CHAKUHAWATA wajibu tuhuma za viongozi wao kugawana Tsh. Milioni 400 za michango ya Wanachama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Chama cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA) kimejibu tuhuma kuwa kuna baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho wanafuja fedha za michango ya Wanachama kwa kugawana zaidi ya Tsh. Milioni 400.

Kufahamu zaidi kilichosemwa kuhusu tuhuma hizo, soma hapa - CHAKUHAWATA wawageuza Walimu upatu, wagawana milioni tsh milioni 400

Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Kutetea na Kulinda Haki za Walimu Tanzania (Chakuhawata), Ashery Kisogoro Ntayomba amezungumza na JamiiForums na kusema hakuna ukweli kuhusu tuhuma hizo na kuwa zinafanywa na watu wasiowatakia mema.

Amesema “Ninachoweza kujibu kwa ufupi ni kuwa habari hiyo ya viongozi wa Kitaifa wamegawana zaidi ya Milioni 400 na madai kuwa wanagawana mgawanyo wa fedha za michango Tsh. 3000 kwa Tsh. 2000, hicho kitu hakipo.

“Ukitaka nitoe au upate taarifa zaidi au maelezo ya tuhuma hizo basi aliyeleta mada naye alete ushahidi.”

Ameongeza “Mapato na matumizi ya taasisi zote Duniani zinapaswa kuwa wazi, taarifa zipo na tunazipeleka kwa msajili ili tuweze kutambulika.”

Alipoulizwa madai kuwa kuna Wanachama wao ambao wamekuwa wakikatwa mara mbili kuchangia michango kwao na kwenye chama walichokuwa awali, amesema “Madai ya kukatwa mara mbili labda ungesema hilo linafanyika kwa Wanachama wetu wa wapi, lakini changamoto hiyo ilikuwepo kwa Wanachama kadhaa lakini kwa sasa haipo.”
 
CHAKUHAWATA WAJE KILINDI TANGA HAKUNA OFISI NA TUNATAKA KUJUA KWANINI KILINDI HAKUNA OFISI ZAO WAJE WAFUNGUE OFISI NA TUTASIMAMIA HILO MPAKA LIWEZEKANE.
 
Na wenyewe wanatakiwa kuwa wawazi kwenye makato ya 5000 ya wanachama wao wa sasa. Kinyume na hapo watakuwa hawana tofauti na wale wanyonyaji wa muda mredu wa walimu; yaani CWT.
 
Alipoulizwa madai kuwa kuna Wanachama wao ambao wamekuwa wakikatwa mara mbili kuchangia michango kwao na kwenye chama walichokuwa awali, amesema “Madai ya kukatwa mara mbili labda ungesema hilo linafanyika kwa Wanachama wetu wa wapi, lakini changamoto hiyo ilikuwepo kwa Wanachama kadhaa lakini kwa sasa haipo.”
Hence Proved kwamba wanakula hela...
Hawawezi kukwepa hili kwa maelezo yao
 
Ni ukweli fedha wanagawana ,kwanini msajili aliwapa Notisi tarehe 29,kwanini hawafuatii utaratibu katika matumizi ya fedha zao kuanzia ngazi ya wilaya hawana Katibu wala mwekahazina kuna mtu anaeitwa Katibu msaidizi ambae wanadai ni Mwenyekiti...tuambie utaratibu wa katiba na kanuni zetu katika utoaji wa fedha zenu
 
CHAKUHAWATA WAJE KILINDI TANGA HAKUNA OFISI NA TUNATAKA KUJUA KWANINI KILINDI HAKUNA OFISI ZAO WAJE WAFUNGUE OFISI NA TUTASIMAMIA HILO MPAKA LIWEZEKANE.
Bila nyie wenyewe wa kilindi kupambana haitakuwa kazi nyepesi.
Kukusaidia tu ni kuwa kufikia januari mosi mtakuwa mmefikiwa wasiliana na kaimu katibu wa CHAKUHAWATA hapo kilindi.
Changamoto ya kukosa barua ya kumtambulisha kwa mwajiri itakuwa imetatuliwa kufikia januari mosi.
 
Back
Top Bottom