Mchezo wa Sheria: Apoteza haki ya mgawanyo wa mali baada ya mume kudai hajawahi kumuoa Salma Mohammed, mke alibadili jina baada ya kuolewa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,821
Dar es Salaam. Hivi mwanamke aliyebadili jina la baba yake na kutumia la mumewe baada ya kuolewa anajua kama anaweza kupoteza haki ya kumiliki mali walizochuma katika ndoa? Hiki ndicho kilichompata Salma Mohamed Ibrahim.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa juzi na Jaji John Nkwabi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam, mke kutumia jina la mumewe kimazoea bila kulibadili kisheria (deed poll), haiwezi kuwa utetezi pale sheria inapokiukwa.

Mwaka 1993, Salma alifunga ndoa na Mohamed Ibrahim Adam, wakati huo akitumia jina la Salma Abdallah Salum baada ya kufunga ndoa, mumewe alimwambia atumie jina lake hivyo akabadili na kujiita Salma Mohamed Ibrahim.

Hata hivyo, mwaka 2019 Salma akafungua maombi ya talaka na mgawanyo wa mali katika Mahakama ya Mwanzo Temeke.

Mahakama hiyo ilikubali na kutoa mgawanyo sawa isipokuwa nyumba iliyopo Dodoma, Salma alipata kwa asilimia 20 tu.

Mumewe akakata rufaa Mahakama ya Wilaya Temeke akidai hakimu alikosea kwa kutotoa sababu za msingi za kushughulikia mgogoro huo, licha ya hoja yake kuwa hajawahi kumuoa mtu anayeitwa Salma Mohamed Ibrahim.

Katika majibu yake, mrufani (Salma) akaeleza kuwa aliolewa wakati akitumia jina la Salma Abdalah Salum na jina lake la pili ni Salma Mohamed Ibrahim.

Alisema baada ya kuoana, mumewe alimtaka atumie jina lake.

Alieleza hata walipokuwa wanakwenda Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), alikuwa akitumia jina la Salma Mohamed Ibrahim, lakini katika uamuzi wake, Mahakama ya Wilaya ikatengua uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama ya Wilaya kufuta hukumu ya Mahakama ya Mwanzo, Salma alipoteza haki yake ya mgawanyo wa mali walizochuma na aliyedai kuwa mumewe wa ndoa.

Salma akakata rufaa Mahakama Kuu akisema hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke alikosea pale alipokubaliana na sababu za rufaa za mumewe na kuwa kisheria hapakuwepo ndoa baina ya wawili hao.

Salma akapinga sababu za hakimu kuwa aliwasilisha maombi ya talaka kwa kutumia jina la ubini wa mumewe baada ya kuolewa, akisema upo ushahidi walikuwa wanandoa na majina yote mawili ni yake.

Wakili Gabriel Mnyele aliyemwakilisha Salma alisema wanawake hutumia jina la mume na kuhusu sharti la kubadili jina kisheria (deed poll), huo ni wema wa kisheria ambao Salma kama mama wa nyumbani ni vigumu kuufahamu.

Akijibu hilo, wakili Alex Enock aliyekuwa akimtetea mume wa Salma, alisema uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ni sahihi na unastahili kupata baraka za Mahakama hiyo ya juu yake.

Hukumu ya Jaji
Katika hukumu hiyo, Jaji Nkwabi alisema kuna maswali ya kujiuliza kuwa kama inawezekana mtu kubadili jina lake bila deed poll na kama ni sawa kisheria kwa mtu kutumia jina lingine bila kuwa na deed poll ambayo ni takwa la kisheria.

“Ni sheria kwamba mtu hawezi kuvunja sheria na kuja mahakamani kuomba msaada na kusikilizwa na Mahakama ya sheria. Mrufani (Salma) alitakiwa na sheria kusajili mabadiliko ya jina lake,” alisema Jaji.

“Hakufanya hivyo au hakuthibitisha kuwa alisajili mabadiliko hayo ya jina. Kwa hiyo hilo jina (la mumewe) alilorithi halitambuliwi na sheria. Hiyo haiwezi kuitwa ni wema tu wa kisheria kama wakili wake alivyotaka Mahakama iamini.”

Jaji Nkwabi alisema ile Mrufani kuwa mama wa nyumbani sio utetezi wa kufanya mambo nje ya sheria, hivyo akatupilia mbali rufaa ya mwanamke huyo na kubariki uamuzi ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke iliyofuta ushindi wake wa awali.

Mwananchi
 
Kutokujua sheria sio sababu ya kutokupata hukumu stahiki. Sheria haina konakona inanyooka.
 
Replica Aombe rufaa CA atashinda...ile equity maxim inaweza kumsaidia.....Inasema hivi: "One o f the Maxims o f Equity is that 'Equity treats as done that which ought to have been done'..... as long as waliishi kama mke na mume lkn akasahau kubadili jina, hiyo maxim itamsaidia
 
Akili za wanawake wa saizi ni kuolewqq alaf wachike ili wapate mali ambazo hawajazitolea hata tone la jasho. Shubastic
 
"Wema wa sheria" mawakili huwa wanajitahidi sana mahakamani kuwatetea wateja wao.

Huo msemo sijui upo kwenye sheria ipi kifungu namba ngapi!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Patamu hapo. Ila kwa nini binadamu tumekuwa watu wa kujali mali zaidi pasipo na ubinadamu? Hivi unajisikiaje mtu ambae mmepotezeana ujana ukashindwa kumpa chochote kwenye kuachana kwenu?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Hilo hata mini nimewqza japo inaonekana kuna bifu kubwa sana na chanzo inawezekana ni mali ndio maana jamaa kaamua kumkomalia.
 
Kuna kulea watoto pia ....nadhani mume atabakia na watoto.....ila mali vs ubinadamu hadi high court.....inaonekana nyumba za maana labda....
 
Dar es Salaam. Hivi mwanamke aliyebadili jina la baba yake na kutumia la mumewe baada ya kuolewa anajua kama anaweza kupoteza haki ya kumiliki mali walizochuma katika ndoa? Hiki ndicho kilichompata Salma Mohamed Ibrahim.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa juzi na Jaji John Nkwabi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam, mke kutumia jina la mumewe kimazoea bila kulibadili kisheria (deed poll), haiwezi kuwa utetezi pale sheria inapokiukwa.

Mwaka 1993, Salma alifunga ndoa na Mohamed Ibrahim Adam, wakati huo akitumia jina la Salma Abdallah Salum baada ya kufunga ndoa, mumewe alimwambia atumie jina lake hivyo akabadili na kujiita Salma Mohamed Ibrahim.

Hata hivyo, mwaka 2019 Salma akafungua maombi ya talaka na mgawanyo wa mali katika Mahakama ya Mwanzo Temeke.

Mahakama hiyo ilikubali na kutoa mgawanyo sawa isipokuwa nyumba iliyopo Dodoma, Salma alipata kwa asilimia 20 tu.

Mumewe akakata rufaa Mahakama ya Wilaya Temeke akidai hakimu alikosea kwa kutotoa sababu za msingi za kushughulikia mgogoro huo, licha ya hoja yake kuwa hajawahi kumuoa mtu anayeitwa Salma Mohamed Ibrahim.

Katika majibu yake, mrufani (Salma) akaeleza kuwa aliolewa wakati akitumia jina la Salma Abdalah Salum na jina lake la pili ni Salma Mohamed Ibrahim.

Alisema baada ya kuoana, mumewe alimtaka atumie jina lake.

Alieleza hata walipokuwa wanakwenda Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), alikuwa akitumia jina la Salma Mohamed Ibrahim, lakini katika uamuzi wake, Mahakama ya Wilaya ikatengua uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama ya Wilaya kufuta hukumu ya Mahakama ya Mwanzo, Salma alipoteza haki yake ya mgawanyo wa mali walizochuma na aliyedai kuwa mumewe wa ndoa.

Salma akakata rufaa Mahakama Kuu akisema hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke alikosea pale alipokubaliana na sababu za rufaa za mumewe na kuwa kisheria hapakuwepo ndoa baina ya wawili hao.

Salma akapinga sababu za hakimu kuwa aliwasilisha maombi ya talaka kwa kutumia jina la ubini wa mumewe baada ya kuolewa, akisema upo ushahidi walikuwa wanandoa na majina yote mawili ni yake.

Wakili Gabriel Mnyele aliyemwakilisha Salma alisema wanawake hutumia jina la mume na kuhusu sharti la kubadili jina kisheria (deed poll), huo ni wema wa kisheria ambao Salma kama mama wa nyumbani ni vigumu kuufahamu.

Akijibu hilo, wakili Alex Enock aliyekuwa akimtetea mume wa Salma, alisema uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ni sahihi na unastahili kupata baraka za Mahakama hiyo ya juu yake.

Hukumu ya Jaji
Katika hukumu hiyo, Jaji Nkwabi alisema kuna maswali ya kujiuliza kuwa kama inawezekana mtu kubadili jina lake bila deed poll na kama ni sawa kisheria kwa mtu kutumia jina lingine bila kuwa na deed poll ambayo ni takwa la kisheria.

“Ni sheria kwamba mtu hawezi kuvunja sheria na kuja mahakamani kuomba msaada na kusikilizwa na Mahakama ya sheria. Mrufani (Salma) alitakiwa na sheria kusajili mabadiliko ya jina lake,” alisema Jaji.

“Hakufanya hivyo au hakuthibitisha kuwa alisajili mabadiliko hayo ya jina. Kwa hiyo hilo jina (la mumewe) alilorithi halitambuliwi na sheria. Hiyo haiwezi kuitwa ni wema tu wa kisheria kama wakili wake alivyotaka Mahakama iamini.”

Jaji Nkwabi alisema ile Mrufani kuwa mama wa nyumbani sio utetezi wa kufanya mambo nje ya sheria, hivyo akatupilia mbali rufaa ya mwanamke huyo na kubariki uamuzi ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke iliyofuta ushindi wake wa awali.

Mwananchi
Mahakama haina huruma.
 
Replica Aombe rufaa CA atashinda...ile equity maxim inaweza kumsaidia.....Inasema hivi: "One o f the Maxims o f Equity is that 'Equity treats as done that which ought to have been done'..... as long as waliishi kama mke na mume lkn akasahau kubadili jina, hiyo maxim itamsaidia
Na huko CA akipigwa chini,najua bado utamwambia aombe Review ya kesi!!
 
Back
Top Bottom