga hoja asilimia mia then wanasahau kuchangia hoja.

hawa wakwe zangu ccm nini, kwa nini wamenipangia siku ya kutoa mahari tar 30 July, yaani sijafatilia mdahalo kabisa bt thank to JF.

Hii nimeipenda sana, JN lazima alikaa, kama ngumi kapigwa ya chembe, lazima ukae teh teh teh!

haaaa kumbe wabunge wanaangalia maslahi ya chama chao kwanza, jimbo, taifa afu wao wenyewe hayo ndo majibu ya Ndugai
my take: kumbe sisi wapiga kura ni second priority kwani nani amewachagua ni chama au?
hivi ccm hawakumshauri ya JN, mwenyekiti wake mwenyewe alimkimbia slaa ye nani ajifanye anaweza 1 to 1 CDM, afu mtu mwenyewe TL, huyu jamaa amejitakia kwa kweli mi hata simhurumii

Ndugai ameshachanganykiwa mara hii anajibu asivyoulizwa

si unajua mtu akipata feki afu ile kuingia chumba cha mtihani anakauta maswali si yale aliyotegemea mtu alishameza majibu, hapo lazima swali na jibu vitofautiane

A note to take kwa watz wenzangu.Tumeweza kuingiza wabunge wa upinzani takribani 60 bungeni.matokeo yake tumeona CCM kuchanganyikiwa na kupoteza dira moja kwa moja,wamejikuta wanarukia hoja za wapinzani na kuimplement bila maandalizi na kujikuta na aibu zaidi(mf katiba mpya issue)wanafukuzana chamani wakihisi hiyo itawaponya lakini wapi!!Hima popote ulipo unga mkono juhudi za wabunge wapinzani kuikomboa nchi hii,penye uchaguzi mdogo hakikisha hawarudi bungeni hwa mgamba tena.Najua idadi kuwa kubwa ni jambo jema ila quality ya wabunge tunaopeleka bungeni ndio la msingi sana.Muogope sana mbunge wako toka magamba anaetoa sifa na shukrani muda wote na kuunga mkono hoja 100/100 kisha mwishoni anaanza kusemea matatizo yenu kama ziada.hwatufai hawa!!

kwann bado watu wanaipenda ccm kama viongozi wenyewe km wale?eti naibu spika anaongea vile?miaka 10 nyuma bungeni anafanza nn!

Niliutazama mjadala huo ukumbini, tulikuwa watu wengi. Sura mojawapo baada mdahalo huo iko wazi... ccm inapoteza umaarufu na kuaminika kwake kwa kasi kubwa!

Kwa hakika mdahalo ulikuwa mzuri japokuwa kulikuwa na kasoro za hapa na pale (eg. Sauti kutokusika vema, Kukatika kwa matangazo ya television, Muda kuwa mfupi nk) Kifupi ulikuwa mpambano kati ya Serikali(Job Ndugai) dhidi ya Mwanaharakati(Tundu Lisu) Na hii ni analysis yangu kwa ujumla: *Tundu Lisu aliweza vema kuuthibiti mjadala kwa kukidhi maeneo yote muhimu ya mjadala(Critical debate Parameters) 1/TECHNICS(Ufundi) eg. Mood(Hisia),Motion(Mjadala), Regulation(Kanuni/Taratibu)) 2/TACTICS(Mbinu) eg. Open minded, not offensive, not defensive (Fikra zilizo funguka, sio kushambulia/Kulaumu,Wala sio kujitetea) 3/COMPETENCE(Umahili) eg.Understanding(Kuelewa), Explaination(Ufafanuzi), Convincing(Ushawishi). Hivyo vyote ni vitu muhimu sana katika mijadala yote duniani (eg USA presidential election debates,Havard university-Law chamber debates, UK Prime minister television debates etc). Ni vigezo ambavyo hutazamwa sana na analysts(Washambuzi). Kifupi ndivyo vigezo viliwapa umaarufu mkubwa sana watu kama John Kenedy, JK Nyerere, Nelson mandela, Barack Obama, Tony Blair, David Cameroon etc wakati wanafanya harakati zao kuwa viongozi. *MAKOSA MAKUBWA ALIYOFANYA JOB NDUGAI(TECHNICAL&TACTICAL BLUNDERS) 1/Propaganda(Siasa za upotoshaji wa makusudi) eg.Uvaaji wa Combat,Mzozo wa Shibuda ,Mzozo wa madiwani wa Arusha,Maandamano ya kupinga ukandamizaji,Kutoshirikishwa kwa vyama vingine katika kambi rasmi ya upinzani,Harakati za chadema bungeni .nk. 2/Kutoka nje ya mjadala kwa kuamua kushindana na washiriki badala ya kushindanisha hoja (eg.Inasemekana siku moja kabla, alishatanga ndani ya Bunge kuwa anakwenda kwenye mdahalo akiwa tayari ni mshindi!) That is wrong attitude before the battle(So that he missed the target of the motion).Lengo la mjadala halikuwa kumshindanisha yeye na Lisu,bali kufafanua&kujibu hoja zinazohusu mwenendo mpya wa Bunge letu. 3/Kujaribu kuisemea serikali na watendaji wake(eg. Uwezo wa Pinda bungeni, Utendaji wa serikali etc). Kifupi hakujua yuko pale kama nani (ie.Mwakilishi wa kiti cha spika,Msemaji wa serikali,Mwakilishi wa CCM,au nani?) 4/Kuwashambulia baadhi ya washiriki waalikwa (eg.Alidai Kuwa ni wanachama wa chadema) That is the biggest mistake he did. Remember Good debater always chalenges the motion but never challenge individual opponent (Nafikiri mwongozaji alijaribu kutumia hekima kubwa kwa kumkumbusha kwamba ule ni mjadala mkubwa sana na waliopo pale ni zaidi ya mwanachama wa vyama vya siasa) 5/Kushindwa kuelewa hisia(Mood) za muungozaji(Rose),Mzungumzaji mwenzie(Tundu Lisu) na pia baadhi ya washiriki waalikwa(Kumbuka alikuwa akirudiarudia kusema kuwa watu wote waliokuwa wakimpinga pale ni watu wa Chadema) *KETE ZA USHINDI ALIZOTUMIA TUNDU LISU(CREDIBILITY POINTS) 1/Ufasaha katika kujibu&kutoa maoni katika maswali aliyoulizwa. He was Straight,Effective,Short&Clear hit to the point (eg.Kazi za mnadhimu wa upinzani, Changamoto za bunge hili, Sababu ya kutolewa nje bungeni, Lugha ya kuudhi bungeni etc) 2/Alijikita zaidi kwenye hoja iliyowekwa kujadiliwa(He concentrated to debate the motion,and nothing else) 3/Alijitahidi sana kufuata kanuni za mjadala(He tried to rely on debate regulations).Mfano:kulinda Muda,Kuheshimu mwongozaji,Kutuliza munkari wa wachangiaji, Kuvumilia shutuma alizotupiwa, Kukwepa kumshambulia mtu binafsi nk) *MWISHO(MAONI YANGU) 1/Tundu Lisu yuko vizuri sana katika katika kujenga hoja yake au kubomoa hoja ya mpinzani wake. Kifupi ni aina ya mwanasiasa ambaye watanzania wanaweza kumtumia,kujifunza na hata kujivunia.He is impressing young generation to join in political movement in a proper way. Jamaa huko Calm,Confident&Competent katika harakati zake za kisiasa. I wish him all the best in his political movement. 2/Mdahalo ni jambo muhimu sana katika kukua kwa uelewa wa jamii. Hivyo basi iandaliwe vizuri na mara kwa mara. Wakati mwingine CCM iandae watu wenye uwezo katika kukabiliana na hoja muhimu kama hizi na siyo kukurupuka tu. Kwani wanatia aibu. Kumbuka hii siyo mara ya kwanza kwa wawakilishi wa CCM kutia aibu katika mijadala muhimu. Mfano: @Tambwe hiza (Mswaada wa katiba mpya-Karimjee) @Prince Bagenda(Mjadala wa katiba mpya-UDSM) @Hawa Ngubi(Mchakato majimboni-Ubungo). Hawa wote walishindwa kukidhi mahitaji ya hoja muhimu. Tafadharini sana CCM anzeni kujifunza sasa mfikie viwango vya wapinzani wenu. Bado humjachelewa. Kukimbia midahalo hakukusaidia na kuikimbilia pia hukutawasaidia.Kaeni chini mjifunze kutengeneza hoja na siyo kudandia au kubeza hoja za wapinzani wenu. NAWASILISHA.
Huu ni uandishi gani sasa? tutasomaje namna hii?

Ndugai hakuudhuria kama Naibu Spika pale ila kama Mwanachama na Mbunge wa CCM kama alivyoudhuria Lissu kama Mwanachama na Mbunge wa CDM.Kama ni kuzingatia nafasi zao basi Lissu angepaswa kuitwa na Lukuvi na si Ndugai.

Vile vile tukubaliane kuwa interest to a party may hinder a person to judge fairly to other party.Look comments to Lissu + Ndugai.
Kwa nini wewe kila siku huna akili? simaanishi uwe pro CHADEMA, lakini nashangaa kwa nini huna akili?

Kwanza nizungumzie mdahalo wenyewe:

Kuna haja ya kujifunza kutoka kwa wenzetu pia. Midahalo mingi huwa ni ya muda wa masaa matatu na kuendelea.

Washiriki, wale wanaokuwa mbele hutengewa muda mrefu wa takriban robo saa kueleza hoja zao na baada ya li saa

ndio hadhira nayo upewa fursa ya kuuliza maswali.

Tuna mwanya wa kujifunza na pia kwa midahalo inayorushwa laivu ni muhimu kwa hizi stesheni za televisheni kuwa

na director on the floor na a minimum of 5 cameras so that there is sufficient coverage and coordination ya event

na matukio muhimu.

Pili nizungumzie mdahalo wenyewe :

Kwa mazingira ya huu mdahalo ilikuwa si rahisi kujibu kila swali vema huku ukijenga hoja sawia. Muda ulibana mno.

Kuna swala la staha na haiba limeonekana wazi wazi. Naibu spika anachakujifunza apa. Ni muhimu kuelewa nafasi

yako katika jamii. Kiongozi anatakiwa kuwa na kauli za heshima na uvumilivu na kamwe asiwe anabeza na kutumia

lugha rejareja.

Imeedhihirika kuwa watanzania wanaanza kuelewa mwanasiasa wa sasa anatakiwa awe na vigezo gani. Tazama midahalo ya karne

hii na utajifunza kuwa, siasa ya sasa imejkita katika kujenga hoja na uzalendo juu ya nchi. Hii imejionesha sana katika midahalo ya katiba.

Vyama vinanvyopwaya ni vile ambavyo vinafanya siasa za enzi ya ukombozi yaani political propaganda. Imeedhihirika mara nyingi chama

tawala CCM kimekua kinaendesha siasa za namna hii na hata wanachama wake wengi bado hawajaelewa nafasi ya mwanasiasa katika zama

hizi. Kwa sababu hii bado wamejkita katika siasa za malumbano na kuamini mwanasiasa mzuri ni yule aliye mahiri kwa kuzungumza na kushutumu

sana. Tazama Nape Nnauye, Tambwe Hizza, Yussuf Makamba, Jakaya Kikwete, John Malecela, Wassira, Membe n.k

Ni wazi kuwa Naibu spika alipwaya sana mbele ya mnadhimu wa kambi ya upinzani. Tuondoe ushabiki, CDM nao wanayo ya kujifunza lakini

wanastahili sifa kwa kuwa wepesi wa kujisahihisha wanapoteleza, Bw. Lissu alitamka kuwa bunge la 9 halikufanya kazi na kuwa hili la 10 ni bora zaidi

lakini alipoulizwa na Engr. Manyanya kuhusu hilo alikiri tena moja kwa moja kuwa bunge hilo lilifanya kazi na akaendelea na majibu mengine

tofauti na Bw. Ndugai ambae katika hilo hilo swala yeye alikwenda kushambulia tu akisema kuwa Dk. Slaa alikuwa sehemu ya bunge la 9,

kwahiyo hakufanya kazi kulingana na kauli ya Bw. Lissu, vivyo hivyo kwa Bw. Mbowe kwenye bunge la 8. Haya ni mapungufu ambayo

upande wa CCM umekua ukiyaonesha mara kwa mara.

Kuhusu swala la Mb. H. Mdee, nafikiri mwanasiasa yeyote mahiri angelikwepa hilo. Si sahihi kuwatuhumu au kuzungumzia mapungufu ya

mwenzio mbele ya umma. Kwa wale walio na ndoa wanajua, mke na mume hawalumbani hadharani na kadharika hawajadili mapungufu yao

kwa watu wengine bali huwekana sawa wao wakiwa wawili.

Kwa kuhitimisha:

Tunahitaji midahalo mingi ya namna hii ili kuchochea fikra na kuelimishana na kujfunza.

Watanzania wote tutumie fursa hii kujifunza na kujiimarisha, vivyo hivyo kwa CDM na CCM.

Jamani mbona mnapenda kupindisha hoja unnecessary? Mtu mwenye chuki na mwingine atamsifia? Hivi wewe ukiwa safarini, unaesafiri nae sio mwenzio? Katika mazingira yale Ndugai alikuwa Mwenzie Lissu kwani walikuwa na sifa moja, wazungumzaji wakuu wa mdahalo ule. Tuache siasa za jazba na kuingiza chuki binafsi na personal attacks. Palipo na hoja, hoja itumike kujibu.

duh weee ndio umealimu kabisa twende jukwaa la lugha
mimi naona posho huko sahihi hakukua na sababu za BEN kutumia neno MWENZIE
lina maana nyingi na BEN anajua hiyo kwa mimi naweza sema
alikuwa na maana LISU ni gamba na nikabaki kuwa sahihi kama msomi na mwana diplomasia anajua hilo
kutoa kauri tata kafanya makusudi

Ndugai alikubali kwenda kwenye mdahalo kwasababu yupo psychological affected na makofi anayopigiwa na wabunge wa ccm Bungeni kwa kila anachokisema, so alidhani popote atakapokwenda na chochote atakachokisema kitapigiwa makofi kama ianavyotokea Bungeni, Matokeo yake akajikuta kati kati ya watu makini ambao hawababaishi na ushabiki bali nguvu ya hoja.

Ndugai alikubali kwenda kwenye mdahalo kwasababu yupo psychological affected na makofi anayopigiwa na wabunge wa ccm Bungeni kwa kila anachokisema, so alidhani popote atakapokwenda na chochote atakachokisema kitapigiwa makofi kama ianavyotokea Bungeni, Matokeo yake akajikuta kati kati ya watu makini ambao hawababaishi na ushabiki bali nguvu ya hoja.

cdm wamechemka ktk mdahalo wa leo uliofanyika ktk ukumbi wa saint gasper Dodoma na hii ni mara ya pili mdahalo wa kwanza ulikuwa kati ya mbowe na Hamad Rashid ambapo mh mbowe alibwagwa vibaya, Leo tena mh Lissu hakuwa anajibu kile anachoulizwa, ndugai amejibu vema leo amemfedhehesha Lwaitama na maswali yake fitna ambapo mh ndugai alijibu vema.

Nilikuwa nasoma kwanza ili nichangie ila siwezi kukuacha bila kukujibu. Kama umeona Ndugai kajieleza vyema basi tatizo sio yeye ila ni wewe, unahitaji tiba ndugu yangu

Back
Top Bottom