Mchinjita: Serikali Imefeli Kuondosha Uhaba wa Petroli na Diseli

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Utangulizi

Itakumbukwa kwamba tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilitangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. Bei hizo ziliibua malalamiko na vilio kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, kutokana na kupaa kwa bei hizo kwa wastani wa shilingi 463 kwa petroli na shilingi 391 kwa Diseli.

Sisi, ACT Wazalendo tulifanya uchambuzi wa kina wa hoja zilizoelezwa kusababisha kupanda kwa bei hizo na kubainisha sababu halisi zilizopelekea kupanda kwa bei hizo. Katika kukumbushia tulieleza kwamba sababu mbili zilizotajwa na Serikali hazikuwa za kweli. Hasa kuhusu gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji. Kutokana na uchambuzi wetu tulibainisha kwamba bei za mafuta katika soko la dunia kwa kuzingatia utaratibu wa kawaida wa ununuzi wa mafuta, ni kuwa mafuta yanayotumika mwezi Agosti ni yale yaliyoagizwa mwezi Juni ambapo bei zake zilikuwa zipo chini. Pia, hali hiyo ni sawa kwa gharama za uagizaji ambazo kwa mwezi huu zimekuwa za chini zaidi.

Aidha, tulikubaliana na sababu zingine zilizotajwa na EWURA kama vile changamoto ya uhaba wa dola za Kimarekani na kushuka kwa thamani ya shilingi. Vilevile tulionyesha uamuzi wa Serikali wa kuongeza kodi ya shilingi 100 na kuondoa ruzuku ya mafuta iliyokuwa inaitoa kwa lengo la kushusha bei za mafuta nchini ndio sababu kubwa katika kuongeza bei hizo.

Kutokana na hali hiyo tulipendekeza hatua kadhaa za kuhakikisha Serikali inakabiliana tatizo la kupaa kwa bei hizo ili kutoa nafuu kwa wananchi. Katika mapendekezo yetu tulionyesha hatua za haraka na za muda mrefu na tulionyesha hatua za kupunguza matumizi na kuongeza uzalishaji ili kutatua tatizo la uhaba wa dola. Tunashangaa sana kuona Serikali haijachukua hatua zozote madhubuti za kukabiliana na chngamoto hii.

Hali ya upatikanaji wa mafuta ya petroli na diseli.

Katika uchambuzi wetu tulioufanya Agosti 2, 2023 ulijikita zaidi katika kuangalia tatizo la kupanda kwa bei za mafuta na sababu zilizopelekea kupaa huko na tulitoa mapendekezo yetu ili kushusha bei hizo. Lakini hivi karibuni tumekuwa tukifuatilia kwa karibu zaidi juu ya hali ya upatikanaji wa mafuta nchini. Utafiti wetu umebaini kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta katika hifadhi ya mafuta bandarini (Dar es Salaam).

Changamoto ya upatikanaji wa mafuta imepelekea waagizaji wa mafuta hususani kwa waagizaji wadogo kuchelewa kupata mzigo kutoka bohari za bandari ya Dar es Salaam. Awali iliwachukua siku 1 tu sasa inachukua siku 3 hadi 4 kupata mafuta na kupakia katika Bohari za Dar es salaam jambo linalopelekea uhaba katika maeneo mengi. Hali katika bandari ya Mtwara imekuwa mbaya kwa mafuta ya petroli ambapo hayapatikani kabisa, jambo linaloplekea wauzaji wote waliokuwa wanachukua mafuta katika bandari ya Mtwara kulazimika kufuata Dar es Salaam.

Aidha, jambo lililotupa wasiwasi zaidi kutokana na taarifa za uhakika tulizopata kuhusu hifadhi ya mafuta yaliyopo yanaweza kukidhi mahitaji ya siku 8 tu. Ingawa tunafahamu uwezo wa nchi kuhifadhi mafuta ni wa mwezi mmoja, lakini tulikuwa tunaagiza mafuta kwa kutangulia miezi miwili. Lakini kwa sasa mafuta yanayotumika ni yale yaliyoagizwa mwezi huu wa nane.

Sababu kubwa inayopelekea kuwepo kwa tishio la uhaba wa mafuta nchini ni kupungua kwa uwezo wa kuagiza mafuta kwa waagizaji wetu. Tangu mwezi Machi kutokana na uhaba wa dola waagizaji wamekuwa wakipunguza kiasi wanachoagiza. Hii ni kutokana na uhaba wa dola za marekani na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania kwa dola, jambo linalopelekea waagizaji kupoteza kiasi kikubwa cha fedha katika kubadilisha shilingi kwenda dola za marekani.

Katika hali hii Serikali haipaswi kusubiria miujiza kukabiliana na changamoto hizi au kusubiri kutokea kwa athari kubwa zaidi ndio ichukue hatua za kunusuru. Hatari ya Serikali kutochukua hatua za haraka ni kupelekea kupandisha bei zaidi na kuongeza kiwango cha uhaba zaidi nchini. Hivyo basi, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali sasa ichukue hatua zifutazo kuhakikisha inakabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini;

  • Ni wakati sasa Serikali kuweka msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya Petroli na Diseli kwa kutumia nishati mbadala ya Gesi asilia. Hii inawezekana kwa kuchukua hatua kadhaa za haraka;
  • Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) na bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG)
  • Vilevile, mabasi ya mwendokasi nayo yabadilishwe mfumo na yaanze kutumia gesi asilia
  • Pia, magari ya abiria ya mikoani (mabasi) yote yafungwe mfumo wa kutumia mitungi ya Gesi asilia (CNG), ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta.
  • Serikali ianze kupunguza matumizi ya dola za Kimarekani kwa Benki Kuu kuruhusu wanunuzi wa mafuta kulipia kwa shilingi kisha benki hiyo ndio iwalipe wanunuzi wa nje kwa dola za Kimarekani ili kuwarahisishia wafanyabiashara ya mafuta wasihangaike kutafuta dola.
  • Hatua nyingine, ni kuhakikisha Serikali inadhibiti mahitaji ya dola kwa kuhakikisha matumizi yote ya Ndani yanafanywa kwa Shilingi yetu.
  • Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Ni muhimu kwa Serikali kuuza nje bidhaa zinazotokana na kilimo badala ya kuuza malighafi.
  • Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa watanzania.
Mwisho, tunaona tatizo la mafuta upatikanaji na gharama zake linahitaji hatua za makusudi za Serikali. Tunatambua hali ya upatikanaji wa dola unazikumba nchi mbalimbali lakini hatupaswi kukaa na kuridhika bila kuchukua hatua za kisera na kikodi au zile za uzalishaji.

Ndg. Isihaka Rashid Mchinjita

Twitter: @Isihakamchinji1

Waziri Kivuli wa Sekta ya Nishati.

ACT Wazalendo.

17 Agost 2023.
 
Nyie si ndo mnampaka rangi Samia. Imekuwaje tena
 
Back
Top Bottom