Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

PAUL MAKONDA ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa mkoa, vilevile majukumu yake ni kutekeleza sheria za nchi, ikiwemo sheria namba 5 ya 2015 ya kupambana na madawa ya kulevya, katika mkoa wake na kusimamia shughuli za serikali. Paul Makonda ameteuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Kifungu 61 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Sasa kama GWAJIMA anapambana na PAUL MAKONDA, ajue wazi kuwa anapambana na Serikali, sheria za nchi, katiba ya nchi na Rais wa nchi ambaye ni John Pombe Magufuli.

Tatizo ni vyeti baaaasi
 
Makonda hakuwa sahihi kumtaja Gwajima kuwa anahusika na dawa za kulevya wakati hakuwa na ushahidi angalau wa asilimia 90. Kitendo cha Gwajima kutofunguliwa mashitaka, maana yake alimtaja bila ushahidi.

Gwajima hapaswi kuendesha vita yake binafsi na Makonda kupitia Kanisa. Ni kama ambavyo Makonda hakuwa sawa kutumia cheo chake kumpa Gwajima tuhuma nzito za dawa za kulevya.

Tafsiri ni kuwa Makonda alitumia ofisi yake vibaya, naye Gwajima ametumia madhabahu yake vibaya. Kwa msemo wa mtaani, hiyo wanaita “mbwa kala mbwa! Yaani mechi sare. Kwamba ngoma droo.

Wanasheria wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika kesi, hufanya marejeo ya kesi za nyuma zenye mfanano na kesi husika ili kuzipa uzito hoja au hukumu, wenyewe huita legal citation.

Kwa kesi hii, ‘legal citation’ ambayo naitumia ni tukio la miaka nane iliyopita, pale mfanyabiashara Reginald Mengi alipotangaza wafanyabiashara watano kuwa ndiyo mafisadi papa. Aliwataja kuwa ni Rostam Aziz, Yusuf Manji, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subhash Patel.

Rostam alimjibu Mengi kwa kumtaja kuwa ni fisadi nyangumi. Baada ya hapo mzee Mengi alikwenda mahakamani, akituhumu kuchafuliwa jina lake.

Swali likawa, je, kwani wakati yeye anataja mafisadi papa, alidhani Rostam angechekelea na asingeumia? Kila nafsi ina nyama na damu, kinachokuumiza wewe, na mwenzako akitendewa kitamuumiza.

Kama ambavyo Makonda anaumia na hata kutoa machozi kwa sababu ya mjadala wa cheti, ndivyo na Gwajima aliumia sana kutajwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Zaidi Gwajima alilala mahabusu, akapelekwa nyumbani kupekuliwa kisha kupimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Gwajima hakulia ila aliumia.

Kinachotokea kati ya Makonda na Gwajima, ni ile dhana kuwa ukichezewa rafu uwanjani kisha ukarudisha, wewe unakuwa umekosea zaidi. Hata hivyo ukweli usiopingika ni kuwa anayetumia mamlaka ya nchi kumkabili raia isivyofaa, anapaswa kuwa mkosefu zaidi.

Kwa msingi huo, watu wanaomlaumu Gwajima kutumia uwanja wa taasisi yake ya kidini kumkabili Makonda, wanatakiwa kuwa wakali zaidi kumsema Makonda kutumia ofisi ya umma kuzushia watu kashfa na kuwachonganisha na jamii

By chibudeeee
bfa8c004895a2a4b054c55f67c46e31b.jpg
Sema precedent badala ya citation.
 
Chibudee

Kama jina lake lilitajwa polisi kuripotiwa ulitaka amuache mseme mengine?

Na nani alikuambia alitoa chozi sababu ya Pastor?

Chozi lile lilikuwa la kushukiwa na roho mtakatifu, chozi la kumshinda shetani. Na jua hajaumizwa na mtu yoyote hata hao mapapa wengine wanaowavuta kufata mkumbo wa udanganyifu juu ya Mh. Makonda.

Na wewe kukaa na kumfikiria kila siku ni kuonyesha kuwa unamkubali sana na unajua yeye ni Kiongozi jembe..hata ukatae si usingemwandika.

Unaonyesha wivu juu ya Mh. Makonda na utaendelea kuumia. Mh. JPM anajua hana alichokosa, wewe ni nani kusema amekosa hata cha kutudanganya unacho kama proof hauna.

Una lako binafsi tamaa labda ya cheo chake, uvivu, wivu haswa juu.

Skku nyingine acha kumuandika kutafuta kiki humu, hauna chochote? Basi jenga njia yako nawe uwe bora na jembe kama yeye.

Kiongozi jembe

Makonda oyeeeeeee
 
acha blablaaa TUNA
Naona mmeanza kugeukana. Wenzako wanasema Makonda kaiba vyeti, wewe unasema kanunua! Lazima mvurugane mwaka huu
ACHA BLABLAAA.... TUNATAKA VYETI VYA DAUDI HAPA!!
 
Ukweli upi? Si aweke vyeti hadharani aache maneno? Then na yeye aweke vyeti vyake vya uchungaji sheinzi type, atuambie alisomea wapi uchungaji
swala hapa lipo hivi

huyu bwana daudi kutoka kolomije ni mtumishi wa uma ambapo mtukufu raisi alimtuma akatafute majina yote ya watumishi wenye vyeti feki ...
sasa yeye binafsi huyu rc anatumia cheti feki alipata wapi nguvu za kumdanganya raisi kuwa yeye ni makonda wakati kumbe yeye ni daudi?
je hakuna majina mengine hewa huyu rc hajayapeleka kwa raisi achilia mbali la kwake ?
kwanini unamkingia kifua ilhali hata hao watumishi 19 elf pia wanamahitaji muhimu ya kibinadamu kama makonda?

kwanini makonda asifutwe kazi na kupandishwa kizimbani?
dunia nzima hii tunaona hata S.A juzijuzi kuna mwanasiasa mmoja kajiuzulu kwa sababu ana phd feki...

lengo la raisi lilikuwa ni nini au mpango wa kuondoa watumishi wachache na kubakisha wengine anaowataka anawaacha kwa matakwa yake?
kwanini haki isitendeke je unaona kuwa makonda peke yake ndo mwenye uwezo wa kuiongoza dar?

😱KWANINI KAMA ANACHETI HAKWENDA KULIPUKA CLAUDS KAMA ALIVYOTANGAZA MAJINA YA KINA MANJI TUNDA PHILEMON ?

UTASIKIA WAUZA
NGADA AKA MI NAUZA UBUYU NA KARANGA MBICHI HUKU, MSISINGIZIE WAUZA NGADA
HAWA WOTE WANA MAKOSA SI MUUZA NGADA WALA MWENYE CHETI FEKI ILI TWENDE SAWA NA YEYE ALETE CHETI ILI IWE KAMA WENZIWE WALIVOPIMWA MKOJO NA DAMU NA KUPEKULIWA VINGINEVYO APOTELEE HUKO KAMA DAUDI BALALI KUOKOA MABOSI ZAKE tumechoshwa na figisu za kubebana za kiushkaji
 
swala hapa lipo hivi

huyu bwana daudi kutoka kolomije ni mtumishi wa uma ambapo mtukufu raisi alimtuma akatafute majina yote ya watumishi wenye vyeti feki ...
sasa yeye binafsi huyu rc anatumia cheti feki alipata wapi nguvu za kumdanganya raisi kuwa yeye ni makonda wakati kumbe yeye ni daudi?
je hakuna majina mengine hewa huyu rc hajayapeleka kwa raisi achilia mbali la kwake ?
kwanini unamkingia kifua ilhali hata hao watumishi 19 elf pia wanamahitaji muhimu ya kibinadamu kama makonda?

kwanini makonda asifutwe kazi na kupandishwa kizimbani?
dunia nzima hii tunaona hata S.A juzijuzi kuna mwanasiasa mmoja kajiuzulu kwa sababu ana phd feki...

lengo la raisi lilikuwa ni nini au mpango wa kuondoa watumishi wachache na kubakisha wengine anaowataka anawaacha kwa matakwa yake?
kwanini haki isitendeke je unaona kuwa makonda peke yake ndo mwenye uwezo wa kuiongoza dar?

😱
Ushahidi ukipatikana sheria itachukua mkondo wake kikubwa pelekeni ushahidi necta au kwenye vyombo husika. Lissu kibatala prof safari jenerali ulimwengu mko wapi?
 
Ushahidi ukipatikana sheria itachukua mkondo wake kikubwa pelekeni ushahidi necta au kwenye vyombo husika. Lissu kibatala prof safari jenerali ulimwengu mko wapi?
yeye ndo shahidi wa kwanza wa hii ishu wacha kugeuza geuza maneno
 
Back
Top Bottom