Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,484
- 119,336
Mimi nakataa kwamba hapa duniani kuna uchawi na nimeshatoa changamoto nyingi tu, hapa JF na hata nje ya JF kuwa kama kweli uchawi upo basi yeyote yule mwenye uwezo wa kuniroga ili tu kunithibitishia kuwa kweli upo, na afanye hivyo.
Mpaka sasa hakuna lolote. Watu wameishia kutoa vitisho hewa tu na Ngabu bado nipo nadunda tu.
Nimejaribu kufanya kauchunguzi kangu kasiko rasmi na nimebaini kwamba, kwa Tanzania hii wadada ambao hawaukubali uchawi ni wachache mno na pengine hawapo kabisa.
Hapo namaanisha nini? Namaanisha wale wenye mtazamo sawa na wa kwangu kuwa uchawi pamoja na nguvu au uwezo wake, kiuhalisia haupo bali ni simulizi tu.
Wadada wengi ambao nimewachunguza katika huo utafiti wangu, kama hawaukubali uchawi basi wanafanya hivyo kwa msingi wa imani ya mungu na si vinginevyo kama niukataavyo mimi.
Yaani, wanakubali kuwa uchawi upo lakini wao wamewekeza zaidi nguvu zao katika imani ya mungu.
Sasa jambo linalonitatiza ni uwepo wa wadada ambao wanakataa uwepo wa uchawi na nguvu zake bila kuingiza mambo ya mungu.
Kwa hadhira ya hapa jamvini, mpo nyie wadada?