Mchumba wa Dk. Slaa aibua tuhuma nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchumba wa Dk. Slaa aibua tuhuma nzito

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Informer, Sep 22, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  • Adai kuna mpango wa kumuua mumewe kwa sumu, uchawi

  MWANDISHI WETU | Kulikoni | Sep 21, 2012

  [​IMG]

  MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi, ametoa madai mazito kwa vyombo vya dola akidai kuwapo kwa mpango wa kumdhuru mumewe.

  Josephine amekataa kuingia undani wa madai hayo, pamoja na kukiri kuyaweka katika mtandao kupitia ukurasa wake wa Facebook, kwa maelezo kuwa yuko nje ya nchi kwa sasa.

  Madai hayo yanataja baadhi ya watu wazito ndani ya serikali, ambao wanadaiwa kuwa katika mpango huo, lakini baadhi ya wanaotajwa kutokuwapo kiunganishi na tuhuma husika.

  Katika madai yake, mama huyo machachari, ameandika kwamba kumekuwa na vikao vya watu ndani ya serikali vyenye lengo la kutaka kummaliza Dk. Slaa, kwa njia yoyote ile.

  “Wanaamini kwamba Slaa ndiye mzizi katika Chadema na anaweza kuiangusha CCM 2015. wameona mazingira ya kuchakachua 2015 ni magumu sana,” anaeleza.

  Anaendelea kwa kudai kwamba njia pekee ambayo imebakia ni kuwaondoa wagombea ambao ni tishio na wenye ushawishi wa kuhamishia wanasiasa wengine walio CCM kwenda Chadema.

  Katika madai yake hayo, Josephine amewataja watu ambao wamekuwa wakitajwa mara kwa mara wakihusishwa na matukio ya utesaji kukiwa na jina moja jipya. Majina tunayahifadhi kwa sasa.

  Kama hadithi ama sinema, madai hayo yanawataja watu mbalimbali walioathiriwa na matukio yanayoituhumu serikali kuhusika.

  Katika hali ya kutatanisha, Josephine anahusisha madai ya kuwapo hata ushirikina ambao utatumika kumdhuru Dk. Slaa.

  “Kwenye kikao chao cha kidhalimu, mmoja wao akapendekeza matumizi ya ama uchawi au sumu inayoua taratibu. Huyu aliyependekeza anahofia kuwa njia yoyote itakayofanana na nyingine italeta kelele na dunia nzima itagundua. Anajaribu kuwashawishi wenziwe waachane na hiyo, isipokuwa watumie njia hizi mbili mbadala; sumu au uchawi,” anaeleza Josephine na kuendelea;

  “Jamaa wanamiliki wachawi wengi sana na wachawi hawa wako makundi mawili. Kundi la kwanza ni lile linalotumika kulinda viongozi na huwa linafanya kazi kila wiki mara moja. Kundi hilo liko kwenye payroll ya serikali.

  Anaendelea: “Kundi la pili ni lile la wachawi waliotaka kumuua .... (anataja jina la kiongozi) kipindi fulani. Kundi hili liko katika mazungumzo na ... (anataja kiongozi) kwa ajili hiyo.”

  Imeelezwa na mama huyo kwamba mkakati huo unapangwa kutekelezwa baada ya Dk. Slaa kurejea kutoka nje ya nchi.

  Katika madai yake hayo, Josephine anataja hadi namba za gari ambalo linaelezwa kutumika katika mkakati huo unaofanana na sinema ya Kinigeria.

  Mbali ya Dk. Slaa, mama huyo anadai kwamba kuna mpango wa kuwadhuru wabunge ambao wanaamini hawahongeki kifedha.

  Hata hivyo, viongozi mbalimbali wa serikali na watu mbalimbali, wameelezea tuhuma hizo kama njia ya kumchota akili Dk. Slaa ili kumuondoa katika hoja za msingi na hata kumtisha asirejee nchini na hazina ukweli wowote.

  “Hizi tuhuma zinachanganya sana maana inaonekana baadhi ya wanaotajwa ni wale wale wanaotajwa katika tuhuma nyingine na hii inaonesha kwamba ni madai ya kupikwa na watu wenye nia ya kutaka kummchezea akili Dk. Slaa na pengine kumfanya asiaminike katika jamii,” anaeleza kiongozi mmoja mstaafu serikalini.

  Habari zimethibitisha kwamba vyombo vya dola vimeanza kufuatilia kwa karibu taarifa hizo na huenda ikatolewa taarifa rasmi hivi karibuni, pamoja na kutokuwapo kiongozi aliyekuwa tayari kuzungumzia tuhuma hizo.
   

  Attached Files:

 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  Ni mke wake au mchumba wake?
  HALAFU, HIVI BADO WATU WANAAMINI USHIRIKINA? .... THATS STUPID!!
   
 3. aye

  aye JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  izi habari zilikuwako humu zikaondolewa fasta
   
 4. P

  Penguine JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Kama wapo na tunawaona waliotishwa kwa namna hiyohiyo inayoelezwa na huyo anaeitwa mchumba wa Dr. Slaa. Wakatishwa na kudhuriwa. Serikali kupitia vyombo vyake uchunguzi ikasema madai hayo ni uzushi tu! Walotishwa na kujitetea wakadhurika kweli, kwa nini mwenye akili asione ukweli wa madai ya huyu mama?
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mchumba .......... Anasema mume wake........???!!!!!! yupo nje ya nchi aki4marisha chama. huyu mama na mchumba wake wana kiwanda cha kutung uongo
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  This is very serious, na sijui kwanini kwa nje serikali haiamini uchawi, ndani ni watumiaji wazuri sana wa uchawi. Waweke wazi ili watu wapunguze kuuana, anayetuhumiwa kwa uchawi ashtakiwe badala ya wananchi kumkata mapanga!
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Mimi naona Slaa akae uhamishoni, akiendesha chama remotely, with advanced technology it is possible (hotuba za conference calls etc) aje tu wakati wa uchaguzi. This people kwa kweli wameamua!
   
 8. K

  Kima mdogo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchumba au mke??
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..magazeti mengine bwana.

  ..kwenye heading wanasema Josephine ni mchumba.

  ..kwenye sub heading wanam-refer Slaa kama mume.

  ..binafsi nikishaona makosa kama hayo huwa sijisumbui kusoma habari nzima.
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Kweli CCM wameshikwa pabaya sana wanafikiria kuua tu kwa sasa...sera zimegoma!!wakiua ndio watazidisha hasira kwa vijana wooote wapenzi wa Dr Slaa na CDM kwa ujumla!ndio mtaharibu kabisaaa....mtakosa ubunge hadi hamtaamini hata kama urais mkichakachua,haitasaidia maana wabunge wengi sanaa watakuwa vijana wa CDM,huko bungeni hakutakalika!!
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Walishafunga ndoa lakini nashangaa gazeti bado linamwita 'mchumba wake'.
  Mkuu wewe huamini kama kuna ushirikina? Sisemi kama unaamini katika ushirikina bali nauliza unaamini ushirikina upo?
   
 12. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hivi nani atamuua huyu babu wakati kaishajichokea? nonsense!
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  hizi habari zililetwa humu mara nne na zikaondolewa,sasa imekuja upya ikiwa ndani ya gazeti sijui hawa mods kama wataitoa au watafanya nini,tunatazama kwa karibu
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mod Naomba upige BAN gazeti la KULIKONI maana watu humu walikula BAN
  si kawaida

  PLEASE MOD DO THE NEEDFUL BAN KULIKONI NIMEREPORT [​IMG]
   
 15. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Inakera sana hii tabia ya ku copy na ku paste ...let's try to be creative walau kidogo basi
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Bado ni Wachumba mpaka leo?
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  Kweli?
   
 18. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kiwanda cha umbea on motion
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mazinguzi tu haya, mpaka leo wachumba wakati weshazalishana....?
  Basi watazeekea uchumbani.....!!
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  sometime DR. na riz1 akili zenu zinakuwa na akili
   
Loading...