Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa

1. Naona hapa unataka kuchakachua hoja. Alisema kama Chadema wali'lobby' ili mfumo unaotoa fursa ya mishahara minino kwa wabunge ubadilishwe lakini hawajafanikiwa. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yao na siyo kususia mishahara.

Ni kama mtu anayelalamika kuwa analipwa mshahara kidogo, sidhani kama hoja ni kukataa huo mshahara mdogo bali kuwepo mfumo bora wa kufanya mishahara ilipwe kwa haki. Hali kadhalika kama mtu ana hoja kuwa mishahara ni mikubwa sana, hoja siyo kukataa mshahara huo mkubwa bali kuwepo mfumo unaozingatia hali halisi ya nchi na kuweka mishahara inayoendana na maisha ya Watanzania.

Sidhani kama mtu anayefanya kazi na mshahara wake ni mkubwa sana kuna njia ya kuupunguza yeye mwenyewe bila kuweka mfumo au sheria ya kufanya hivyo.

2. Rashidi alisema alipokuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni alikuwa anapata Sh100,000,000 kwa ajili ya kambi ya upinzani (ndivyo kanuni zilivyo hadi sasa). Lakini alisema walishapeleka mapendekezo ili hizo fedha zilipwe kwa vyama husika kuliko kupitia kiongozi wa upinzani. Bado hakujafanyika marekebisho yoyote. Sidhani kama serikali ikitoa Sh100,000,000 kwa ajili ya kambi ya upinzani, Chadema watazilamba wao peke yao (unless kama ndivyo kanuni za Bunge zinavyosema).

Naomba tujadili hoja kwa kuzingatia kipi kinazungumzwa na siyo ushabiki wa kisiasa. Nia yetu siyo kuonekana nani anajua kukosoa wengine bali kuweka njia mbadala ambazo kama viongozi wetu watazizingatia hatimaye tuna nafasi kubwa ya kurekebisha kasoro tulizonazo na kufanya vizuri zaidi kwa baadaye.
 
why Nguruwe na isiwe nyani? ina maana hajui nguruwe ni sacred animal kwa baadhi ya watu?

Hii inaonyesha jinsi gani moyo wake ulivyo jazwa na udini. Kwa kweli jambo ambalo ni la kijinga ambalo mlw JK alituingiza Watanganyika ni kutunganisha na hawa jamaa walio bobea katika ubaguzi wa kidini. Kumbe mwl aliligundua hilo ndio maana alijitahidi kulikemea sana lakini wapi, wakati huu wamewapata na vibaraka wao wa huku bara ndio hasa wanajitahidi tunase kwenye huo mtego. Watanganyika tulio wengi tumesha wastukia hata walio wachache wetu wanalikumbatia kwa maslahi yao binafsi sio ya dini zao, tafakari, chukua hatua.
 
Tumpe Mheshimiwa Rashid the benefit of doubt. Kama ni mchemshaji atachemsha tena tu. Tukumbuke mwanzoni mwa Mfumo wa Vyama vingi Baba wa Taifa alipata kusema "I cannot allow by Country go to the Dogs!" na mheshimiwa mmoja aliyekuwa ameingia kwenye vyama vingi kwa Munkari akadai kwamba Mwalimu alikuwa amewatukana Wapinzani kwa Kuwaita Mbwa! Ni Vionjo vya Lugha tu.
 
Kinachonifurahisha kwenye mjadala huu ni kuwa watu hawa hawa waliokuwa wanawapigia kelele CCM kukimbia midahalo leo wanaitaka CHADEMA nayo ikimbie mdahalo!

MWANZO WA KUISHIWA mara nyingi unakuwa namna hii!

Huu mdahalo ulitayarishwa kwa madhumuni ya kuishindilia msumari CUF na Chadema walitayarisha watu wengi kujaza ukumbi ili kumzomea Mh. Hamad Rashid. Fortunately, CUF walipata hizi taarifa na wao wakajaza watu wao. Sasa kama mngeendelea na mpango wenu wa kutaka kumzomea Mh. Hamad Rashid basi nyie mafisadi wadogo kutoka Sinza na Mbezi, mlionyang'anywa matonge na CCM, ndiyo mngekula kichapo kutoka kwa watoto wa Manzese, Buguruni, Kigogo, Tandika na Mbagala.

Mdahalo wa Hamad na Mbowe ilikuwa ni burudani ya CCM!Wana CCM waliburdika kuona wapinzani wakikwaruzana!
 
Wana Jf baada ya kufwatilia mdahalo wa jana kati ya Mh Hamad R na Mh Freeman, nilibaki na maswali mawili magumu kwangu dhidi ya kauli ya Mh Hamadi aliposema kuwa "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba".

Sasa je,
1 Mh Hamadi anafananisha washiriki (watu au vyama) wengine kwenye uchaguzi kama HARAMU?

2.Mh Hamad anatuambia kwamba siasa(shamba) imeingiliwa na watu HARAMU?

Hebu nisaidieni wana Jf

Alichokizungumza Mh Hamad ni kua alitumia mifano miwili tofauti kwa ajili ya kuwafahamisha watu na kufanya hivyo kunaitwa kufananisha. Kama tutachunguza vizuri tutakuta kua kufananisha kuna masharti yake ambayo ni lazima yakamilike. Sasa tujaribu kuangalia ni yapi hayo masharti ili tuweze kupata muangaza.

1-kinachofananishwa 2- kinachofananishiwa 3- njia zinazofanya hivyo vitu vfanane 4- hukumu ya kile ya kile kinacho fananishiwa.

Sasa tuje ktk maneno ya Mh ili tuone anajaribu kufananisha nini. Alisema "CUF kutoshiriki uchaguzi wa 2015 ni sawa na kuwaachia NGURUWE shamba". Kwa kuangalia maneno yake

1- kinachofananishwa ni Cuf 2- kinachofananishiwa ni Nguruwe 3- Njia zinazofanana kati ya Cuf na nguruwe ni kuacha mali yoyote bila ulinzi au bila usimamizi. 4- Hukumu yake ni kua hukutekeleza wajibu wako.

Haya kwa wachambuzi labda kwa kua alitajwa nguruwe wengi walishtuka lakin sidhani kua kwa maneno yale walifananisha hao washiriki na nguruwe na vilevile sio makubaliano ya wote kua nguruwe ni kitu kibaya kwani wapo ktk binadanu wanaokula nguruwe.
 
kwanini wasisubiri kukamata dola ili kubadilisha katiba ila wako tayari kusubiri kukamata dola ili kupunguza mishahara?

100M anataka kutumia na chadema tu ndio maana hataki kuungana na akina mrema. uchoyo umewatawala chadema
 
Kaka nna mashaka na kauelewa kako kwenye hii lugha kwa wale waliosoma miaka ya nyuma kati ya 80s na 90s wakati huo unaingia kufanya mtihani wa kiswahi ukilazimika kuielewa fasi simulizi, andishi na misemo, methali na wakati huo unawekusa swali linalokutaka uifafanue lugha kweli kweli, kwanyakati hizi za walimu wa vodafaster ningumu sana kwa mwalimu kumfanya mwanafunzi wake kuwa mahili kwenye lugha ya kiswahili.

Kama kumbukumbu zangu ni nzuri miaka twajwa ndio nimemaliza shule ya msingi, sekondari, na chuo kikuu, ila kufikiria kwa kuangalia kwa mitizamo ya kiswahili kinavyo maanisha tu, wakati kiswahili kilikuwa kinatumiwa na mwanasisa ambaye kwa kuuangalia uso wake unayaona maslahi yake ni zaidi ya siasa anayoiongelea. Mie shule yangu haikunipa elimu finyu kiasi hicho
 
Kuna msemo wa kiswahili [ Ukicheka na nyani utavuna mabua] nafikiri mh Hamad alikuwa na maana ya kuwaachia ccm ni sawa na huo msemo hapo juu Lakini kwa sababu ni mwislamu haikuwa sahihi kwake kutumia neno nguruwe
 
Mimi naona tunachanganya vitu. Kuna Official opposition ambao ndio wanaopewa fursa ya kuunda serikali kivuli. Serikali hii hailazimiki kuwakilisha wabunge wote ambao hawamo katika chama tawala. Pesa zinazotolewa ni kwa ajili ya kuendesha hii serikali na si kwa ajili ya kambi ya upinzani maana hamna kitu kama kambi ya upinzani bali vyama ambavyo havikuunda serikali. Tukichukulia mfano kwa wenzetu, chama cha Labour kama official opposition party hakiwajibiki kushirikiana na wakina Respect au BNP kwa vile havimo katika serikali tawala. Kama Chadema wataunda serikali kivuli kutokana na wabunge wao peke yao bila kuwashirikisha wengine ( kitu ambacho si lazima) basi itabidi watumie pesa yote hiyo kwa ajili ya shughuli hiyo kubwa na muhimu na si kuigawa kama takrima kwa vyama vingine.

Amandla......
 
Jenifa,
Nadhani ni vizuri kuelewa msingi wa hoja ya chadema ya kujadiliwa kwa Katiba. Hata swala la mishahara mikubwa ya Wabunge ni swala la Mfumo. Ndio msingi wa Mbowe kujibu kuwa "Chadema ingelishinda ingelibadilisha Mafao hayo". sidhani kama Mbowe alikataa kujibu swali. Nilikuwapo na nilimsikiliza live na siyo kwenye TV. Hivyo deliberate efforts za kupotosha si vema zikaachiwa. Hata hivyo kwa wale wasiofahamu ni vizuri nikaeleza mfumo wa kupanga Mishahara na Posho za Wabunge:
i) Kwa sasa Mishahara ya Wabunge inapangwa na Tume ya Huduma za Bunge ( yaani Parliamentary Service Commmission) ambao wajumbe wake wengi wanatoka CCM. Wapinzani katika Commission ni wachache sana na hata ikipigwa kura watashindwa daima kama ilivyo ndani ya ukumbi. Ni tatizo la kimfumo na ni tatizo la ukiritimba wa Chama kimmoja. Ndio hoja ambayo siku zote tumeiweka kwa Watanzania, ndio maana tumekuwa tukisema " Watanzania wenyewe ndio wanaosababisha kwa sehemu kubwa umaskini wao kwa kuchagua wabunge wa Chama kimmoja". Ukiachilia mbali uchakachuaji uliofanyika, nafurahi kuwa Watanzania wamelitambua hilo na ndio maana idadi ya Wabunge wa Upinzani imeongezeka sana. Pasingelikuwa na Uchakachuaji, nina hakika ukombozi ungelikuwa umefika au ungelikuwa mlangoni. Hivyo isingelikuwa Busara kwa Mbowe kujibu hoja ambayo hana mamlaka nayo na wale hawezi kwa njia yeyote ile " kuibadili:" au hata ku " influence". Msingi huu ukifahamika vizuri, hoja yako ya kwanza inakuwa haina mshiko wowote.
ii) Tume ya Huduma ya Bunge inatokana na Katiba Mbovu na Sheria zake. Hivyo ukifanikiwa Kubadili au kupata Katiba mpya, ndio ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo. Kumbuka, kuwa Tume ya Bunge "inapendekeza" kwa Rais, na ukiwa na Rais makini, atakataa kupitisha mapendekezo ambayo yanaifilisi Taifa. Rais wetu kwa mujibu wa Katiba aikiisha kuipitisha hakuna mahali pengine unaweza kuhoji, au kama utataka kumhoji kuna utaratibu mgumu sana wa kuihoji Serikali mahakamani, kwanza "lazima utoe Notice nadhani ya siku 90, kisha upate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mara nyingi kibali hicho hakitolewi". Tumekwisha kujaribu njia hizo katika kipindi changu cha miaka 15 Bungeni lakini ilishindikana. Hivyo jibu pekee ni Marekebisho makubwa ya Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais (Excessive powers).
iii) Katika hoja yako ya pili kuhusu kuunganisha nguvu za Upinzani, unazungumzia Chadema kuchukua 100M kwa kuunda Serikali Kivuli. Ni kweli Utaratibu wa sasa, tena ambao hauko ndani ya Sheria, wala Kanuni unatenga kila Mwaka Bajeti ya Tshs 100 Millioni kwa "Kiongozi wa Upinzani". Hivyo Ungelifanya utafiti, hoja yako isingelikuwa flawed kama sasa a) Chadema haina haki wala haiwezi kuvuta 100 million kutokana na kuundwa kwa Kambi ya Upinzani kwa vile fedha hizo zimetengwa, kwa kilichoelezwa jana na Mhe. Hamad kama ulimsikiliza vizuri kuwa ni kwa "Kiongozi wa Upinzani" wala siyo kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani. Conclusion yako ni matokeo ya kutokusikiliza vizuri na kutokufanya utafiti. Hamad amekuwa Kiongozi wa Upinzani toka 2005 hadi 2010, alitakiwa kuulizwa hizo fedha alizutumia kwa kazi gani, na Katibu wa Bunge anatakiwa kutoa hadharani matumizi ya fedha hizo ili Watanzania waone zilitumika kwa kazi gani na kwa manufaa ya nani. Kama hazikutumika kwa manufaa ya watanzania wana haki ya kupiga kelele kwani millioni 100 ni fedha nyingi na zingeweza kujenga madarasa kadhaa kupunguza upungufu wa madarasa au zahanati. b) Mimi nilikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani, katika miaka yangu yote niliyokuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani sijawahi kuona Break down ya fedha hizo na matumizi yake. Tulipodai zitumike kwa gharama za ofisi mathalan, kumlipa "mratibu wa Kambi"ambaye kwa taarifa yako "ameajiriwa" na Kambi na mishahara(posho zake zinalipwa kwa kuchangiwa na wabunge wenyewe ambao tulikuwa tunakatwa kutoka kwenye mishahara na posho zetu wakati kuna fedha za Kiongozi wa Upinzani), tuliambiwa kuwa hizo ni za Kiongozi wa Upinzani na labda fungu lingine litafutwe kwa ajili ya Kazi za Kambi. Ungelifanyia utafiti swala hilo usingelitoka na hoja kuwa Chadema wanachukua hizo fedha, kwani Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema hadi jana, haijapokea fedha zozote kutoka Ofisi ya Bunge ( labda Gari rasmi la Kiongozi wa Upinzani, ambalo sina hakika hata kama linahudumiwa na kasma hiyo). Hoja yake inaweza pia kugeuzwa kuwa Hamad hataki kuungana na Chadema kuunda Kambi rasmi kwa vile kama alivyokuwa Dr. Slaa, Naibu Kiongozi wa Kambi ambaye hakuwa anajua hizo fedha zilifanya nini, naye sasa atakuwa Naibu hivyo hatakuwa na fedha. Labda kwa kuunda Kambi "ndogo isiyo Rasmi" naye pia kwa mlango huo huo anaweza kupewa mafao kama ya Kongozi wa Upinzani yaani gari, Ofisi, Nyumba na Fedha 100 Millioni. Lakini tukumbuke tukiendekeza kugawa fedha, Kodi za Watanzania maskini kwa mtindo huu, hatutafika na Taifa litaendelea kuporomoka na kuzama katika lindi la Umaskini.
iv) Mtafiti wa kweli angeliuliza, na Jenifer angeliuliza swali kwenye Mdahalo au hata kwenye JF kuwa " Je Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema itaendelea kutumia hizo 100 Million kwa matumizi Binafsi ya Kiongozi wa Upinzani au kwa matumizi ya shughuli za Kambi mathalan utafiti na kazi za mawaziri Kivuli, nina hakika angelipata jibu sahihi kuliko kufanya conclusion kwenye "hisia" ambazo nazo kama tulivyoona jana kwenye mdahalo zinaweza kuwa na sababu zake.
Jenifer, naamini nimeweza kutoa mchango wangu kwa manufaa ya wana JF wote ambao hawajui hizi fedha kama zilikuwepo, ziko, na kama ziko zinalenga kufanya kazi gani chini ya uongozi mpya wa Kambi ya Upinzani inayoongozwa na Chadema.

mdahalo wa jana ulinishangaza sana kuhusu mbowe kwenye mambo mawili

(i) anataka kujadili katiba ili kuondoa ulaji wa CCM lakini hataki kujadili mishahara mikubwa ya wabunge ili kuondoa ulaji wa wabunge

(ii) anakataa kuunganisha nguvu za upinzani na vyama vingine kumbe kuna 100M ambazo chadema wanachukua kwa kuunda serikali kivuli. hataki agawaned hizi pesa na akina mrema

hawa ndio viongozi wetu wapendwa
 
- Mkuu tatizo la Wapinzani kutokuuungana ndipo hasa kwenye mtaji wa CCM kutawala hili taifa kwa muda mrefu sana, I mean realistically itachukua miaka mingapi chama kimoja cha upinzani Tanzania, kuweza kuingiza majority ya wabunge bungeni bila ya kuungaana na vyama vingine?

- I mean ni chama gani cha siasa Duniani ambacho lengo lake sio kushinda uchaguzi na kutawala, utafanya mageuzi gani kama hutawali? Au hata kua na harufu ya kutawala? Kweli unaamini kwamba Chadema on its own wana uwezo wa kuwalazimisha CCM, kubadili katiba? CCM sawa wana mapungufu makubwa sana kwenye uongozi, lakini hawajawahi kuwa na mapungufu kwenye ku-figure out how to stay in power, I mean politically Wapinzani wawili wanapopigana lazima kuna atakayefaidika na ile vita na huhitaji kuwa na PhD kujua mshindi wa vita vya leo ni nani,

- Chadema wanahitaji sana kuwa strong Bara na Visiwani pia, kwa mwendo wa huu mdahalo wa leo hiyo ni ndoto ya muda mrefu saaaana, CCM hawawezi kuwa wajinga kukubali serikali ya Muafaka kwenye uchaguzi huu unafikiri waliona nini mbele? Ni lazima walijua kwamba CUF wakishinda uchaguzi Visiwani wakashika nchi ni rahisi sana kuhamishia mabadiliko hayo huku Bara, kuyazuia ilikuwa lazima kukubali muafaka in the process kuwagawa zaidi Wapinzani kama ilivyothibitishwa leo na huu mdahalo, I mean nothing personal lakini Demokrasia inaturuhusu kutoa analysis tofauti kwa the same political event!

Thaanks!

William.

mwanangu pole kwa uchungu wa kuona mageuzi hayaendi unavyo pendelea hakika huhitaji kuwa na shahada ili kuona kwamba hapahitajiki kuunganisha vyama kuna mfano kuwa panya mia wakiungana akija paka hakuna panya atakaye simama vivo hivyo kwa hivi vyama vina malengo yake na njia za kufikia hayo malengo acha walumbane ili wanananchi tuwe na uwanja mpana wa kupime nani mtetezi wao halisi....
 
kwanini wasisubiri kukamata dola ili kubadilisha katiba ila wako tayari kusubiri kukamata dola ili kupunguza mishahara?

100M anataka kutumia na chadema tu ndio maana hataki kuungana na akina mrema. uchoyo umewatawala chadema

100 milioni si takrima bali ni za kuendesha wizara vivuli. Mawazo kuwa kila pesa inayoingia ni ya ulaji ndio unaofanya tuzidi kudumaa. Hamna uchoyo hapa.

Nilikuwa sijamsoma Dr. Slaa hapo juu. Kumbe alikuwa anakatiwa kiongozi wa upinzani na hakulazimika kuzitolea maelezo! Kwa mtaji huu, tutafika kweli?

Amandla.....
 
Hamad na mfanowe wa nguruwe naona hakujibu swali halisi, watu wengi wamerukia maneno aliyotumia bila kuona kama je mfano wake una kidhi kujibu swali kuhusu uchaguzi wa 2015? Kwa tafsiri ya haraka, hamad alimaanisha cuf hawawezi kuwaachia ccm "kula" ama "ulaji" wa uchaguzi ujao, nionavyo kwa wao hata katiba isipobadilishwa Hilo haliwaumizi cuf?Na kwanini? Au wao kugombea ni ulaji ilhali wanajua fika na katba ilyopo hawawezi shinda? Mfano wa nguruwe naona unatafsiri kubwa kuliko maneno yaliyotumiwa.
 
Jenifa,
Nadhani ni vizuri kuelewa msingi wa hoja ya chadema ya kujadiliwa kwa Katiba. Hata swala la mishahara mikubwa ya Wabunge ni swala la Mfumo. Ndio msingi wa Mbowe kujibu kuwa "Chadema ingelishinda ingelibadilisha Mafao hayo". sidhani kama Mbowe alikataa kujibu swali. Nilikuwapo na nilimsikiliza live na siyo kwenye TV. Hivyo deliberate efforts za kupotosha si vema zikaachiwa. Hata hivyo kwa wale wasiofahamu ni vizuri nikaeleza mfumo wa kupanga Mishahara na Posho za Wabunge:
i) Kwa sasa Mishahara ya Wabunge inapangwa na Tume ya Huduma za Bunge ( yaani Parliamentary Service Commmission) ambao wajumbe wake wengi wanatoka CCM. Wapinzani katika Commission ni wachache sana na hata ikipigwa kura watashindwa daima kama ilivyo ndani ya ukumbi. Ni tatizo la kimfumo na ni tatizo la ukiritimba wa Chama kimmoja. Ndio hoja ambayo siku zote tumeiweka kwa Watanzania, ndio maana tumekuwa tukisema " Watanzania wenyewe ndio wanaosababisha kwa sehemu kubwa umaskini wao kwa kuchagua wabunge wa Chama kimmoja". Ukiachilia mbali uchakachuaji uliofanyika, nafurahi kuwa Watanzania wamelitambua hilo na ndio maana idadi ya Wabunge wa Upinzani imeongezeka sana. Pasingelikuwa na Uchakachuaji, nina hakika ukombozi ungelikuwa umefika au ungelikuwa mlangoni. Hivyo isingelikuwa Busara kwa Mbowe kujibu hoja ambayo hana mamlaka nayo na wale hawezi kwa njia yeyote ile " kuibadili:" au hata ku " influence". Msingi huu ukifahamika vizuri, hoja yako ya kwanza inakuwa haina mshiko wowote.
ii) Tume ya Huduma ya Bunge inatokana na Katiba Mbovu na Sheria zake. Hivyo ukifanikiwa Kubadili au kupata Katiba mpya, ndio ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo. Kumbuka, kuwa Tume ya Bunge "inapendekeza" kwa Rais, na ukiwa na Rais makini, atakataa kupitisha mapendekezo ambayo yanaifilisi Taifa. Rais wetu kwa mujibu wa Katiba aikiisha kuipitisha hakuna mahali pengine unaweza kuhoji, au kama utataka kumhoji kuna utaratibu mgumu sana wa kuihoji Serikali mahakamani, kwanza "lazima utoe Notice nadhani ya siku 90, kisha upate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mara nyingi kibali hicho hakitolewi". Tumekwisha kujaribu njia hizo katika kipindi changu cha miaka 15 Bungeni lakini ilishindikana. Hivyo jibu pekee ni Marekebisho makubwa ya Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais (Excessive powers).
iii) Katika hoja yako ya pili kuhusu kuunganisha nguvu za Upinzani, unazungumzia Chadema kuchukua 100M kwa kuunda Serikali Kivuli. Ni kweli Utaratibu wa sasa, tena ambao hauko ndani ya Sheria, wala Kanuni unatenga kila Mwaka Bajeti ya Tshs 100 Millioni kwa "Kiongozi wa Upinzani". Hivyo Ungelifanya utafiti, hoja yako isingelikuwa flawed kama sasa a) Chadema haina haki wala haiwezi kuvuta 100 million kutokana na kuundwa kwa Kambi ya Upinzani kwa vile fedha hizo zimetengwa, kwa kilichoelezwa jana na Mhe. Hamad kama ulimsikiliza vizuri kuwa ni kwa "Kiongozi wa Upinzani" wala siyo kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani. Conclusion yako ni matokeo ya kutokusikiliza vizuri na kutokufanya utafiti. Hamad amekuwa Kiongozi wa Upinzani toka 2005 hadi 2010, alitakiwa kuulizwa hizo fedha alizutumia kwa kazi gani, na Katibu wa Bunge anatakiwa kutoa hadharani matumizi ya fedha hizo ili Watanzania waone zilitumika kwa kazi gani na kwa manufaa ya nani. Kama hazikutumika kwa manufaa ya watanzania wana haki ya kupiga kelele kwani millioni 100 ni fedha nyingi na zingeweza kujenga madarasa kadhaa kupunguza upungufu wa madarasa au zahanati. b) Mimi nilikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani, katika miaka yangu yote niliyokuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani sijawahi kuona Break down ya fedha hizo na matumizi yake. Tulipodai zitumike kwa gharama za ofisi mathalan, kumlipa "mratibu wa Kambi"ambaye kwa taarifa yako "ameajiriwa" na Kambi na mishahara(posho zake zinalipwa kwa kuchangiwa na wabunge wenyewe ambao tulikuwa tunakatwa kutoka kwenye mishahara na posho zetu wakati kuna fedha za Kiongozi wa Upinzani), tuliambiwa kuwa hizo ni za Kiongozi wa Upinzani na labda fungu lingine litafutwe kwa ajili ya Kazi za Kambi. Ungelifanyia utafiti swala hilo usingelitoka na hoja kuwa Chadema wanachukua hizo fedha, kwani Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema hadi jana, haijapokea fedha zozote kutoka Ofisi ya Bunge ( labda Gari rasmi la Kiongozi wa Upinzani, ambalo sina hakika hata kama linahudumiwa na kasma hiyo). Hoja yake inaweza pia kugeuzwa kuwa Hamad hataki kuungana na Chadema kuunda Kambi rasmi kwa vile kama alivyokuwa Dr. Slaa, Naibu Kiongozi wa Kambi ambaye hakuwa anajua hizo fedha zilifanya nini, naye sasa atakuwa Naibu hivyo hatakuwa na fedha. Labda kwa kuunda Kambi "ndogo isiyo Rasmi" naye pia kwa mlango huo huo anaweza kupewa mafao kama ya Kongozi wa Upinzani yaani gari, Ofisi, Nyumba na Fedha 100 Millioni. Lakini tukumbuke tukiendekeza kugawa fedha, Kodi za Watanzania maskini kwa mtindo huu, hatutafika na Taifa litaendelea kuporomoka na kuzama katika lindi la Umaskini.
iv) Mtafiti wa kweli angeliuliza, na Jenifer angeliuliza swali kwenye Mdahalo au hata kwenye JF kuwa " Je Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema itaendelea kutumia hizo 100 Million kwa matumizi Binafsi ya Kiongozi wa Upinzani au kwa matumizi ya shughuli za Kambi mathalan utafiti na kazi za mawaziri Kivuli, nina hakika angelipata jibu sahihi kuliko kufanya conclusion kwenye "hisia" ambazo nazo kama tulivyoona jana kwenye mdahalo zinaweza kuwa na sababu zake.
Jenifer, naamini nimeweza kutoa mchango wangu kwa manufaa ya wana JF wote ambao hawajui hizi fedha kama zilikuwepo, ziko, na kama ziko zinalenga kufanya kazi gani chini ya uongozi mpya wa Kambi ya Upinzani inayoongozwa na Chadema.

Thanks umenifanya hata mimi niwe wiser than i was a minute ago..... Je kama wananchi tukijipanga na kusign petition ya kudai katiba ili kuondokana na huu upuuzi, itasaidia kwenye movement yetu. Signed petition has been known to work in other countries, Je? itafanya kazi tanzania
 
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees!!!!! POWERRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR!!

Asante kwa kuwakilisha mheshimiwa Rais, Mapinduzi daima!!

Dadaangu wanye busara wanasema usipande juu ya mti wakati nguo uliyovaa imetoboka ktk makalio (mimi naongezea usipande juu ya mti ukiwa umevaa sketi bila skin tight au underwear) MAANA WATU WATAONA UTUPU WAKO.

Inawezekana mdahalo uliusikiliza lakini hoja zilivyokuwa zinaongelewa hukuwa ukizielewa, lakini wewe ulidhani unazielewa. MHE HAMAD RASHID aliweka wazi kuwa kiongozi wa upinzani bungeni katengewa bajeti ya tsh 100mil, na wao kama wapinzani ktk bunge la 9 walikuwa wanapigania kuwepo na bajeti ya seriksli ya upinzani na si bajeti ya kiongozi wa upinzani. na haksisitiza hoja hiyo ya kudai bajeti ya upinzani iendelezwe. HIVYO fedha hizo tsh 100 mil haziendi CHADEMA bali ni za Mkuu wa kambi ya upinzani BUNGENI ambaye ni MBOWE anazitumiaje ni suala la muda maana ajaanza kuzipata, HAMAD alipokuwa mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni alizitumiaje? kama ulimfuatilia vizuri maelezo yake ya jana jibu unalo.

Suala la katiba na mishahara ya wabunge ni vitu viwili tofauti sana na vinatofautiana hata kwa ukubwa na uzito wake kama ni ukubwa KATIBA ni mlima kilimanjaro na Mishahara ya wabunge ni mlima senkeke kama unaijua milima hii utabaini tofauti yake, Mishahara ya wabunge inamchango mdogo sana ktk kudidimiza uchumi wetu na ukifuatilia kiundani unaweza ukabaini kuwa impact yake ktk uchumi wa tanzania ni ndogo sana, hoja ya CHADEMA ni kuwa watumishi wa umma na sekta binafsi wanalipwa mishahara midogo sana wakati tofauti ya mishahara yao na wabunge wao ni kubwa mno (hapa zingatia kuwa ni mishahara na posho walipwazo wabunge) hapa utujaangalia wakulima. kumbuka wakulima na wafanyakazi ndio wapiga kura wakubwa wa wabunge. Yaani wabunge hawawatendei haki wapiga kura wao kwa maana mfanyakazi wa kima cha chini mshahara wake wa mwezi ni pungufu au sawa na posho ya mbunge ya siku moja. Hivyo hoja hapa ni wabunge kupigania maslahi ya wananchi wote na si kuangalia maslahi yao binafsi, kama standard of living ya TANZANIA inaruhusu malipo ya kimacha chini cha 100,000/ kwa mwezi (sasa ni 135,000/=) basi wabunge waadjust mishahara na posho zoa ziendane na hali hiyo hiyo ndio hoja ya CHADEMA na kama wabunge hawataki kushusha mishahara yao basi wahakikishe wa wafanyakazi inapanda kukidhi hali ya maisha na kipato cha mkulima na cho kinaongezeka kukidhi hali ya maisha huku mfumuko wa bei ukidhibitiwa. Hivyo hoja hii ni ya msingi lakini si kuzidi katiba.
KATIBA ndio sheria mama, yaani ni mama wa sheria zote hapa nchini, sheria yeyote ikienda kinyume na katiba sheria hiyo ni batili. KATIBA ndio inayobeba na kutoa HAKI ZA BINADAMU na inatoa misingi ya uongozi wa nchi, ina hainisha haki za raia inaweka taratibu za mfumo wa kiuongozi katika nchi, kiufupi katiba ndio muongozo wa kimsingi wa utawala,sheria,utamaduni na mahusiano ya kimataifa. KATIBA ndio msingi wa Taifa hivyo si sawa kulinganisha katiba na mishahara ya wabunge ni vitu viwili tofauti kabisa.

JENIFA tukipata KATIBA mpya iliyokidhi mahitaji yote ya TAIFA na inayothamini watu wote na inayotoa dira ya ulinzi wa RASILIMALI zetu na kusisitiza usawa kwa kuuwa matabaka ndani ya nchi, SI AJABU tatizo la mishahara mikubwa na ya kinyonyaji ya wabunge likamalizwa kirahisi na wananchi wenyewe kwa kutumia nguvu ya UMMA bila kutegemea wabunge au CHADEMA.

HIVYO narudia JENIFA ni vyema utafakari kabla ya kusema/kuandika maana THREAD zako zinaweza kuonyesha jinsi gani usivyo na ueledi wa mambo ya msingi kwa nchi yako. jifunze kwa kusikiliza sana na kutafakali uku ukiongea kidogo. busara na hekima uja kwa kukirimiwa na MUNGU lakini ueledi uja kwa kujifunza.
 
Nakubaliana nawe. Ushauri wangu ni kuwa kwa siku zijazo, badala ya kila mtu kuamua kuwa anataka kuhudhuria mdahalo, ni vema waandaji waweke vigezo vya watu wanaoruhusiwa, na kabla ya mdahalo washiriki wasomewe kanuni, na pia kuwepo panel ya watunza nidhamu/kanuni za mdahalo. Wale ambao watakiuka taratibu watolewe nje mara moja.
 
mkuu ..... kwa kuwa wahudhuria midahalo wanaonyesha jazba na kuwa na hulka hasi.... nadhani wakati mdahalo ukipendekezwa basi mada itolewe na watu watume maswali kwa waandaa mada..... kwenye mdahalo wawe watoa mada tu na mwendesha mdahalo... maswali yenye tija na yenye mantiki yataelekezwa kwa wahusika kwa kumtaja aliyeuliza na anapotokea... hapo ndio tutapata fursa ya kunufaika na mdahalo
 
Tumpe Mheshimiwa Rashid the benefit of doubt. Kama ni mchemshaji atachemsha tena tu. Tukumbuke mwanzoni mwa Mfumo wa Vyama vingi Baba wa Taifa alipata kusema "I cannot allow by Country go to the Dogs!" na mheshimiwa mmoja aliyekuwa ameingia kwenye vyama vingi kwa Munkari akadai kwamba Mwalimu alikuwa amewatukana Wapinzani kwa Kuwaita Mbwa! Ni Vionjo vya Lugha tu.

Mwl JK alimaanisha mbwa kweli, na kila wakati na sema huyu bwana MUNGU alimjalia akili na hekima zisizo za kawaida. Jaribu kukumbuka upinzani wa wakati ule ulijazwa na viongozi wa aina gani? Kuwa viongozi hao walikuwa wana akili zilizo oshwa ambazo zina subiri wengine wafikirie na kuamua halafu wao watumwe kutekeleza matakwa ya walio amua na wakati mwingine bila hata kujiuliza madhara ya yale watakayo ya tekeleza. Nitakupa mfano askari FFu anaamriwa kampige mwl anayendamana kuadai maslahi mazuri ili afumndishe vizuri manafunzi wa FFU anaye mpiga aliye shule kwake. Huyu FFU utamchukulia je?akili yake imeoshwa au? Sijui hata viongozi wengi wetu wa sasa wako kwenye kundi gani? kwamuji wa Mwl anyway. Ila umenifanya nikumbuka ya MPendazoe na ukomavu wa akili. By the way akili zilizooshwa huwa zinafanishwa na mbwa, Na mbwa kwa hulka yake huwa anaitii amri ya bwana wake haijalishi ana njaa au akashiba
 
Tatizo ni mfumo mbovu,Mbowe yuko sahihi na nikweli ungekuwa Mtihani ungepata zero kabisa please fikilia kabla ya kuandika!
 
Back
Top Bottom