Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Dr.Josephat Gwajima, leo kanisani kwake mbele ya umati wa waumini akiwaita wanafamilia wake, ametoa maelezo yakinifu juu ya tuhuma zinazomkabili ndg. Paul Makonda na katika clip inayosambaa kwa kasi mitandaoni.

Askofu Gwajima amedai anaoushahidi wa kutosha kua ndg. Makonda alitumia vyeti visivyo vyake.

Katika clip hiyo mchungaji Gwajima amesema ana vyeti vinavyotoa ushahidi kua Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.

Swali: Je, Rais atamwacha Makonda na kulifumbia macho hilo suala?


=======

PAUL MAKONDA:

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.

Acha chuki were Gwajima.Kumbe RC alikaa darasani hata kama umejaribu kuudhihirishia umma kuwa aalitumia vyeti vya MTU mwingine.Madai yako yangepata mashiko kama hakukaa darasan kuisotea elimu yake.

Nikukumbushe pia kuwa mabadiliko ya jina yalifanyika kisheria

Hebu na wewe jitafakari usafi wa utumishi wako.
 
Hivi inawezekanaje mkuu wa mkoa kupata division ZERO? inamaana darasani alikuwa anasoma ujinga? Haya tuwekee vyeti mezani ndug Bashite
 
Kwa haya yanayoendelea kuhusu Bashite na ukimya wa viongozi wastaafu wa nchi hii,ni wazi Nyerere tu ndie alikuwa na uwezo wa kuwakemea warithi wake lakini kwa sasa hakuna tena kiongozi kama yeye.

Ninaamini Nyerere angekuwepo leo hii asingemuone mtu fulani aibu kwa kukalia kimya mambo haya na asingesita kumueleza ukweli tena hadharani kuwa anakosea.

Ni aibu sana!
 
huo unaouongelea wewe ni uchungaji wa mshahara, sio uchungaji wa wito. uchungaji wa wito hauhitaji shule bali wito. angalia mitume wote tangu kitabu cha mwanzo hadi ufunuo kama walienda shule ya Bible. waliitwa na kupakwa mafuta tu kwasababu anayeongoza ni Mungu ndani yao wala sio elimu waliyoipata skuli.
Hao wa zamani walikuwa na mkufunzi MKUU yaani YESU mwenyewe,,

Hata alipowaacha aliwaachia VYETI vya kudumu ambaye ndiye ROHOMTAKATIFU wa Bwana.

Sasa yeye Gwajima nani kamuweka WAKFU wa kuwa Askofu achilia mbali Uchungaji wa kawaida.
Aweke hapa Vyeti vyake vya Taaluma yke,,
 
Hao wa zamani walikuwa na mkufunzi MKUU yaani YESU mwenyewe,,

Hata alipowaacha aliwaachia VYETI vya kudumu ambaye ndiye ROHOMTAKATIFU wa Bwana.

Sasa yeye Gwajima nani kamuweka WAKFU wa kuwa Askofu achilia mbali Uchungaji wa kawaida.
Aweke hapa Vyeti vyake vya Taaluma yke,,
kina petro walisoma wapi, kina paulo (saul) alisoma wapi. ninyi wachungaji wa vyeti ndio maana mnakuwa hadi wachawi kwasababu mnajali cheo siu utume.
 
habari wana jf nmekua nikiwaza huyu gwajima ana muda gani toka afahamu kua RC wetu ana vyeti ambavyo si vyake,na kama nafahamu toka mda mrefu kwanini hakusema kipindi kile cha PAUL MAKONDO kuwa mkuu wa wilaya? Au kwasababu amemhusishwa na uchunguzi wa madaw?
 
habari wana jf nmekua nikiwaza huyu gwajima ana muda gani toka afahamu kua RC wetu ana vyeti ambavyo si vyake,na kama nafahamu toka mda mrefu kwanini hakusema kipindi kile cha PAUL MAKONDO kuwa mkuu wa wilaya? Au kwasababu amemhusishwa na uchunguzi wa madaw?

Umenizidi mkuu

upload_2017-3-21_8-39-14.png
 
Jiongeze mtoa mada. Hivi wewe ulishawahi kujadili kauli za Sizonje kabla hajawa mkuu wa njiii? Unapotenda kosa ndio unatoa mwanya wa watu kukuchunguza usafi wako.
Nikukumbushe tu misemo kama usitukane mamba kabla........, ukitaka kuruka agana na .........., lakini kubwa kuliko usianzishe vita ya mawe wakati unaishi kwenye jumba la udongo.
Nikukumbushe tu kuwa Gwajima ana helicopter anatua mpaka kolomije
 
Back
Top Bottom