Me and me
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 345
- 631
Watu mnapenda kujisahaulisha wakati wengi wenu mmetokea familia za Mama Golikipa na maisha yalikuwa yanaenda na mkalelewa hadi leo mmekuwa hivyo mnajifanya kama vile ni jambo ambalo haliwezekani.Kwahy mdada anatakiwa akae nyumbani awe anasubiria mshahara wa mume? Ikiwa alikuwa ashatafuta nafasi na akapata? Aiache kwasababu gani? Na huyo kaka umeskia anaenda kusoma nje ya nchi, ikitokea akapata mchumba mwingine huko yy huyu wa huku atabakije?
Anyway Mimi sijasema Mwanamke huyo akae nyumbani ila nimekuonesha tuu kuwa maisha ya Mama anabaki nyumbani kusimamia nyumba na malezi sio tuu yanawezekana bali ndio asili ya Familia zetu nyingi huko nyuma.
Hapa tunazungumza kuhusu hiyo kazi yenyewe ambayo hata mtoa mada ndio ametaka ushauri kwayo.
Unadhani kama ingekuwa ni Post ya TRA mtoa mada angetaka ushauri??
Kwaiyo nimemshauri kuwa kama ambavyo hajakusikiliza now kuhusu hilo la upolisi basi hatokusikiliza Chochote kuhusu career yake au kuhusu Ajira yake kwani hivyo kwake ni vya Muhimu kuliko Hata Ndoa yenyewe.
Sasa Mwanamke kuwa na msimamo huu ni Vizuri kama hajaolewa ila akiwa ameolewa kuna shida itapatika huko Mbeleni kwa sababu ndoa nayo ni taasisi inayohitaji kusimamiwa kuheshimiwa na kupewa kipaumbele jambo ambalo wanawake wakileo hawalijui au hawalitaki tena.
Wao kazi zao ni muhimu kuliko Chochote hata kuliko watoto wake mwenyewe.
Na ndio utaona watoto wa siku hizi wanalelewa kama mayatima ilihali baba na Mama wote wapo hai.