Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mimi pamoja na kufuatilia kwa karibu na kuahirisha shughuli zote ili niweze kufuatilia mdahalo wa jana uliokuwa na wasemaji wakuu toka Chadema na CUF, nilibaki na maswali ambayo majibu sikupata. Mwaka 2005, vyama vyote viliunga mkono CUF kuunda kamba ya upinzani bungeni kwa vile walitimiza masharti ya kanuni.

Mwaka 2010, CHADEMA wametimiza matakwa hayo CHADEMA, CUF inakuja na hoja ya "manolity" ili waunde kambi ndogo ya upinzani bungeni ingawa hawakutimiza masharti ya kanuni hiyo.

Kama Suala la Manolity ni muhimu kwa CUF, basi lingeweza kutumika Zanzibar kuwaingiza vyama vingine katika serikali ya umoja wa kitaifa maana umoja wa kitaifa siyo CCM na CUF bali vyama vyote vya siasa!!

Na kama CHADEMA wametimiza kanuni ya Bunge kuunda kambi ya upinzani bungeni, maana yake wataisimamia serikali na watakuwa na mtizamo tofauti na Serikali ya CCM katika kuishauri. Je CUF na kambi yake ambayo haipo kisheria au kikanuni itakuwa imeungana na CCM au CHADEMA? Au itakuwepo bila kuunga mkono sehemu yoyote?!

Maswali bado ni mengi, tunahitaji majibu bado. Kwa hiyo waandaji waandae tena waheshimiwa waje hapo kuendelea kutuletea majibu zaidi. Inawezekana wapo ambao wamechanganyikiwa zaidi yangu...

Nawasilisha
 
Ahsante sana kwa michango yenu. Tatizo la screening maswali si vema. Maana again tutarudi pale pale kuwa wandaaji wanaweza kuchakachua maswali. Mimi tatizo langu ni hadhira inayohudhuria nafikiri hapo ni lazima pafanyiwe kazi. Maana katika msafara wa Mamba na Kenge wamo. Sasa wale wenye Jazba ni vema kukawa hata na Mabounser wazuri tu iukibidi kuwanyannua juu juu labda wengine watajifunza kujiheshimu.
 
Jenifa,
Nadhani ni vizuri kuelewa msingi wa hoja ya chadema ya kujadiliwa kwa Katiba. Hata swala la mishahara mikubwa ya Wabunge ni swala la Mfumo. Ndio msingi wa Mbowe kujibu kuwa "Chadema ingelishinda ingelibadilisha Mafao hayo". sidhani kama Mbowe alikataa kujibu swali. Nilikuwapo na nilimsikiliza live na siyo kwenye TV. Hivyo deliberate efforts za kupotosha si vema zikaachiwa. Hata hivyo kwa wale wasiofahamu ni vizuri nikaeleza mfumo wa kupanga Mishahara na Posho za Wabunge:
i) Kwa sasa Mishahara ya Wabunge inapangwa na Tume ya Huduma za Bunge ( yaani Parliamentary Service Commmission) ambao wajumbe wake wengi wanatoka CCM. Wapinzani katika Commission ni wachache sana na hata ikipigwa kura watashindwa daima kama ilivyo ndani ya ukumbi. Ni tatizo la kimfumo na ni tatizo la ukiritimba wa Chama kimmoja. Ndio hoja ambayo siku zote tumeiweka kwa Watanzania, ndio maana tumekuwa tukisema " Watanzania wenyewe ndio wanaosababisha kwa sehemu kubwa umaskini wao kwa kuchagua wabunge wa Chama kimmoja". Ukiachilia mbali uchakachuaji uliofanyika, nafurahi kuwa Watanzania wamelitambua hilo na ndio maana idadi ya Wabunge wa Upinzani imeongezeka sana. Pasingelikuwa na Uchakachuaji, nina hakika ukombozi ungelikuwa umefika au ungelikuwa mlangoni. Hivyo isingelikuwa Busara kwa Mbowe kujibu hoja ambayo hana mamlaka nayo na wale hawezi kwa njia yeyote ile " kuibadili:" au hata ku " influence". Msingi huu ukifahamika vizuri, hoja yako ya kwanza inakuwa haina mshiko wowote.
ii) Tume ya Huduma ya Bunge inatokana na Katiba Mbovu na Sheria zake. Hivyo ukifanikiwa Kubadili au kupata Katiba mpya, ndio ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo. Kumbuka, kuwa Tume ya Bunge "inapendekeza" kwa Rais, na ukiwa na Rais makini, atakataa kupitisha mapendekezo ambayo yanaifilisi Taifa. Rais wetu kwa mujibu wa Katiba aikiisha kuipitisha hakuna mahali pengine unaweza kuhoji, au kama utataka kumhoji kuna utaratibu mgumu sana wa kuihoji Serikali mahakamani, kwanza "lazima utoe Notice nadhani ya siku 90, kisha upate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mara nyingi kibali hicho hakitolewi". Tumekwisha kujaribu njia hizo katika kipindi changu cha miaka 15 Bungeni lakini ilishindikana. Hivyo jibu pekee ni Marekebisho makubwa ya Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais (Excessive powers).
iii) Katika hoja yako ya pili kuhusu kuunganisha nguvu za Upinzani, unazungumzia Chadema kuchukua 100M kwa kuunda Serikali Kivuli. Ni kweli Utaratibu wa sasa, tena ambao hauko ndani ya Sheria, wala Kanuni unatenga kila Mwaka Bajeti ya Tshs 100 Millioni kwa "Kiongozi wa Upinzani". Hivyo Ungelifanya utafiti, hoja yako isingelikuwa flawed kama sasa a) Chadema haina haki wala haiwezi kuvuta 100 million kutokana na kuundwa kwa Kambi ya Upinzani kwa vile fedha hizo zimetengwa, kwa kilichoelezwa jana na Mhe. Hamad kama ulimsikiliza vizuri kuwa ni kwa "Kiongozi wa Upinzani" wala siyo kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani. Conclusion yako ni matokeo ya kutokusikiliza vizuri na kutokufanya utafiti. Hamad amekuwa Kiongozi wa Upinzani toka 2005 hadi 2010, alitakiwa kuulizwa hizo fedha alizutumia kwa kazi gani, na Katibu wa Bunge anatakiwa kutoa hadharani matumizi ya fedha hizo ili Watanzania waone zilitumika kwa kazi gani na kwa manufaa ya nani. Kama hazikutumika kwa manufaa ya watanzania wana haki ya kupiga kelele kwani millioni 100 ni fedha nyingi na zingeweza kujenga madarasa kadhaa kupunguza upungufu wa madarasa au zahanati. b) Mimi nilikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani, katika miaka yangu yote niliyokuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani sijawahi kuona Break down ya fedha hizo na matumizi yake. Tulipodai zitumike kwa gharama za ofisi mathalan, kumlipa "mratibu wa Kambi"ambaye kwa taarifa yako "ameajiriwa" na Kambi na mishahara(posho zake zinalipwa kwa kuchangiwa na wabunge wenyewe ambao tulikuwa tunakatwa kutoka kwenye mishahara na posho zetu wakati kuna fedha za Kiongozi wa Upinzani), tuliambiwa kuwa hizo ni za Kiongozi wa Upinzani na labda fungu lingine litafutwe kwa ajili ya Kazi za Kambi. Ungelifanyia utafiti swala hilo usingelitoka na hoja kuwa Chadema wanachukua hizo fedha, kwani Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema hadi jana, haijapokea fedha zozote kutoka Ofisi ya Bunge ( labda Gari rasmi la Kiongozi wa Upinzani, ambalo sina hakika hata kama linahudumiwa na kasma hiyo). Hoja yake inaweza pia kugeuzwa kuwa Hamad hataki kuungana na Chadema kuunda Kambi rasmi kwa vile kama alivyokuwa Dr. Slaa, Naibu Kiongozi wa Kambi ambaye hakuwa anajua hizo fedha zilifanya nini, naye sasa atakuwa Naibu hivyo hatakuwa na fedha. Labda kwa kuunda Kambi "ndogo isiyo Rasmi" naye pia kwa mlango huo huo anaweza kupewa mafao kama ya Kongozi wa Upinzani yaani gari, Ofisi, Nyumba na Fedha 100 Millioni. Lakini tukumbuke tukiendekeza kugawa fedha, Kodi za Watanzania maskini kwa mtindo huu, hatutafika na Taifa litaendelea kuporomoka na kuzama katika lindi la Umaskini.
iv) Mtafiti wa kweli angeliuliza, na Jenifer angeliuliza swali kwenye Mdahalo au hata kwenye JF kuwa " Je Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema itaendelea kutumia hizo 100 Million kwa matumizi Binafsi ya Kiongozi wa Upinzani au kwa matumizi ya shughuli za Kambi mathalan utafiti na kazi za mawaziri Kivuli, nina hakika angelipata jibu sahihi kuliko kufanya conclusion kwenye "hisia" ambazo nazo kama tulivyoona jana kwenye mdahalo zinaweza kuwa na sababu zake.
Jenifer, naamini nimeweza kutoa mchango wangu kwa manufaa ya wana JF wote ambao hawajui hizi fedha kama zilikuwepo, ziko, na kama ziko zinalenga kufanya kazi gani chini ya uongozi mpya wa Kambi ya Upinzani inayoongozwa na Chadema.

Mawazo ya mtu ambaye elimu aliyopata imemkomboa kifikra.
 
We ulitakaje wakupe na wewe?acha ujinga wewe hiyo sio hoja ya kuleta hapa watu wenye akili zetu tuijadili. Waache chadema waongoze kambi ya upinzani kanuni zimewapa uwezo huo na wao ndio wenye mamlaka ya kuamua nani wamuingize nani wasimuungize, na kwa sasa chama cha upinzani ni chadema tu. Cuf tayari wanandoa na ccm, nccr nao walewale ,tlp ,udp hakuna kitu wote walewale. Chadema endeleeni na mpangoo wenu mkiwangiza hawa wanafiki watakiua chama na ndio lengo lao.
People powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa

Jenifa nadhani umekurupuka na kujaribu kujenga hoja ambayo haina mantiki yoyote ile! Jaribu kufanya utafiti mdogo wa haya niliyoainisha hapa chini:-

  1. MFUMO:- Tafiti ni mfumo gani unaoendesha siasa na serikali hapa nchini. Je mfumo huu unatoa fursa ya UKWELI NA UWAZI kwa kambi ya upinzani kuipinga serikali na serikali kukubali hoja hizo? Maana unataka Mbowe na CDM wawe tayari kupunguza mishahara na posho za wabunge huku at the same time hawana idadi kubwa ya wabunge watakaokubali "kupigia kura hoja hiyo"!! Unadhani ni wabunge wangapi wa CCM watakaokubali hoja ya kushusha posho zao say kwa 50%?? Kwa kifupi hoja hiyo ikiletwa bungeni SERIKALI YA CCM na WABUNGE WAKE hawataisupport....jiulize tu, UMEWAHI KUSIKIA MBUNGE WA CCM au RAIS, au WAZIRI MKUU kuwaomba wabunmge kufikiria uwezekano wa kupunguza bajeti hiyo?? JIBU ni hapana.....tatizo serikali hii ambayo imeingia madarakani, na iliyokuwepo kwa miaka HAINA DHAMIRA HIYO (Commitment) Sasa kwa nini leo unamhukumu MBOWE kwa kitu ambacho hana mamlaka nacho? Ungetaka kumpima vizuri basi MNGEICHAGUA CHADEMA ili muone!!
  2. Sambamba na hilo fanya utafiti mdogo tu: NI CHAMA GANI AMBACHO MGOMBEA WAKE WA URAIS ALITHUBUTU KUWEKA WAZI KWAMBA ENDAPO ATAINGIA MADARAKANI BASI MISHAHARA YA WABUNGE , RAIS NA MAWAZIRI INGEFANYIWA MAREJEO (revised) ILI KUIPUNGUZA NA KUMPUNGUZIA MZIGO MLIPA KODI??....Kwa taarif ayako hakuwa kiongozi wa CCM, NCCR, CUF wala TLP, alikuwa ni Kamanda wa kweli, mtu watu na mkereketwa wa nchi hii, Dr (Dr wa kusomea) Wilbroad Slaa; ambaye kama huna taarifa anawakilisha chama ambacho Mheshimiwa Mbowe ndiye kiongozi wake (Mwenyekiti)! Kwa maana hii Mbowe alikuwa na mikakati hii (kichama) hata kabla ya mdahalo wa juzi!
  3. Tangu siasa za vyama vingi zimeingia hapa, sijawahi kusikia Serikali au Kiongozi wa chama cha upinzani AKIZUNGUMZIA BAJETI HII YA 100m!! Mheshimiwa Rashid yeye alikuwa kiongozi wa Uopinzani kwa takribani miaka mitano (2005 - 2010)...huko nyuma sina kumbukumbu!! Kwa miaka yot ehiyo amekaa kimya, sikuwahi kumsikia akiizungumzia hii popote pale, TUWE WAKWELI, lakini leo hii Freeman Mbowe amekuwa kiongozi wa Upinzani (kwa mujibu wa kanuni) tayari watu wanasema anang'ang'ania kwa kuwa kuna Milioni 100 pale!! Hebu tumtendeeni haki huyu jamaa; hata kama hatuipendi CDM lakini maswali ya msingi kama ni wewe ningeuliza: Kumbe kulikuwa na 100m, Mheshimiwa HR amlizitumiaje? Na kwa nini hakuwahi kuzizungumzia popote pale? Unaposema Mbowe hataki kugawana na wenziwe je hao waliopita waligawana na nani?
  4. Acha kuwa mamluki na kuhoji vitu ambavyo havina tija kwa maendeleo ya mtanzania. Hizo Milioni 100 kwa mwaka ni Bajeti ya "Kiongozi wa Kambi ya Upinzani". Kanuni za Bunge zinamtambua Mbowe kama mwenye haki hiyo, sasa kwa nini sasa hamtaki kumpa iliyo haki yake ili (kama hizo hela zipo) azichukue na kuzitumia kuendesha ofisi yake?? Hamad Rashid amepokea Milioni 500 kwa miaka mitano iliyopita, je alizitumiaje? ALIGAWANA NA WENZIWE? Ilikuwa ni dhambi au kwake ni sawa??
  5. Mwisho, mimi si msemaji wa Mbowe, lakini sidhani kama Freeman tunayemfahamu wewe na mimi atakuwa anatokwa mate kwa milioni 100 (kwa mwaka) kama baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani (kama Mrema ambaye aliweza hata kuhudhuria mikutano ya CCM na kukishabikia chama kwa wazi) ...na tunavyomjua alivyofulia....!!
 
Asante kwa uchambuzi Dr. Kwa kweli kuna mengi watanzania wa kawaida hatuyajui,kwa maana hiyo Hamad ameondoka na M500 kwa kipindi cha miaka mitano?Tunahitaji mapinduzi ya hali ya juu,vinginevyo tutaendelea kuomba misaada kwa wazungu hadi Yesu atakaporudi.Chadema msibwetwete hilo fungu lisaidie kuimarisha chama pamoja na pesa za ruzuku,vjijini bado watu wamelala,kunahitaji mapinduzi makubwa ya kifikra,2015 sio mbali.

Jenifa,
Nadhani ni vizuri kuelewa msingi wa hoja ya chadema ya kujadiliwa kwa Katiba. Hata swala la mishahara mikubwa ya Wabunge ni swala la Mfumo. Ndio msingi wa Mbowe kujibu kuwa "Chadema ingelishinda ingelibadilisha Mafao hayo". sidhani kama Mbowe alikataa kujibu swali. Nilikuwapo na nilimsikiliza live na siyo kwenye TV. Hivyo deliberate efforts za kupotosha si vema zikaachiwa. Hata hivyo kwa wale wasiofahamu ni vizuri nikaeleza mfumo wa kupanga Mishahara na Posho za Wabunge:
i) Kwa sasa Mishahara ya Wabunge inapangwa na Tume ya Huduma za Bunge ( yaani Parliamentary Service Commmission) ambao wajumbe wake wengi wanatoka CCM. Wapinzani katika Commission ni wachache sana na hata ikipigwa kura watashindwa daima kama ilivyo ndani ya ukumbi. Ni tatizo la kimfumo na ni tatizo la ukiritimba wa Chama kimmoja. Ndio hoja ambayo siku zote tumeiweka kwa Watanzania, ndio maana tumekuwa tukisema " Watanzania wenyewe ndio wanaosababisha kwa sehemu kubwa umaskini wao kwa kuchagua wabunge wa Chama kimmoja". Ukiachilia mbali uchakachuaji uliofanyika, nafurahi kuwa Watanzania wamelitambua hilo na ndio maana idadi ya Wabunge wa Upinzani imeongezeka sana. Pasingelikuwa na Uchakachuaji, nina hakika ukombozi ungelikuwa umefika au ungelikuwa mlangoni. Hivyo isingelikuwa Busara kwa Mbowe kujibu hoja ambayo hana mamlaka nayo na wale hawezi kwa njia yeyote ile " kuibadili:" au hata ku " influence". Msingi huu ukifahamika vizuri, hoja yako ya kwanza inakuwa haina mshiko wowote.
ii) Tume ya Huduma ya Bunge inatokana na Katiba Mbovu na Sheria zake. Hivyo ukifanikiwa Kubadili au kupata Katiba mpya, ndio ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo. Kumbuka, kuwa Tume ya Bunge "inapendekeza" kwa Rais, na ukiwa na Rais makini, atakataa kupitisha mapendekezo ambayo yanaifilisi Taifa. Rais wetu kwa mujibu wa Katiba aikiisha kuipitisha hakuna mahali pengine unaweza kuhoji, au kama utataka kumhoji kuna utaratibu mgumu sana wa kuihoji Serikali mahakamani, kwanza "lazima utoe Notice nadhani ya siku 90, kisha upate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mara nyingi kibali hicho hakitolewi". Tumekwisha kujaribu njia hizo katika kipindi changu cha miaka 15 Bungeni lakini ilishindikana. Hivyo jibu pekee ni Marekebisho makubwa ya Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais (Excessive powers).
iii) Katika hoja yako ya pili kuhusu kuunganisha nguvu za Upinzani, unazungumzia Chadema kuchukua 100M kwa kuunda Serikali Kivuli. Ni kweli Utaratibu wa sasa, tena ambao hauko ndani ya Sheria, wala Kanuni unatenga kila Mwaka Bajeti ya Tshs 100 Millioni kwa "Kiongozi wa Upinzani". Hivyo Ungelifanya utafiti, hoja yako isingelikuwa flawed kama sasa a) Chadema haina haki wala haiwezi kuvuta 100 million kutokana na kuundwa kwa Kambi ya Upinzani kwa vile fedha hizo zimetengwa, kwa kilichoelezwa jana na Mhe. Hamad kama ulimsikiliza vizuri kuwa ni kwa "Kiongozi wa Upinzani" wala siyo kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani. Conclusion yako ni matokeo ya kutokusikiliza vizuri na kutokufanya utafiti. Hamad amekuwa Kiongozi wa Upinzani toka 2005 hadi 2010, alitakiwa kuulizwa hizo fedha alizutumia kwa kazi gani, na Katibu wa Bunge anatakiwa kutoa hadharani matumizi ya fedha hizo ili Watanzania waone zilitumika kwa kazi gani na kwa manufaa ya nani. Kama hazikutumika kwa manufaa ya watanzania wana haki ya kupiga kelele kwani millioni 100 ni fedha nyingi na zingeweza kujenga madarasa kadhaa kupunguza upungufu wa madarasa au zahanati. b) Mimi nilikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani, katika miaka yangu yote niliyokuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani sijawahi kuona Break down ya fedha hizo na matumizi yake. Tulipodai zitumike kwa gharama za ofisi mathalan, kumlipa "mratibu wa Kambi"ambaye kwa taarifa yako "ameajiriwa" na Kambi na mishahara(posho zake zinalipwa kwa kuchangiwa na wabunge wenyewe ambao tulikuwa tunakatwa kutoka kwenye mishahara na posho zetu wakati kuna fedha za Kiongozi wa Upinzani), tuliambiwa kuwa hizo ni za Kiongozi wa Upinzani na labda fungu lingine litafutwe kwa ajili ya Kazi za Kambi. Ungelifanyia utafiti swala hilo usingelitoka na hoja kuwa Chadema wanachukua hizo fedha, kwani Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema hadi jana, haijapokea fedha zozote kutoka Ofisi ya Bunge ( labda Gari rasmi la Kiongozi wa Upinzani, ambalo sina hakika hata kama linahudumiwa na kasma hiyo). Hoja yake inaweza pia kugeuzwa kuwa Hamad hataki kuungana na Chadema kuunda Kambi rasmi kwa vile kama alivyokuwa Dr. Slaa, Naibu Kiongozi wa Kambi ambaye hakuwa anajua hizo fedha zilifanya nini, naye sasa atakuwa Naibu hivyo hatakuwa na fedha. Labda kwa kuunda Kambi "ndogo isiyo Rasmi" naye pia kwa mlango huo huo anaweza kupewa mafao kama ya Kongozi wa Upinzani yaani gari, Ofisi, Nyumba na Fedha 100 Millioni. Lakini tukumbuke tukiendekeza kugawa fedha, Kodi za Watanzania maskini kwa mtindo huu, hatutafika na Taifa litaendelea kuporomoka na kuzama katika lindi la Umaskini.
iv) Mtafiti wa kweli angeliuliza, na Jenifer angeliuliza swali kwenye Mdahalo au hata kwenye JF kuwa " Je Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema itaendelea kutumia hizo 100 Million kwa matumizi Binafsi ya Kiongozi wa Upinzani au kwa matumizi ya shughuli za Kambi mathalan utafiti na kazi za mawaziri Kivuli, nina hakika angelipata jibu sahihi kuliko kufanya conclusion kwenye "hisia" ambazo nazo kama tulivyoona jana kwenye mdahalo zinaweza kuwa na sababu zake.
Jenifer, naamini nimeweza kutoa mchango wangu kwa manufaa ya wana JF wote ambao hawajui hizi fedha kama zilikuwepo, ziko, na kama ziko zinalenga kufanya kazi gani chini ya uongozi mpya wa Kambi ya Upinzani inayoongozwa na Chadema.
 
nimekupata mkuu... lakini undhaniye ndiye siye.... ku control civilized audience itakuwa kazi..... unadhani jana watu waliingia ilimradi tu waingie.... walicuja watu lakini matokeo ndio hayo.... uneona midahalo effective kama HARDTALK ya Tim Sebastian BBC ni watu watatu tu mjengoni... na maswali anayouliza yanatokana na poll questions za mada ya mdahalo....inawezekana kupata mdahalo mzuri .... kwa yote haya
 
Hapo bado hujagundua kuwa CUF ni chama cha uislamu? bado hujagundua CUF ni CCM-B? Hujagundua kuwa CUF ni chama cha zenj?

Heri wajiunge na ccm kuliko chadema!

CHADEMA itaendelea kukua bila hata kushirikiana na chama chochote!
 
Katiba mpya tunatarajia kuipata kwa njia gani?
 
Hapo bado hujagundua kuwa CUF ni chama cha uislamu? bado hujagundua CUF ni CCM-B? Hujagundua kuwa CUF ni chama cha zenj?

Heri wajiunge na ccm kuliko chadema!

CHADEMA itaendelea kukua bila hata kushirikiana na chama chochote!

Ulikuwa ni mdahalo kati ya mwanasiasa(Mbowe) na mswahili wa pwani(HR).

Nilikuwa nasikia mipasho na vijembe tu kutoka kwa HR. moja wapo ni kujitapa kuwa yeye ni 'mwanasiasa mkongwe'.

njaa na wivu vinawasumbua CUF.

Kuungana na chadema ni mwiko.

cuf ni wanafiki. utaungana vipi na mnafiki?
 
hamada sory hamad rashid ni mzee wa marupurupu,hana dhamira ya kweli ya upinzani,
amepoteza nafasi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,bado anaitamani kwa gharama yoyote ile hata ikiwa kuwadharirisha wapinzani wenzake,
bora anyamaze kimya kwani anavyozidi kutafuta nafasi ya kuongea anajipunguzia heshima yake mbele ya jamii,
amesahau kuwa watanzania wa huku bara si mabwege,hajui kuwa wapiga kura wa zanzibar yote ni sawa na jimbo la ubungo tu,
amevamia treni kwa mbele,asubrie kifo chake,kwani ameshagundulika,kuwa ni pandikizi
 
Nimekuwa nikijiuliza, mbona watu wanagombea kuwa kiongozii wa upinzani.Duuuuuuuuuuuuu. Kumbe kiongozi wa upinzani anapeta fedha nyingi namna hiyoooo.Kumbuka ni kiongozi na sio chama cha kambi ya upinzani ni fedha za kiongozi wa upinzani.mhhhhhhh.

Sahizi ndo naona wazi vita ya waliomsusia rais na waliopinga kususa.Mhhhhhhhh
 
Dr.
Well said! Sielewi inakuaje mtu hasikilizi vizuri hoja alafu anaropoka tu. Nadhani hao ni jamii ya yule mwandishi wa gazeti la Mtanzania leo kuandika mambo ya mdahalo ambayo ni upotoshwaji wa makusudi na wa wazi. Hilo ndo gazeti la kufunga na si Mwanachi!
 
kwa kweli mm nnahangaika kutafuta nn walichozungumza ili nipembue mwenyewe mchele na pumba lkn sijaona pahala walipoweka hayo mazungumzo au walau clips zake

kulikoni kikawaida matokeo kama haya tunaweka video clips zake na hapo tunakuwa huru sasa kuchangia na kutoa kile tunachoona ila kwa muundo huu uliopo kila mmoja anavutia kwake na la kushangaza wako wengine hupelekwa tu kama migombe

nnaomba tuwekee clips kwa alonazo tuone nn wameongea hasa
 
Mimi pamoja na kufuatilia kwa karibu na kuahirisha shughuli zote ili niweze kufuatilia mdahalo wa jana uliokuwa na wasemaji wakuu toka Chadema na CUF, nilibaki na maswali ambayo majibu sikupata. Mwaka 2005, vyama vyote viliunga mkono CUF kuunda kamba ya upinzani bungeni kwa vile walitimiza masharti ya kanuni.

Mwaka 2010, CHADEMA wametimiza matakwa hayo CHADEMA, CUF inakuja na hoja ya "manolity" ili waunde kambi ndogo ya upinzani bungeni ingawa hawakutimiza masharti ya kanuni hiyo.

Kama Suala la Manolity ni muhimu kwa CUF, basi lingeweza kutumika Zanzibar kuwaingiza vyama vingine katika serikali ya umoja wa kitaifa maana umoja wa kitaifa siyo CCM na CUF bali vyama vyote vya siasa!!

Na kama CHADEMA wametimiza kanuni ya Bunge kuunda kambi ya upinzani bungeni, maana yake wataisimamia serikali na watakuwa na mtizamo tofauti na Serikali ya CCM katika kuishauri. Je CUF na kambi yake ambayo haipo kisheria au kikanuni itakuwa imeungana na CCM au CHADEMA? Au itakuwepo bila kuunga mkono sehemu yoyote?!

Maswali bado ni mengi, tunahitaji majibu bado. Kwa hiyo waandaji waandae tena waheshimiwa waje hapo kuendelea kutuletea majibu zaidi. Inawezekana wapo ambao wamechanganyikiwa zaidi yangu...

Nawasilisha

Ule ulikuwa ni mdahalo mbovu katika midahalo yote niliyowahi kuiona, kuisikia au kuhudhuria.

Kwanza Mwenyekiti alikuwa hajui akifanyacho. Alikuwa ana act kama vile ni mwenyekiti wa kikundi cha kuigiza.

Huyo Mbowe ndio kabisaa, hata sijui alikuwa anaongea nini, mara Rais tunamtambuwa, Mara serikali tunaitambuwa mara Matokeo jinsi yalivyotolewa hatuyaytambuwi, yaani ni kama komedi origino, na ataipata wiki hii kwa hao kina komedi, akajitazame.

Na huyo Hamad alikuwa haeleweki, yaani ni upupu mtupu.

Bogus.

Kwa hiyo ndugu yangu' kama ulikuwa unategemea majibu, nakupa pole sana. Wala hutopata majibu kutoka Chadema wala CUF.

Nadhani Chadema wangempeleka Zitto angeongea la maana kuliko huyo Professional DJ.
Bora kidogo HR aliongea vizuri.
 
Dar Es salaam motoooooooooooooooo...... au baridiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba

Hapa nguruwe ni CCM au Vyama vya Upinzani? Shamba lilisimama badala ya Nchi au ulaji? Mkulima ni nani, ni CUF au nani? Mazao je, ni wananchi au madaraka?
Naombeni ufafanuzi ili tuchangie vizuri siyo kutafsiri kitu ambacho hakieleweki vizuri kwa watu!
 
kwanini wasisubiri kukamata dola ili kubadilisha katiba ila wako tayari kusubiri kukamata dola ili kupunguza mishahara?

100M anataka kutumia na chadema tu ndio maana hataki kuungana na akina mrema. uchoyo umewatawala chadema

Jenifa
Kwa kufanya hivyo wanaua ndege wawili kwa jiwe moja.
pia katiba ikiwa ni ya wananchi mambo yote yanakuwa rahisi
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba".

Sasa je,
1 Mh Hamadi anafananisha washiriki (watu au vyama) wengine kwenye uchaguzi kama HARAMU?

2.Mh Hamad anatuambia kwamba siasa(shamba) imeingiliwa na watu HARAMU?

Hebu nisaidieni wana Jf
kiswahili cha pwani hicho... kwamaana ni sawa na kususia mechi ya mchezo kama mpira vile...ukisusa unapoteza point 3 na goi 3... kwahiyo wao CUF hawawezi kufanya hivyo...
 
Back
Top Bottom