Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Makonda hakuwa sahihi kumtaja Gwajima kuwa anahusika na dawa za kulevya wakati hakuwa na ushahidi angalau wa asilimia 90. Kitendo cha Gwajima kutofunguliwa mashitaka, maana yake alimtaja bila ushahidi.

Gwajima hapaswi kuendesha vita yake binafsi na Makonda kupitia Kanisa. Ni kama ambavyo Makonda hakuwa sawa kutumia cheo chake kumpa Gwajima tuhuma nzito za dawa za kulevya.

Tafsiri ni kuwa Makonda alitumia ofisi yake vibaya, naye Gwajima ametumia madhabahu yake vibaya. Kwa msemo wa mtaani, hiyo wanaita “mbwa kala mbwa! Yaani mechi sare. Kwamba ngoma droo.

Wanasheria wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika kesi, hufanya marejeo ya kesi za nyuma zenye mfanano na kesi husika ili kuzipa uzito hoja au hukumu, wenyewe huita legal citation.

Kwa kesi hii, ‘legal citation’ ambayo naitumia ni tukio la miaka nane iliyopita, pale mfanyabiashara Reginald Mengi alipotangaza wafanyabiashara watano kuwa ndiyo mafisadi papa. Aliwataja kuwa ni Rostam Aziz, Yusuf Manji, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subhash Patel.

Rostam alimjibu Mengi kwa kumtaja kuwa ni fisadi nyangumi. Baada ya hapo mzee Mengi alikwenda mahakamani, akituhumu kuchafuliwa jina lake.

Swali likawa, je, kwani wakati yeye anataja mafisadi papa, alidhani Rostam angechekelea na asingeumia? Kila nafsi ina nyama na damu, kinachokuumiza wewe, na mwenzako akitendewa kitamuumiza.

Kama ambavyo Makonda anaumia na hata kutoa machozi kwa sababu ya mjadala wa cheti, ndivyo na Gwajima aliumia sana kutajwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Zaidi Gwajima alilala mahabusu, akapelekwa nyumbani kupekuliwa kisha kupimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Gwajima hakulia ila aliumia.

Kinachotokea kati ya Makonda na Gwajima, ni ile dhana kuwa ukichezewa rafu uwanjani kisha ukarudisha, wewe unakuwa umekosea zaidi. Hata hivyo ukweli usiopingika ni kuwa anayetumia mamlaka ya nchi kumkabili raia isivyofaa, anapaswa kuwa mkosefu zaidi.

Kwa msingi huo, watu wanaomlaumu Gwajima kutumia uwanja wa taasisi yake ya kidini kumkabili Makonda, wanatakiwa kuwa wakali zaidi kumsema Makonda kutumia ofisi ya umma kuzushia watu kashfa na kuwachonganisha na jamii

By chibudeeee
bfa8c004895a2a4b054c55f67c46e31b.jpg
kwa gwajima wacha ajivue uchungaji kwa muda ili amalize hii kadhia ya DAUDI.. maana bashite alizidi kupindukia.. wacheni gwajima afanye yake ili ajiweke swafi mbele ya jamii
 
Babu yangu alikuwa mwinjilisti watu wakazidi kumwonea kutokana na huko kuwa na YESU. Mzee akasema sasa yatosha, ikawa mtu akimkorofisha anamwambia nitamtundika YESU wangu mtini halafu nikushughulikie kwanza nikishamalizana na wewe naenda kumchukua tena! Hicho ndo Gwajima alikifanya baada ya manyanyaso ya mheshimiwa sana RC Daudi Alubati Bashite. Hukumu yako Chibudee ni ya haki kabisa wala haina kona kona! Makonda kulialia wala haimsaidii alete vyeti hapa! Hivi naye huwa anakunywa MAJI mengi kama Ray?
 
safi sana
 
kwa gwajima wacha ajivue uchungaji kwa muda ili amalize hii kadhia ya DAUDI.. maana bashite alizidi kupindukia.. wacheni gwajima afanye yake ili ajiweke swafi mbele ya jamii
Hapa kaisari anapewa vilivyo vyake, hakuna kosa
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Anayedaiwa kuibiwa vyeti hajalalamika popote na wanaolalamika siyo wanaodaiwa kuibiwa. Kwa mtu mwenye akili timamu atabaini kuwa hapa ni porojo ndizo zinachezwa na lengo ni kusogeza siku ili 2020 ifike kwa vile CHADEMA hawana hoja za kujenga kwa wananchi.

Ndugu zangu, CHADEMA siku zote hubwabwaja na wakati mwingine hawajui lolote juu ya hicho wanachosema. Walituambia hapa kuwa PAUL CHRISTIAN MUYENGE ni mfanyakazi wa Radio FM Tabora na alipata Division One form four. Wakatuambia kuwa alishindwa kuendelea na masomo kwa vile alikosa ada ya kugharamia masomo ya kidato cha tano na sita. Hawajaeleza iweje amudu kugharamia masomo hadi kidato cha Nne akashindwa kugharamia miaka miwili tu. Hapa kuna hoja ya kujibu. Hawajatuambia kuwa wakati anaajiriwa Radio FM Tabora, aliwasilisha vyeti gani na wakati anaajiriwa, alikuwa na kiwango gani cha elimu. Kama alikuwa na elimu inayozidi form four, hawajatuambia alijiendelezaje ilhali vyeti vyake vinatumiwa na MAKONDA.

Akaja yule mchungaji mihogo na story kuwa PAUL MAKONDA jina lake halisi ni DAUDI ALBERT BASHITE. Bashite ndio imekuwa kick ya kuwatoa kisiasa. Akatuambia kuwa Makonda aliiba vyeti vya Division Three ili akasome chuo cha Uvuvi. Hapa Division One ya akina Mange Kimambi imeota mbawa.

Ili kuhitimisha mjadala huu, kwa vile PAUL CHRISTIAN MUYENGE yupo, CHADEMA mshinikizeni akafungue kesi ya madai na jinai mahakamani. Huwezi kuibiwa vyeti na wewe ukatulia tu then ukatumia vyeti hivyo hivyo kujiendeleza kitaaluma mpaka ukapata taaluma ya Habari. CHADEMA mna mawakili wasomi ambao wanaweza kumsaidia MUYENGE kupata haki yake. Kama mmemsaidia WEMA SEPETU anayekabiliwa na matumizi ya moshi, mbona huyu Muyenge mnamtenga?
 
Makonda hakuwa sahihi kumtaja Gwajima kuwa anahusika na dawa za kulevya wakati hakuwa na ushahidi angalau wa asilimia 90. Kitendo cha Gwajima kutofunguliwa mashitaka, maana yake alimtaja bila ushahidi.

Gwajima hapaswi kuendesha vita yake binafsi na Makonda kupitia Kanisa. Ni kama ambavyo Makonda hakuwa sawa kutumia cheo chake kumpa Gwajima tuhuma nzito za dawa za kulevya.

Tafsiri ni kuwa Makonda alitumia ofisi yake vibaya, naye Gwajima ametumia madhabahu yake vibaya. Kwa msemo wa mtaani, hiyo wanaita “mbwa kala mbwa! Yaani mechi sare. Kwamba ngoma droo.

Wanasheria wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika kesi, hufanya marejeo ya kesi za nyuma zenye mfanano na kesi husika ili kuzipa uzito hoja au hukumu, wenyewe huita legal citation.

Kwa kesi hii, ‘legal citation’ ambayo naitumia ni tukio la miaka nane iliyopita, pale mfanyabiashara Reginald Mengi alipotangaza wafanyabiashara watano kuwa ndiyo mafisadi papa. Aliwataja kuwa ni Rostam Aziz, Yusuf Manji, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subhash Patel.

Rostam alimjibu Mengi kwa kumtaja kuwa ni fisadi nyangumi. Baada ya hapo mzee Mengi alikwenda mahakamani, akituhumu kuchafuliwa jina lake.

Swali likawa, je, kwani wakati yeye anataja mafisadi papa, alidhani Rostam angechekelea na asingeumia? Kila nafsi ina nyama na damu, kinachokuumiza wewe, na mwenzako akitendewa kitamuumiza.

Kama ambavyo Makonda anaumia na hata kutoa machozi kwa sababu ya mjadala wa cheti, ndivyo na Gwajima aliumia sana kutajwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Zaidi Gwajima alilala mahabusu, akapelekwa nyumbani kupekuliwa kisha kupimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Gwajima hakulia ila aliumia.

Kinachotokea kati ya Makonda na Gwajima, ni ile dhana kuwa ukichezewa rafu uwanjani kisha ukarudisha, wewe unakuwa umekosea zaidi. Hata hivyo ukweli usiopingika ni kuwa anayetumia mamlaka ya nchi kumkabili raia isivyofaa, anapaswa kuwa mkosefu zaidi.

Kwa msingi huo, watu wanaomlaumu Gwajima kutumia uwanja wa taasisi yake ya kidini kumkabili Makonda, wanatakiwa kuwa wakali zaidi kumsema Makonda kutumia ofisi ya umma kuzushia watu kashfa na kuwachonganisha na jamii

By chibudeeee
bfa8c004895a2a4b054c55f67c46e31b.jpg
PAUL MAKONDA ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa mkoa, vilevile majukumu yake ni kutekeleza sheria za nchi, ikiwemo sheria namba 5 ya 2015 ya kupambana na madawa ya kulevya, katika mkoa wake na kusimamia shughuli za serikali. Paul Makonda ameteuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Kifungu 61 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Sasa kama GWAJIMA anapambana na PAUL MAKONDA, ajue wazi kuwa anapambana na Serikali, sheria za nchi, katiba ya nchi na Rais wa nchi ambaye ni John Pombe Magufuli. Hivyo, Gwajima anapaswa kuelewa hili kabla ya kuendeleza ubabe wake ambao kwa asilimia 100% atashindwa na kujikuta mahala pabaya.
Laiti mimi ndiyo ningekuwa Rais wa nchi hii, Gwajima angepata somo. Paul makonda yuko sahihi katika vita hii. Labda tu watu wanaompenda Gwajima wampe ushauri ili aache kupambana na serikali. Atii sheria za nchi. Vinginevyo, ataonekana na ni mchungaji mbabaishaji tu mbele ya jamii. Kamaanaweza kudhibitisha jambo kwa kunukuu vifungu vya Biblia, anashindwaje kudhibitisha kwa kuonyesha hadharani hivyo vyeti anavyodai kuwa navyo?.
 
Ingekuwa vema anayetuhumiwa akatoaa cheti tu mchezo uishee, sinema ya kihindi ingeishiaa hapo. Swali je atatoa??
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Anayedaiwa kuibiwa vyeti hajalalamika popote na wanaolalamika siyo wanaodaiwa kuibiwa. Kwa mtu mwenye akili timamu atabaini kuwa hapa ni porojo ndizo zinachezwa na lengo ni kusogeza siku ili 2020 ifike kwa vile CHADEMA hawana hoja za kujenga kwa wananchi.

Ndugu zangu, CHADEMA siku zote hubwabwaja na wakati mwingine hawajui lolote juu ya hicho wanachosema. Walituambia hapa kuwa PAUL CHRISTIAN MUYENGE ni mfanyakazi wa Radio FM Tabora na alipata Division One form four. Wakatuambia kuwa alishindwa kuendelea na masomo kwa vile alikosa ada ya kugharamia masomo ya kidato cha tano na sita. Hawajaeleza iweje amudu kugharamia masomo hadi kidato cha Nne akashindwa kugharamia miaka miwili tu. Hapa kuna hoja ya kujibu. Hawajatuambia kuwa wakati anaajiriwa Radio FM Tabora, aliwasilisha vyeti gani na wakati anaajiriwa, alikuwa na kiwango gani cha elimu. Kama alikuwa na elimu inayozidi form four, hawajatuambia alijiendelezaje ilhali vyeti vyake vinatumiwa na MAKONDA.

Akaja yule mchungaji mihogo na story kuwa PAUL MAKONDA jina lake halisi ni DAUDI ALBERT BASHITE. Bashite ndio imekuwa kick ya kuwatoa kisiasa. Akatuambia kuwa Makonda aliiba vyeti vya Division Three ili akasome chuo cha Uvuvi. Hapa Division One ya akina Mange Kimambi imeota mbawa.

Ili kuhitimisha mjadala huu, kwa vile PAUL CHRISTIAN MUYENGE yupo, CHADEMA mshinikizeni akafungue kesi ya madai na jinai mahakamani. Huwezi kuibiwa vyeti na wewe ukatulia tu then ukatumia vyeti hivyo hivyo kujiendeleza kitaaluma mpaka ukapata taaluma ya Habari. CHADEMA mna mawakili wasomi ambao wanaweza kumsaidia MUYENGE kupata haki yake. Kama mmemsaidia WEMA SEPETU anayekabiliwa na matumizi ya moshi, mbona huyu Muyenge mnamtenga?

Bashite weka vyeti mezani hizi blah blah peleka Lumumba.
 
PAUL MAKONDA ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa mkoa, vilevile majukumu yake ni kutekeleza sheria za nchi, ikiwemo sheria namba 5 ya 2015 ya kupambana na madawa ya kulevya, katika mkoa wake na kusimamia shughuli za serikali. Paul Makonda ameteuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Kifungu 61 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Sasa kama GWAJIMA anapambana na PAUL MAKONDA, ajue wazi kuwa anapambana na Serikali, sheria za nchi, katiba ya nchi na Rais wa nchi ambaye ni John Pombe Magufuli. Hivyo, Gwajima anapaswa kuelewa hili kabla ya kuendeleza ubabe wake ambao kwa asilimia 100% atashindwa na kujikuta mahala pabaya.
Laiti mimi ndiyo ningekuwa Rais wa nchi hii, Gwajima angepata somo. Paul makonda yuko sahihi katika vita hii. Labda tu watu wanaompenda Gwajima wampe ushauri ili aache kupambana na serikali. Atii sheria za nchi. Vinginevyo, ataonekana na ni mchungaji mbabaishaji tu mbele ya jamii. Kamaanaweza kudhibitisha jambo kwa kunukuu vifungu vya Biblia, anashindwaje kudhibitisha kwa kuonyesha hadharani hivyo vyeti anavyodai kuwa navyo?.
Aoneshe kwani vyake au vya bashite??

Pia Umejaribu kumtetea Bashite lakini bado uteteze auna Tija

Makonda kama anajiamini Na anauwakika na elimu yake kwann Asiweke uwalali wa elimu yake

Kwaiyo kisa makonda kateuliwa. Na raisi ndio hatuna mamlaka ya kumjaji??

Au kuteuliwa na raisi nisababu ya kuuongopea umma??

Ninavyo mjua makonda nimpenda sifa sanaa angekua kweli Anaelimu yahaja lazima angelizima iliswala la vyeti kwambwembwe zoote cloud's lakini huwezo huo hanaa

Hatukotayari kuongozwa nakiongizi asie muadilifu
 
Baada ya thread ya kifo cha Mh. Regia Mtema (Mb); thread ya/za "Kashfa ya Bashite" ndio inayoshika rekodi ya pili kwa michango mingi tangu kuanzishwa kwa JF.
 
Back
Top Bottom