Kibri kipi bwana ukweli chuki tu ukweli usemwe Kimaro Ndo habari ya mjini tukubali tukatae Mimi ujue sikosagi vipindi vyake nikipata nafasi anatia faraja yule anafundisha nadhani wameogopa anawaoutshine Sanaa viongozi
Kuhusu picha ni vitu vidogo tafsiri zao Ndo zao yeye ukute hamaanishi wanavomaanisha
Ni wivu tu hakuna lingine wanadamu wanaangalia kitu kidogo sana Ndo wanakibeba kuliko mema yake

Si wangesubiri amalize semina kama wao Wana hofu na Mungu kweli!mtu amejipanga halafu mnamkatisha palipo na riziki hapakosi fitna
KKKT wamefeli Kwa hili
Huko IG ni kawaida yake kupost mafundisho mara kwa mara.

Hata mimi huwa namfuatilia Bina,
Anaupiga mwingi mno.

Mungu kumuinua imekuwa nongwa.
 
Hayo mambo ya kusimuliana story za wanafunzi wa Yesu sijui walifanya hivi mara vile kila ibada yanaboa. Mtu lisaa lizima anasimulia habari za waefeso sijui wafarisayo huo ujinga nani anataka.
Eti kufuata Calendar
Shetani anapanga na kupangua mbinu kila siku, nyie mmekaa mmeshikilia Calendar.

Maombi ya asubuhi na jioni,na semina
Ndivyo vinavyowafanya waseme amekiuka taratibu.
Hivi kuimba,kuomba na kujifunza neno ni dhambi??
KKKT wana moto wao special aisee.
 
Eti kufuata Calendar
Shetani anapanga na kupangua mbinu kila siku, nyie mmekaa mmeshikilia Calendar.

Maombi ya asubuhi na jioni,na semina
Ndivyo vinavyowafanya waseme amekiuka taratibu.
Hivi kuimba,kuomba na kujifunza neno ni dhambi??
KKKT wana moto wao special aisee.
Jamaa ana wivu wa kike tu,,, na siku zote wivu huzaa dhambi ya fitina. Sasa aendeleze yeye hio ibada ya asubuhi ili sadaka ale yeye. 🤣🤣🤣
 
Huko IG ni kawaida yake kupost mafundisho mara kwa mara.

Hata mimi huwa namfuatilia Bina,
Anaupiga mwingi mno.

Mungu kumuinua imekuwa nongwa.
Kwanini msimuombe huyo mungu amuinue tena matokeo yake mnaandamana hapo kijitonyama.


Ndio maana hizi Dini huwa naziona michosho Tu.


Kama mnaamini Kati mungu muweza WA yote kwanini msimuombe awezeshe hili la kimaro arudishwe ? Mmebaki mnapiga kelele kama vichaa. Mnaenda kanisani kusali Kwa kumuangalia MTU na sio Injili. This is nonsense ndio maana makanisa mengi waumini wamekuwa kama misukule.


Kama kimaro kaonewa fanyeni maombi kumuomba huyo mungu awaadhibu hao viongozi waliomtoa na huyo mungu anrudishe hapo kijitonyama forcefully
 
shida inakuja pale, ameshaitwa sana na vikao vya maboss wake kurekebisha baadhi ya mienendo yake, yeye amekaidi mbele zao kwamba hawezi kupangiwa (kwa fununu za ndani), anajiona yeye ni maarufu sana pale kijitonyama kiasi kwamba hawana uwezo kumtoa kwasababu ameshajenga mizizi ya kutosha na waumini watamtetea, ndio maana amenyamaza kimyaaa hataki kuwanyamazisha hao waumini wake. dawa yake Malasusa anatakiwa aidha afunge kanisa kwa muda kupisha upepo kupita, halafu awaambie tu waumini kwamba anayetaka kuja kusali aje, asiyetaka byebye. kwasababu kanisa lile sio la mtu, ni la kkkt, hata kama wanajiona wamechanga pesa san akujenga, haimaanishi kwamba wanalimiliki, na walioko mle haimaanishi kwamba watakaa mle milele wanaweza kuhama wapendavyo, hivyo anayetaka aendelee kusali, asiyetaka amfuate kimaro.

ila kosa kubwa wataweka precedent mbaya ni kuonekana wameshindwa mbele ya kimaro kwa kumrudisha, kwasababu atatokea tena mchungaji sehemu nyingine atafuata tabia anazofanya kimaro za kujiona maarufu na hawezi kuhamishwa pale (wakati waanzilishi wa kanisa la pale walishahamaga hata yeye alitokea kariakoo kkkt, alilikuta tu pale). kila mchungaji atakuwa anafanya tu hivyo na kubishana na wakubwa zake akijua waumini watamtetea. ikiwezekana hata kumfukuza wafukuze tu.
 
Kwanini msimuombe huyo mungu amuinue tena matokeo yake mnaandamana hapo kijitonyama.


Ndio maana hizi Dini huwa naziona michosho Tu.


Kama mnaamini Kati mungu muweza WA yote kwanini msimuombe awezeshe hili la kimaro arudishwe ? Mmebaki mnapiga kelele kama vichaa. Mnaenda kanisani kusali Kwa kumuangalia MTU na sio Injili. This is nonsense ndio maana makanisa mengi waumini wamekuwa kama misukule.


Kama kimaro kaonewa fanyeni maombi kumuomba huyo mungu awaadhibu hao viongozi waliomtoa na huyo mungu anrudishe hapo kijitonyama forcefully
Kimaro alishainuliwa na Mungu huyo..
Hakuna atakayemshusha.
Mungu ana sifa ya kujipambania mwenyewe .

Peleka huo ushauri kwa kijitonyama.
Mimi si mlutheri na wala sipo kijitonyama.
 
Binafsi naona kama Kiburi kimemzamisha akiwa kati kati ya jahazi la utumishi. Alitumia madhabahu ya Mungu kujijenga yeye binasfi na sio MWILI WA KRISTO. Ndio maana yeye akawa maarufu kuliko utakatifu wa waumini wake. kumbuka kipimo cha kazi ya mwaadamu aliyeitwa na Mungu ni matunda aliyoweza kuzalisha.
Umemaliza.

Na ''kiburi cha Uzima'' ndicho kilichozamisha Watumishi wengi wakubwa ulimwenguni tangu enzi na enzi tangu misingi ya kanisa

Ila Wakristo wa leo hawapendi ''UKWELI'' wanakuambia wanapenda ''Vibe''
 
Eti kufuata Calendar
Shetani anapanga na kupangua mbinu kila siku, nyie mmekaa mmeshikilia Calendar.

Maombi ya asubuhi na jioni,na semina
Ndivyo vinavyowafanya waseme amekiuka taratibu.
Hivi kuimba,kuomba na kujifunza neno ni dhambi??
KKKT wana moto wao special aisee.
Uwepo WA huyo Shetani ni dalili huyo anaeitwa mungu Hayupo na kama yupo Hana hizo nguvu nyie mataahila mnazoaminisha watu Yuko nazo.

Kama mungu muweza WA yote anaejua kesho yetu anashindwaje kujua mipango ya shetani ya kesho ili aizuie. Kama Shetani kila siku anapanga mipango yake huyo mungu anaejua kesho yetu anafanya nini sasa.


Kuweni na akili nyie mataahira huu upuuzi unajichimbia huku Africa maana kuna nchi huu utapeli umeanza kushtukiwa
 
Mchaga sijawahi kumuona na sidhani kama itakuja kutokea anytime soon. Hao wengine wote huenda ikaja kutokea maana ni makabila madogo madogo sana. Nafikiri makabila makubwa ndio huwa hayapewi kipaumbele sana.
Wachaga si kabila kubwa kufika hata nusu ya Wasukuma. Ambao wametoa Rais. Wanyakyusa ni Kabila kubwa lenye Jiji nchini halifikii Wasukuma.

Nlitaka uweze kufikiria kwa upana zaidi nje ya box ujue kitu flani kutotokea haimaanishi hakitotokea. Lakini pia ufahamu kuwa safari bado. So far katika Tanzania yenye Makabila zaidi ya 100 waliotawala hawazidi makabila 10. Hali kadhalika katika madhehebu yote hayo inawezekana yasizidi madhehebu ma 3. Katika Iinsia yenye watu wengi ndo imetoa Rais mara moja. Katika jamii yenye watu wachache zaidi imetoa Rais mara Mbili.
 
Kimaro alishainuliwa na Mungu huyo..
Hakuna atakayemshusha.
Mungu ana sifa ya kujipambania mwenyewe .

Peleka huo ushauri kwa kijitonyama.
Mimi si mlutheri na wala sipo kijitonyama.
Sasa kama ameinuliwa na mungu na hakuna WA kumshusha kwanini watu wanabeba mabango arudishwe. Si wasubiri mungu atamrudisha ??!!!! Yani hizi Imani zingine ni upuuzi Sana.


Jinga weyeeeee
 
Jamaa ana wivu wa kike tu,,, na siku zote wivu huzaa dhambi ya fitina. Sasa aendeleze yeye hio ibada ya asubuhi ili sadaka ale yeye. 🤣🤣🤣
as long as upo kkkt kama mchungaji unatakiwa kufuata taratibu za huko, au la ondoka. huwezi kuwa kijitonyama ukalifanya kama lile kanisa ni independent of others wakati hata pale wee umehamishiwa tu kama mfanyakazi.
 
Ndio maana kuna options.

Mkuu ni vigumu SANA kubadilisha Mfumo wa Mamlaka, kama huamini Muulize hata MARTIN LUTHER mwenyewe aliyekuwa Padri na Mwanzilishi wa Lutheran na vita alivyopitia

Au Waulize CHADEMA

''Join them na kutii or Leave them''

That's All.
Mkuu umesema jambo sahihi wengi wanalolipita kama hawalijui ilhali wanapaswa kulijua. Tumia njia sahihi kubadili mfumo, ukishindwa ungana na mfumo na ukishindwa zaidi achana nao. Ukilazimisha sana ukubali purukushani za uasi.
 
Atoke akaanzishe kanisa lake mwenyewe, Makanisa nayo yana likizo, yaani mchungaji unakuwa umeajiriwa?kwani ni kampuni hiyo?uchungaji ni wito sio ajira,mtafanya watu wa act kua wachungaji ili waajiriwe nyie,jua ni kali sana mtaani 😂😂

ndio maana nilienda zangu mashahidi wa jehova
Yaelekea wewe hujui mchungaji/padre/Askofu nae ni mtu anahitaji kupumzika au unadhani nao wanafanya kazi ndogo? Ndio huenda likizo
 
Kimaro alishainuliwa na Mungu huyo..
Hakuna atakayemshusha.
Mungu ana sifa ya kujipambania mwenyewe .

Peleka huo ushauri kwa kijitonyama.
Mimi si mlutheri na wala sipo kijitonyama.
mbona sasa hakuna huwa anahubiri, ni motivational speeches tu ambazo hazisaidii na anatafuta to popularity na kupiganiwa na watu. kwanza akaokoke ndio mengine yafuate.
 
Back
Top Bottom