Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

kwa wasiowajua wachina ni kwamba ni WAZURI MNO KATIKA KUKARIRI. wanaweza kukariri mpaka NUKTA PACHA. kingine ,mimi sioni ajabu mchina kupata B ya kiswahili, Aangepata hata A nisingeshangaa kwa sababu hiyo ni lugha tu ukimakinika nayo utaijua tu na kizuri ni kuwa amejifunza katika nchi husika.Mbona kwao wanafunzi wa kigeni hujifunza lugha mwaka mmoja na kufanya mtihani wa lugha maarufu kama HSK na watu hufaulu kwa kupiga A za hatari. Tena kichina ni KIGUMU hasa "hanzi" sikwambii "tone" zake lakini watu wanafaulu. sasa hawa ni mwaka mmoja tu, seuze yeye kajifunza lugha kutoka darasa la pili?
Ninachokiona mimi ni kuwa sisi waswahili hatumakiniki na lugha kwa kule kujiona ni yetu basi tunajua. hata kwao hawa, wapo wachina wanafeli kabisa somo la kichina
cc Watu8
 

Eti wana IQ kubwa kuliko binadamu wote. Takataka. Historia ya IQ test ni ya kisiasa zaidi kuliko sayansi ya dhati.

Ina-elemea sana kwenye mazingira, kuliko genes. Kwa maana, hiyo muafrika na mchina wakikuzwa kwenye mazingira yaleyale, kwa wastani, watakuwa na IQ zinazofanana.
 
So IQ ni mazingira cio gene ya mtu?
 
Tuacheni utani wachina ni wagumu sana kuelewa huyo mchina ni genius tu kazaliwa hivyo.. Mimi nimesoma na wachina nchi za nje ni vilaza hatari. Wao wataluburuza tu kwenye Hesabu basi ..
sasa kama mtu anajua hesabu ,kuna uwezekano mkubwa kufanya vizuri masomo mengine
 
Mara tutasikia malalamiko kuwa "wachina wanachukua nafasi zetu katika mitihani, waondoke"!
Ha Ha Ha! Usinikumbushe O-Level miaka ileee ya 47. Kuna jamaa mmoja alikuwa ana akili sana. Alienda kwenye mkondo wa biashara baadae akabadili nia akaja darasani kwetu mkondo wa sayansi. Dah watu wakanza sema huyu anakuja chukua namba yetu huyu, matokeo yalikuwa yakitolewa kimkondo! Bila kujua kuwa kuja kwake kunasaidia ushindani!
 
Acheni upopona yani MTU anasoma feza halafu mnamsifia
 
Awajaji ubora was shule aliyokuwa anasoma wanajaji matokeo
 
Nawaza tuu, mchina anapata B ya kiswahili anasikitika lakini sisi PhD holder anashindwa kuzungumza kiingereza fasaha alichokitumia kusomea kwa miaka kadhaa mpaka kuhitimu na tunaona kawaida tuu
Unao uhakika na hicho unachokinena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…