Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Philipo Mwakilima ambaye ni Wakili wa Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyangali amesema kuwa taarifa alizopewa na maafisa wa Jeshi la Polisi ni kuwa wateja wao ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya uhaini pamoja Dk. Slaa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani Mkoani Mbeya hii leo Agosti 16, 2023.
Ameyasema hayo akizungumza na Watetezi tv ilipofanya nae mahojiano kujua nini kinaendelea dhidi ya watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa zaidi ya saa 48.
Ikumbukwe watuhumiwa hao Mdude na Mwambukusi walikamatwa kwa pamoja mkoani Morogoro huku Dk. Slaa akikamatwa kwa wakati tofauti lakini wote wakidaiwa kukabiliwa na tuhuma za uhaini.
Hata hivyo baadhi ya wadau ambao ni Watetezi wa Haki za Binadamu ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Jukwaa la Katiba Tanzania wamepaza sauti wakitaka watuhumiwa hao kuachiwa bila mashariti au kufikishwa mahakamani.
Jana ilibuka taarifa kutoka kwa Wakili wa Dk. Slaa kuwa hafahamu mteja wake alipo ikiwa ni baada ya kushindwa kumuona kwenye kwenye kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es salaam.
Lakini itakumbukwa kukamatwa kwao kulikuja ikiwa ni muda mchache baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura kutoa tamko mbele ya Wanahabari akudai kuna watu wana njama ya kutaka kuiangusha Serikali akisisitiza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi yao huku akiwataka wananchi kuwapuuza watu hao aliodai kuwa wanaandaa maandamano yasiyo na ukomo.
Source: Watetezi TV