AKIBOA vs Madereva Moshi Arusha Ngoma nzito

Jun 20, 2023
55
52
Madereva wanaoendesha mabasi kati ya Arusha na Moshi wameibua tuhuma nzito juu ya viongozi wa chama cha wasafrishaji Moshi Arusha (AKIBOA) kwamba wanawatoza sh. 2,000 kila wanapopakia Abiria .

Kwamba fedha hizo hawajui zinapelekwa wapi na hawapewi stakabadhi ya malipo.

Tuhuma hizo zipo kwenye barua yao ya Januari 17 mwaka huu kwenda kwa mamlaka za serikali .

Kutokana na tuhuma hizo mamlaka za serikali zimechukua hatua za kuwahoji viongozi wa AKIBOA na jana kikao kizito kilifanyika kuanzia saa tano asubuhi hadi jioni.

"Piga hesabu Moshi Arusha zipo coaster ngapi na kila coaster inatoa 2000 kila siku na hatujui fedha hizi wanazipeleka wapi?"

"Tunataka hii biashara ikomeshwe mara moja maana hazipo kisheria na huu ni wizi kama wizi mwingine"

Ukitaka kujua mengi zaidi ni hapo Jumatatu tutakapopata kauli ya serikali na AKIBOA wenyewe
 
Back
Top Bottom