Nakubaliana na wewe, na kubaliana na kuwa Slaa ni tishio kwa viongozi wa CCM ila sikubaliani na madai niliyosoma hapo kwenye gazeti. Kuamini kwangu kuwa Slaa yupo katika hati hati hakunipi sababu yeyote ya kuamini kila lisemwalo baya ama lolote la kuonesha "imani yangu ya usalama wake" ni sawa, na hii nazungumza kwa vigezo hivi... (Labda unipe sababu za kushiba to convince me otherwise);
Kuna habari mtu ukipata hata kama ya kushtua inatakiwa saana kuiangalia kwa umakini na undani pia. Kwa mtazamo wangu naona kuwa Madame Slaa kwa hili kachemka.. Hiii ya yeye kuongea na kuachia wazi hii (kama kweli ni yeye kasema haya) inafanya habari ionekane na uwakakini mkubwa sana! Habari kama hii ni lazima u question sio tu kuipokea ilivo...
1. Kwa habari nzito kama hizi je kazipeleka moja kwa moja kwa Chama (CDM) ili kuona muitikio na reliability ya hii habari hasa in the lines of verification?
2. Yeye ni mke wa Slaa, hivi kweli haoni implications za yeye kutangaza hii habari as opposed kama mwingine angetuma?
4. Sitaki kuamini kuwa Dr Slaa anaweza pata habari then ampe Madam Slaa kuzisambaza (kama ni hivo nina wasi wasi na Msimamo wa maamuzi ya Slaa hasa kwa kuhusiana na Uongozi wake). Labda sababu tumejaaliwa kuwa nae kama member ningependa sana dada
Josephine kama anaweza eleza kuwa yeye hizi habari anazichukuliwa vipi?
5. Nini hasa lengo ya kuachia habari kama hii? Hii habari ni nzito sana na mara ya kwanza kuiona nilijua ni uzushi na wamemuonea, sasa sababu ni kweli nabaki nikijiuliza yeye kama mke wa Slaa lengo kubwa la kuachia habari kama hii ilikuwa ni nini?
Bahati mbaya iliyoje, majority wanaichukua na kuamini habari kama ilivo bila hata kujiuliza… Huo kwa kweli inakuwa sio ushabiki tena. Inatia huruma, inakuwa sawa na mzazi unapomuongopea mtoto ale mboga za majani itamfanya aweze kupaa na hali inamsaidia tu kukuwa. Sad.
Nikirudi upande wa Serkali, nakubaliana na uliyoongea kuwa kwa kweli wamekuwa tishio na hawaaminiki... Lakini bado hainipi sababu ya mimi kuamini hii habari...