Dar: Mke wa Bilionea Msuya akutwa na Kesi ya Kujibu mauaji ya wifi yake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa mke wa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya, maarufu kwa jina la Bilionea Msuya, Miriam Mrita, anayetuhumiwa kumuua wifi yake, Aneth.

Mbali na Mrita mshtakiwa mwingine aliyekutwa na kesi ya kujibu ni mfanyabiashara Revocatus Muyela. Wamedai kuwa watapeleka mashahidi na vielelezo kuthibitisha tuhuma hizo dhidi yao na pia watajitetea kwa kiapo.

Uamuzi huo mdogo ulitolewa na Jaji Edwin Kakolaki wa mahakama hiyo, baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi kwa mashahidi 25 na vielelezo mbalimbali kikiwamo kisu ambacho kinadaiwa kilitumika kumchinjia Aneth koromeo.

Jaji Kakolaki alisema mahakama baada ya kuzingatia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa, imejiridhisha kwamba kuna kesi ya msingi ambayo inawatosheleza washtakiwa wajitetee kama sheria inavyotaka.

"Washtakiwa simameni, kwa mujibu wa kifungu 293 (2) na (a) (b) na cha (3) mahakama inawafahamisha pamoja na haki zenu nilizokwisha waeleza na pia mawakili wenu watawaelewesha kama mtakuwa hamjaelewa vizuri.

NIPASHE
 
Ila huwa nashindwa kuwaelewa ndugu wanaoanza kugombania mali za ndugu yao baada ya kufariki. Kama ana familia acheni mali kwenye hiyo familia inatosha. Kugombania mali ni dalili za uvivu sawa sawa na ule wa kusubiria urithi.
Makabila ya kaskazini ndio ujinga wao mkubwa ....Usikubali ndugu yako akaolewa huko akifa anapokonywa mali za mumewe zote ...

Dada yangu kaolewa naalewa ,kikubwa kakaza mpaka wamejenga huko Morogoro wanataka kila kitu kipelekwe huko kwao.
 
Hao wakina Msuya ndio wana tatizo,jamaa yenu kashaoa nyie bado mnamfuata tu ...Haya mtu kashafariki bado mnataka mali na kuanza kumuandama wifi yenu kwa nni asiwamalize.

Wajinga wote wamekosa mali, yule aliyeuliwa alikuwa na mdomo sana .
Mkuu una uhakika na unachokisema.......? Au wewe ni sehemu ya familia ya huyo mwanamke.
 
  • Hii kesi Kuna mkanganyiko mkubwa Sana, Shahidi ambaye inasemekana kuwa alikuwa ni mfanyakazi wa Ndani wa aneth msuya, kwa mujibu wa Kibatala ni kuwa hiyo sio mfanyakazi wa Ndani wa aneth msuya Bali ni police
  • Kingine First Crime Report (taarifa ya awali ya kosa la jinai) inasema kuwa mtuhumiwa ni Getrude Peniel Mfuru (mfanyakazi wa Ndani wa aneth msuya) lakini, walioshitakiwa ni Miriam Mrita na Revocatus Muyella, Huyu aliyetajwa kwenye First Crime Report kaletwa Kama Shahidi wa 25 (Shahidi wa Mwisho)
  • Kingine ni Taarifa aliyoileta Sajenti Obadiah, inasema hivi postmortem imefanyika asubuhi ya tarehe 27/5/2015 wakati mauaji yametokea usiku, inawezekanaje hili?
  • Kingine ni kwenye Gwaride la utambulisho nalo Kuna makosa mfano, PGO inataka walete picha ya mnato waliofanyiwa Gwaride mahakamani, Kingine PGO inasema kuwa anayetakiwa kuandaa Gwaride la utambulisho anatakiwa kuwa gazetted officer yaani awe na cheo Cha mrakibu msaidizi wa police (ASP), lakini kwenye ushahidi ulioletwa unaonesha kwamba Gwaride la utambulisho liliandaliwa na Assistant inspector kinyume na PGO
-
 
Back
Top Bottom