Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

kiswahili cha pwani hicho... kwamaana ni sawa na kususia mechi ya mchezo kama mpira vile...ukisusa unapoteza point 3 na goi 3... kwahiyo wao CUF hawawezi kufanya hivyo...

Halafu huyu bwana alijisifia kuwa ni mwana siasa mkongwe kwa kumuonya Mbowe asicheze na wanasisa wakongwe kama yeye na huwa ni makini kwelikweli kwenye kutoa. Sasa kauli tata huwa ni kauli makini. Watu makini wajisifii wenyewe na ukiona husifiwi na wengine bsi jua huna umakini wowote
 
Kiukweli ulioitwa mdahalo wa jana...sikupata mantiki murua yenye dira kwa watanzania tuliotegemea majibu muafaka toka kwa wawili hao.
Nilichokiona tena nikiwa nipo makini saana ilikuwa ni kama njia ya KUUPATANISHA UPINZANI BUNGENI NA UWE NI KITU KIMOJA, hii ndio hali ya kiujumla niliyoiona.
Muongozaji hakuwa taff & punctual kuweza ku-control based topic on her table...na badala yake hakukuwa na dira ya madahalo huo ambapo hata zile vurugu zilizotekea pale ILIKUWA NI SAHIHI KWANI HAKUKUWA NA DIRA ELEKEZI NA ILIYOSIMAMIWA KIKAMILIFU.
MBOWE: Alijitahidi kwa baadhi ya mambo kujaribu kuyaelezea, ila hana uwezo mzuri wa kuchambua mambo na kujipanga kwa PAPO-KWA-PAPO kimaswali ili awakidhi watazamaji na wanachama wake. Aliyumba sana katika kutoa misimamo na maelekezo muhimu kwake na chama chake, aelewe watanzania tunahitaji umoja toka kwao...hivyo angetumia uungwana tu wa kuwajumuisha hata akina Cheyo, Mrema na akina Rashidi katika kambi ili kuleta umoja wa watanzania na kuimarika kwa demokrasia. Mwenzake Hamad Rashid aliweka bayana ni kwa kiasi gani walivyoipigania kifungu cha sheria bungeni katika kutoa wasaa kwa kambi ya upinzani ipate fursa walau stahili, HR alishirikiana na Slaa kulifanikisha hili. Ikumbukwe UMOJA NI NGUVU, Leo hii ndani ya wabunge fulani wa chadema hawaelewani...suluhisho ni kuwa na umoja wa dhati ili taswira njema na nzuri iwepo kwa watanzania kuwaamini hawa viongozi wetu wa kisiasa.
HAMAD RASHID: Alijitahidi kiasi chake kupambanua mambo kwa uzoefu wake wa kuwa waziri na mbunge mkongwe, kilichompeleka ng'ambo kidogo ilikuwa ni hali yake ya KUKASIRIKA ambayo kwa yeyote yule humtoa ulingoni na kumpotezea dira...ila thanks that ulirejea katika hali ya utulivu. Hoja alizozieleza HR zili-base zaidi kuitetea zanzibar kwa jinsi muongozaji alivyokwenda mrama kwa kutozingatia mada husika, alitumia misemo fulani ikiwa ni kiashiria cha hoja aliyokuwa akiielezea. HR aliongelea kundi hili la 'minority' ambalo litabakia ilimradi wapo lakini hawana upande wa kuegemea, hoja ya HR ililenga kuwasaidia akina mrema ambao hawana cha kuegemea katika katiba za sasa zilivyo, NI AFADHALI WANGEUNGANA HAWA minority pamoja na chadema NA KULETA PICHA MOJA ILIYO NA NGUVU KWAMBA ''KAMBI YA UPINZANI BUNGENI'' kwa manufaa ya watanzania na wapiga kura wote, vinginevyo 2015 wananchi watahangaika kuwa na dira kwa kutokana na kutokuwa na ushurikiano wa hivi vyama vya upinzani mara wapatapo nafasi.

Ila kwa sababu tupo hot kiitikadi na ushabiki wa vyama...hatutaweza kuichambua vema walivyopotoka wote wawili zaidi ya sisi kubakia kushabikia upande fulani, KIUKWELI NI MARA MIA SLAA AU KABWE ANGESIMAMA PALE ANGETUKIDHI kiuelewa na kumtazamo bali wangetufanikishia kutupatia the way forward.
 
utuambie alisema nini na maana yake nini? Hata kama alitumia nahau au methali vyote hivyo vina maana siyo kutumika tu. Rejea hoja ya msingi ya wachangiaji na utuweke sawa. Tatizo siyo kiswahili.

labda angetumia neno kiti moto ndio ungemuelewa!!!!! AU MUULIZE MCHUNGAJI MASANILO!!!!
 
Hamad analia na 100mn ya kiongozi wa Upinzani ambayo sasa inaenda Chadema yote ndiyo hasa kilio chake na tamaa ya madaraka maana hata huko anakotaka minority yet anataka kuwa kiongozi kwa nini asiwaachie wengine wawe viongozi ? CUF kujitapa kwao hakuishi Lipumba kesha rusha kijembe kwa Slaa na jana Hamad karusha kwa Mbowe wacha tuone lakini majibu jana niliyapata kwamba CUF wanalilia posho ya kiongozi wa Bunge nk.
 
Hiyo ni misemo ya Kiswahili wadau sioni kama kuna kibaya hapo. Kama mtakumbuka Nyerere alisema mwaka 1995 i can llet my country gone to the DOGS (i stand to be corrected) sasa magazeti yakaandika sana kwamba Nyerere kasema hawezi kuwaachia mbwa nchi yake, kumbe ni misemo ya Kiingereza na LUGHA yetu TUKUFU (Kiswahili)jamani, mjifunze na KISWAHILI wadau. siku hizi LUGHA yetu inapotoshwa sana kila neno linakuwa sometimes kama tusi basi ni bola liende tuuuuuu.
 
Hivi wana JF mna mawazo mgando au? Mh. HR alichosema ni ukweli mtupu kwamba wao kama wao mtu ambaye dini yake hawezi kutawala, Nyerere mimi napenda kumuita Kambarage aliposema I can't allow my to go dogs alikuwa anamaanisha kuwa yeye hatakubali kuona mtu ambaye si mwana CCM anatawala. Je HR alikuwa anamanisha nini?
 
Yaani hata Kiswahili ni tatizo kwenu? Inaonyesha wengi wenu mlikuwa mnakimbia somo la Kiswahili darasani na badala yake mlikuwa mnakimbilia masomo mengine.

Mh. Hamad Rashid kamtoa show DJ na mmiliki wa only strip bar in Tanzania. Akabaki kujichekeshachekesha tu!

Chuki hizi hazisaidii ungaliweza kaa kimya na ukafanikiwa badala ya kuonyesha chuki ambazo si msaada kwako na Taifa una shida na Mbowe unajua pa kumpata why matusi hapa ?
 
Hivi wana JF mna mawazo mgando au? Mh. HR alichosema ni ukweli mtupu kwamba wao kama wao mtu ambaye si dini yake hawezi kutawala, Nyerere mimi napenda kumuita Kambarage aliposema I can't allow my to go to dogs alikuwa anamaanisha kuwa yeye hatakubali kuona mtu ambaye si mwana CCM anatawala. Je HR alikuwa anamanisha nini?
 
Ninachokiona, hivi vyama vya siasa havijatuli kabisa. Beleive me or not...CCM wako pembeni wanasoma weakness za hawa wanasiasa and in the near future vyama vyetu vyaweza kuparanganyika kabla havijaanza tena kupita mtaani kwa OPERESHENI SANGARA etc ili kuwapa tena moyo wananchi baada ya kuparanganyika...
all of the spoken agenda are very well planned, sisi vijana tuwe makini katika kuwasoma na kuchukua uzoefu mzuri wa political leaders wetu katika kutuongoza, coz wanayumba sana.
 
Tumpe Mheshimiwa Rashid the benefit of doubt. Kama ni mchemshaji atachemsha tena tu. Tukumbuke mwanzoni mwa Mfumo wa Vyama vingi Baba wa Taifa alipata kusema "I cannot allow by Country go to the Dogs!" na mheshimiwa mmoja aliyekuwa ameingia kwenye vyama vingi kwa Munkari akadai kwamba Mwalimu alikuwa amewatukana Wapinzani kwa Kuwaita Mbwa! Ni Vionjo vya Lugha tu.

Sasa hebu jaribu kumuangalia huyo muheshimiwa aliye pata munkari hivi sasa mwenendo wake vipi? Je hali matapishi yake kma mbwa? Na kwa mtazamo wako wa sasa Mwl was right or not?
 
Kuna msemo wa kiswahili [ Ukicheka na nyani utavuna mabua] nafikiri mh Hamad alikuwa na maana ya kuwaachia ccm ni sawa na huo msemo hapo juu Lakini kwa sababu ni mwislamu haikuwa sahihi kwake kutumia neno nguruwe


upumbavu, yaani dini ya mtu inakufanya umuchagulie maneno ya kutumia ktk matumizi yake ya lugha, hivi kwa nini watu kila kitu mnakilink na udini hamna kazi ya kufanya- msemo wa Hamad Rashidi upo uchi nini hakieleweki hapo au ushabiki tu
 
Hivi wana JF mna mawazo mgando au? Mh. HR alichosema ni ukweli mtupu kwamba wao kama wao mtu ambaye dini yake hawezi kutawala, Nyerere mimi napenda kumuita Kambarage aliposema I can't allow my to go dogs alikuwa anamaanisha kuwa yeye hatakubali kuona mtu ambaye si mwana CCM anatawala. Je HR alikuwa anamanisha nini?


Kambarage huyo huyo kwa mujibu wake mwenyewe, ndiye aliyeisifia katiba ya cdm kati ya zile alizosoma za vyama vya upinzani. Tena yeye huyo huyo akawaita wapinzani mbwa na inasemekana alio waita mbwa ati walkwienda kumuona msasani. Hivi hawa mbwa walikuwa wapinzani wote au baadhi yao?
 
Ule ulikuwa ni mdahalo mbovu katika midahalo yote niliyowahi kuiona, kuisikia au kuhudhuria.

Kwanza Mwenyekiti alikuwa hajui akifanyacho. Alikuwa ana act kama vile ni mwenyekiti wa kikundi cha kuigiza.

Huyo Mbowe ndio kabisaa, hata sijui alikuwa anaongea nini, mara Rais tunamtambuwa, Mara serikali tunaitambuwa mara Matokeo jinsi yalivyotolewa hatuyaytambuwi, yaani ni kama komedi origino, na ataipata wiki hii kwa hao kina komedi, akajitazame.

Na huyo Hamad alikuwa haeleweki, yaani ni upupu mtupu.

Bogus.

Kwa hiyo ndugu yangu' kama ulikuwa unategemea majibu, nakupa pole sana. Wala hutopata majibu kutoka Chadema wala CUF.

Nadhani Chadema wangempeleka Zitto angeongea la maana kuliko huyo Professional DJ.
Bora kidogo HR aliongea vizuri.

sasa kama mwenyekiti wa chama alikuwa hajui anachokiongea wafuasi watakidefendi vipi chama mitaani, Mdahalo wa jana umenifanya niwaze kuwa kunatatizo ndani ya chadema, wanashindwa kuoganize mambo yao ili wananchi waelewe nini hasa msimamo wao, mara tunamtambua Rais, ila matokeo hatuyatambui, we mbweha nini tushike nini tuache nini? sasa naanza kuona chanzo cha zittoku tokubali suala la kutoka nje wakati mkwele anahutubia kumbe wenda kulikuwa na mkanganyiko katika kutambua basis ya lile tendo ni nini?
 
Hivi nguruwe anauhusiano na dini ipi? Yaani hii imenichanganya!
 
Aliyekosea sio yeye HR, bali ni wahenga, kwani msemo huo upo kwa miaka kadhaa na wala haijawahi kuwa tatizo, au kwa sababu kausema yeye? muwe waelewa wa lugha ya kiswahili hata kama hamuijui. Nguruwe ananasibishwa na uharibifu wa shamba la mihogo na sio uharamu. Na hii sio katika lugha ya kiswahili tu, bali hata lugha ya kiingereza vipo vitu kama hivi...Poleni kwa kuishi Tanzania na kuwa masikini wa lugha yetu.
 
VoiceofReason,
Thanks very much. I like your creativity. I think this is the way discussion should go. Msingi mkubwa wa Matatizo ya nchi yetu iwe ni umaskini, ufisadi, utawala mbovu, matumizi mabaya ya fedha na Rasilimali za Taifa ni Katiba kama nilivyowahi kueleza mara kadhaa.Msingi wa Chaguzi zetu iwe Uchaguzi Mkuu au wa Serikali za Mitaa ni Katiba Mbovu. Dawa itakapopatikana pale Tatizo Msingi litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi. Hivyo, pendekezo lako ni sahihi kabisa, kila avenue inayoweza kutufikisha huko ni muhimu ikatumika, iwapo wananchi Takriban 5 Million wakisaini petition idadi ya kura za "Rais" ninahakika matokeo yake ni kuleta mtetemeko katika duru ya siasa za nchi, na walioshika rungu, kwa halali au la watalazimika kutekeleza. Hii ndio " Falsafa ya Nguvu ya Umma" . Hata hivyo some has to initiate the process, a courageous son or daughter of this land.Once again, thanks very much for this very creative idea, which is happening in other parts of the world.
 
) Kwa sasa Mishahara ya Wabunge inapangwa na Tume ya Huduma za Bunge ( yaani Parliamentary Service Commmission) ambao wajumbe wake wengi wanatoka CCM. Wapinzani katika Commission ni wachache sana na hata ikipigwa kura watashindwa daima kama ilivyo ndani ya ukumbi. Ni tatizo la kimfumo na ni tatizo la ukiritimba wa Chama kimmoja. Ndio hoja ambayo siku zote tumeiweka kwa Watanzania, ndio maana tumekuwa tukisema " Watanzania wenyewe ndio wanaosababisha kwa sehemu kubwa umaskini wao kwa kuchagua wabunge wa Chama kimmoja". Ukiachilia mbali uchakachuaji uliofanyika, nafurahi kuwa Watanzania wamelitambua hilo na ndio maana idadi ya Wabunge wa Upinzani imeongezeka sana. Pasingelikuwa na Uchakachuaji, nina hakika ukombozi ungelikuwa umefika au ungelikuwa mlangoni. Hivyo isingelikuwa Busara kwa Mbowe kujibu hoja ambayo hana mamlaka nayo na wale hawezi kwa njia yeyote ile " kuibadili:" au hata ku " influence". Msingi huu ukifahamika vizuri, hoja yako ya kwanza inakuwa haina mshiko wowote.
ii) Tume ya Huduma ya Bunge inatokana na Katiba Mbovu na Sheria zake. Hivyo ukifanikiwa Kubadili au kupata Katiba mpya, ndio ufumbuzi pekee wa matatizo yote hayo. Kumbuka, kuwa Tume ya Bunge "inapendekeza" kwa Rais, na ukiwa na Rais makini, atakataa kupitisha mapendekezo ambayo yanaifilisi Taifa. Rais wetu kwa mujibu wa Katiba aikiisha kuipitisha hakuna mahali pengine unaweza kuhoji, au kama utataka kumhoji kuna utaratibu mgumu sana wa kuihoji Serikali mahakamani, kwanza "lazima utoe Notice nadhani ya siku 90, kisha upate kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mara nyingi kibali hicho hakitolewi". Tumekwisha kujaribu njia hizo katika kipindi changu cha miaka 15 Bungeni lakini ilishindikana. Hivyo jibu pekee ni Marekebisho makubwa ya Katiba na kupunguza mamlaka ya Rais (Excessive powers).
iii) Katika hoja yako ya pili kuhusu kuunganisha nguvu za Upinzani, unazungumzia Chadema kuchukua 100M kwa kuunda Serikali Kivuli. Ni kweli Utaratibu wa sasa, tena ambao hauko ndani ya Sheria, wala Kanuni unatenga kila Mwaka Bajeti ya Tshs 100 Millioni kwa "Kiongozi wa Upinzani". Hivyo Ungelifanya utafiti, hoja yako isingelikuwa flawed kama sasa a) Chadema haina haki wala haiwezi kuvuta 100 million kutokana na kuundwa kwa Kambi ya Upinzani kwa vile fedha hizo zimetengwa, kwa kilichoelezwa jana na Mhe. Hamad kama ulimsikiliza vizuri kuwa ni kwa "Kiongozi wa Upinzani" wala siyo kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani. Conclusion yako ni matokeo ya kutokusikiliza vizuri na kutokufanya utafiti. Hamad amekuwa Kiongozi wa Upinzani toka 2005 hadi 2010, alitakiwa kuulizwa hizo fedha alizutumia kwa kazi gani, na Katibu wa Bunge anatakiwa kutoa hadharani matumizi ya fedha hizo ili Watanzania waone zilitumika kwa kazi gani na kwa manufaa ya nani. Kama hazikutumika kwa manufaa ya watanzania wana haki ya kupiga kelele kwani millioni 100 ni fedha nyingi na zingeweza kujenga madarasa kadhaa kupunguza upungufu wa madarasa au zahanati. b) Mimi nilikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani, katika miaka yangu yote niliyokuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani sijawahi kuona Break down ya fedha hizo na matumizi yake. Tulipodai zitumike kwa gharama za ofisi mathalan, kumlipa "mratibu wa Kambi"ambaye kwa taarifa yako "ameajiriwa" na Kambi na mishahara(posho zake zinalipwa kwa kuchangiwa na wabunge wenyewe ambao tulikuwa tunakatwa kutoka kwenye mishahara na posho zetu wakati kuna fedha za Kiongozi wa Upinzani), tuliambiwa kuwa hizo ni za Kiongozi wa Upinzani na labda fungu lingine litafutwe kwa ajili ya Kazi za Kambi. Ungelifanyia utafiti swala hilo usingelitoka na hoja kuwa Chadema wanachukua hizo fedha, kwani Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema hadi jana, haijapokea fedha zozote kutoka Ofisi ya Bunge ( labda Gari rasmi la Kiongozi wa Upinzani, ambalo sina hakika hata kama linahudumiwa na kasma hiyo). Hoja yake inaweza pia kugeuzwa kuwa Hamad hataki kuungana na Chadema kuunda Kambi rasmi kwa vile kama alivyokuwa Dr. Slaa, Naibu Kiongozi wa Kambi ambaye hakuwa anajua hizo fedha zilifanya nini, naye sasa atakuwa Naibu hivyo hatakuwa na fedha. Labda kwa kuunda Kambi "ndogo isiyo Rasmi" naye pia kwa mlango huo huo anaweza kupewa mafao kama ya Kongozi wa Upinzani yaani gari, Ofisi, Nyumba na Fedha 100 Millioni. Lakini tukumbuke tukiendekeza kugawa fedha, Kodi za Watanzania maskini kwa mtindo huu, hatutafika na Taifa litaendelea kuporomoka na kuzama katika lindi la Umaskini.
iv) Mtafiti wa kweli angeliuliza, na Jenifer angeliuliza swali kwenye Mdahalo au hata kwenye JF kuwa " Je Kambi ya Upinzani inayoundwa na Chadema itaendelea kutumia hizo 100 Million kwa matumizi Binafsi ya Kiongozi wa Upinzani au kwa matumizi ya shughuli za Kambi mathalan utafiti na kazi za mawaziri Kivuli, nina hakika angelipata jibu sahihi kuliko kufanya conclusion kwenye "hisia" ambazo nazo kama tulivyoona jana kwenye mdahalo zinaweza kuwa na sababu zake.
Jenifer, naamini nimeweza kutoa mchango wangu kwa manufaa ya wana JF wote ambao hawajui hizi fedha kama zilikuwepo, ziko, na kama ziko zinalenga kufanya kazi gani chini ya uongozi mpya wa Kambi ya Upinzani inayoongozwa na Chadema.


Hapa umenikosha dr na nimeelewa vema, am greatly convinced of your positive responses...AHSANTE SANA
 
Back
Top Bottom