Mdada asiyeamini/ asiyeukubali uchawi

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,212
113,502
Mimi nakataa kwamba hapa duniani kuna uchawi na nimeshatoa changamoto nyingi tu, hapa JF na hata nje ya JF kuwa kama kweli uchawi upo basi yeyote yule mwenye uwezo wa kuniroga ili tu kunithibitishia kuwa kweli upo, na afanye hivyo.

Mpaka sasa hakuna lolote. Watu wameishia kutoa vitisho hewa tu na Ngabu bado nipo nadunda tu.

Nimejaribu kufanya kauchunguzi kangu kasiko rasmi na nimebaini kwamba, kwa Tanzania hii wadada ambao hawaukubali uchawi ni wachache mno na pengine hawapo kabisa.

Hapo namaanisha nini? Namaanisha wale wenye mtazamo sawa na wa kwangu kuwa uchawi pamoja na nguvu au uwezo wake, kiuhalisia haupo bali ni simulizi tu.

Wadada wengi ambao nimewachunguza katika huo utafiti wangu, kama hawaukubali uchawi basi wanafanya hivyo kwa msingi wa imani ya mungu na si vinginevyo kama niukataavyo mimi.

Yaani, wanakubali kuwa uchawi upo lakini wao wamewekeza zaidi nguvu zao katika imani ya mungu.

Sasa jambo linalonitatiza ni uwepo wa wadada ambao wanakataa uwepo wa uchawi na nguvu zake bila kuingiza mambo ya mungu.

Kwa hadhira ya hapa jamvini, mpo nyie wadada?
 
Hivi nikisema kwa mfano wateja wengi wa hawa ma ustaadh ni wanawake nitakuwa nakosea?

20160611_133605.jpg
20160608_175410.jpg
 
nami pia huwa siuuamini

Kuna wadada wapumbavu kweli aisee.

Yaani unakuta wanaamini huo upuuzi hadi wanakuwa mazuzu.

Eti sijui limbwata au wanapewa sijui nyama gani za ajabu ajabu wawalishe wanaume zao.

Kinyama kitamfanyaje mtu akupende sasa? Nawadharau sana wanawake wa hivyo.

Kuna kimoja eti kilinitisha kuwa nitaendewa kwa waganga na wanawake wa Dar.

Hahahaaa....that's just incredibly stupid, to put it charitably.
 
Nyani Ngabu kama kweli unataka kurogwa ni pm jina lako halisi na la mama yako halafu chagua mwenyewe unataka urogwe vipi uende chooni every one minute,upige kelele hovyo hovyo au urogwe UKIMWI ni pm mkuu
 
Mwenzio gfsonwin alikuja na hiyo hiyo mbinu yako miaka kama mitatu hivi iliyopita na nikampatia vyote alivyoomba lakini hadi leo bado nipo.

Kama kweli uchawi upo wala huna haja ya kuomba majina yangu na ya mama yangu halafu eti nichague mwenyewe uniroge vipi.

Uchawi ni pango la watu wenye akili ndogo.
 
acha kujidanganya wewe! uchawi upo sema tu wewe huamini kama upo ngoja yakutokee ndio utaleta mrejesho humu kwamba uchawi noma
 
Kuna wadada wapumbavu kweli aisee.

Yaani unakuta wanaamini huo upuuzi hadi wanakuwa mazuzu.

Eti sijui limbwata au wanapewa sijui nyama gani za ajabu ajabu wawalishe wanaume zao.

Kinyama kitamfanyaje mtu akupende sasa? Nawadharau sana wanawake wa hivyo.

Kuna kimoja eti kilinitisha kuwa nitaendewa kwa waganga na wanawake wa Dar.

Hahahaaa....that's just incredibly stupid, to put it charitably.
Hiv vitu mkuu vipo amini usiamini lkn ukweli upo pale pale.
Dunia ina mambo mkuu, ww bado hayajakukuta, siku yakikukuta sidhan km utakuja kubisha
 
tembea uone huko sumbawanga radi zinauzwa pale singida shelui kuna bibi alikua anahamishia mvua shambani kwake
 
tembea uone huko sumbawanga radi zinauzwa pale singida shelui kuna bibi alikua anahamishia mvua shambani kwake
 
acha kujidanganya wewe! uchawi upo sema tu wewe huamini kama upo ngoja yakutokee ndio utaleta mrejesho humu kwamba uchawi noma

Hakuna cha uchawi wala ndumba.

Kama upo nitoleeni mfano mimi.

Zaidi ya hapo ni vitisho hewa tu.
 
Hiv vitu mkuu vipo amini usiamini lkn ukweli upo pale pale.
Dunia ina mambo mkuu, ww bado hayajakukuta, siku yakikukuta sidhan km utakuja kubisha

Hakuna...uchawi ni simulizi tu.

Huo uchawi ungekuwepo basi hakuna ambaye angechepuka mjini hapa.
 
me i do no,wajuvi wa mambo yenyewe hebu mpigeni pigo moja balaa ili alete mrejesho huenda na mm nkaamn..
 
Mwenzio gfsonwin alikuja na hiyo hiyo mbinu yako miaka kama mitatu hivi iliyopita na nikampatia vyote alivyoomba lakini hadi leo bado nipo.

Kama kweli uchawi upo wala huna haja ya kuomba majina yangu na ya mama yangu halafu eti nichague mwenyewe uniroge vipi.

Uchawi ni pango la watu wenye akili ndogo.
NN unajua kuniita kwenye uzi kama huu unanitaka nini lakin??
afu kusema wateja wakubwa awa hao wanaovuta wapenzi ni wanawake you are very wrong.
for sure its a two way. there are women who go for the service as well as men.
kuna wanawake wanalia kabisa kisa aina ya ndoa walizoolewa nikimaanisha waliolewa na wanaume ambao waliwavuta hao wanawake kichawi hadi mwanamke kukubali kuolewa nae.
wapo wanawake waliopata waume kwa njia hizo hizo. siku hizi biashara ya kuvuta wapenzi na yenyewe haina mashiko biashara yao kubwa imebaki kuwa kuvuta watu kwenda kwenye ufreemason na kutoa pesa za bahati ama kuwapa hela za majini.
Bila Mungu mjin hapa hukawii kulishwa kinyesi cha mbuzi ukidhan ni korosho za mtwara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom