Mch. Mwasapile vs. Mch. Rwakatale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Mwasapile vs. Mch. Rwakatale

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Ms Judith, Mar 15, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.

  binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.

  sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.

  kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!

  binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!

  siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)

  naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.

  HUKUMU NI ZAKE BWANA

  mbarikiwe sana wapendwa

  Glory to God
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  PHP:
  binafsi nashindwa kuiita karamauwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakatihainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samungehauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!
  Mbona huulizi kwanini yesu alipokuwa anaponya watu mfano alipokuwa anamponya yule kipofu alichukua mate akachanganga na udongo akapaka machoni pa yule jamaa na akaona. Mbona asimwambie ona tu na akaona. Au mbona Yesu alipokuwa harusini mjini kana aliwaambia watu wajaze maji yale mapipa, mbona huulizi asingeeamuru tu mapipa yajae divai? So hili ni swala la imani and the way it is executed sioni shida, it depends Mungu anataka adhihirike vipi na wapi na kwa namna gani. So kwa kuwa ni swala la imani then sioni sababu ya kuhoji mashart ya Babu...
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hata dawa za hospitalini zinategemea neema ya mungu na hufanya kazi pale utakapoamini kwamba nikitumia dawa hizi nitapona ..... hata dawa za hospitalini zina prescription... panadol 2X3 per day ....... hata chakula unakula kwa kipimo .... oz na kadhalika
   
 4. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  I agree with you da Judy!!
   
 5. Kagwina

  Kagwina Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imani haiulizwi maswali, Yesu aliponya watu kumi wenye ukoma kwa kuwaambia waende wakajisafishe na maji ya Mto Yordan, mbona huulizi? Tatizo vizazi vya sasa kila kitu mnataka kutumia sayansi kupima kama Waziri wa Afya! Hata wakati wa Nuhu watu walibisha vivyo hivyo kwa kutoamini kuwa mvua inaweza kunyesha na kufunika ardhi yote, kwao hii ilikuwa ni ngumu sana kuamini.
   
 6. k

  kimini Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pia hata angefanya jinsi unavotaka wewe, kuna mwingine angependa jinsi anavofany leo hii Babu. Hapa ni suala la imani ndugu.suala la theologia ni kanuni tu.. hizo ni kama njia tu ila lengo ni moja tu kupona.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,594
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Juddy can you question Holy Spirit?

  Unless you have all knowledge about Holy Spirit you cant question various styles of Holy Spirit.

  Believe me beliefs are very complicated that that if you are not careful you easily become confused.

  Every mirarcle that were performed in the bible was unique! Holy Spirit operates in that way, unless you are GOD!
   
 8. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona huulizi kwanini yesu alipokuwa anaponya watu mfano alipokuwa anamponya yule kipofu alichukua mate akachanganga na udongo akapaka machoni pa yule jamaa na akaona. Mbona asimwambie ona tu na akaona. Au mbona Yesu alipokuwa harusini mjini kana aliwaambia watu wajaze maji yale mapipa, mbona huulizi asingeeamuru tu mapipa yajae divai? So hili ni swala la imani and the way it is executed sioni shida, it depends Mungu anataka adhihirike vipi na wapi na kwa namna gani. So kwa kuwa ni swala la imani then sioni sababu ya kuhoji mashart ya Babu...[/QUOTE]

  Miss J, utaumiza kichwa bure kutaka kuhoji juu ya uwezo wa Mungu kutaka kuwaponya / kuwakomboa watu wake. Jiulize: Kulikuwa na haja gani MUNGU mwenye uwezo kumtuma mwanae wa pekee eti aje duniani, ateswe na afe kifo cha aibu msalabani eti KUTUKOMBOA? Si Mungu angeweza kusema tu tena kwa neno moja nasi tukakombolewa!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Masharti yapo...kila tiba/dawa ina masharti yake. Hata Yesu,mra kadhaa alikuwa akiwapa masharti watu anaowapa tiba/uponyaji!


   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Samahani sana mkuu yaani "babu" unataka kumfananisha na Yesu????????? Khaaaaa yaani wewe jamaa wa ajabu sana unamfananisha Messi na Ngasa?! Yesu ni world ICON huwezi kumfananisha na mtu wa kawaida mkuu..............
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hata wewe mbona hujiulizi pia kuwa kwa nini Yesu huyo huyo alimpaka kipofu tope, lakini alipokutana na Bartimayo kipofu alimwambia tu nataka uone na akaona? Na wengine aliwaambia wakajionyeshe tu kwa makuhani na njiani wakapona automatically?

  Elewa ya kuwa Neno linapokujia kwa ajili ya mtu mmoja (maono au Rhema) huja kwa makusudi maalum na inaweza kuwa ni kwa mtu mmoja tu au muda fulani. Lakini unapoescalate inakuwa doctrine (logos) hapo ndipo tatizo huanza. Ikiwa babu aliambiwa ni kwa ajili ya mtu mmoja na anaendelea kuwa maelfu ya watu anakosea, lakini kama aliambiwa atawapa watu wengi, it is well and good.

  Besides nani anajua for sure kuwa sauti aliyoisikia ilikuwa ya Mungu na si vinginevyo? imani huja kwa kusikia.
  - Mohamed alisikia sauti akaanzisha Islam
  - Sindatha Gautama alisikia sauti na akasema he was enlighted akaanzisha Budhism
  - Waanzilishi wa madhehebu na dini zote duniani ukisoma historia zao utaambiwa walisikia sauti zikiwaambia kuanzisha dini au madhehebu/huduma
  *The big question was real God's voice?
   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hata siku ya mwisho kunawatu wataambia Mungu ni yule Pale, ila lazima watauliza na Shetani yuko wapi.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!

  Ndugu mpendwa ufahamu ni jambo muhimu sana,Wana ufahamu ktkt kumjua Mungu na si ktkt maarifa
  ,unaweza ona ufahamu ni muhimu sana ,,nianze kwa kueleza hapo juuu
  usiogope sana babu kuponya kwa maji,,kumbuka miujiza iko mingi na kwa njia nyingi tu,..kumbuka mfalme naamani aliponywa kwa tope,na kumbuka aligusa maji ndipo akapata tope lililomponya,,

  Kuhusu swala la masharti..hiyo isitie shaka..kila uponyaji unakuja kwa jinsi yake....anachofwata babu ni kumfwata na kumheshimu roho mtakatifu ndio maana hata serikali waliojaribu kupinga leo waziri wa afya na u DK wake amefunga domo..kwa nini biblia iko wazi na alaaniwe ashindanae na rohomtakatifu....
  Babu awezi kumbuka kila mtu ana visasi vya familia.aijalishi umelaaniwa..so siwezi kukupa just ilimradi ugawe maji ..je kisasi ulichotupiwa wakaenda kuteseka watanzania babu atajibu nini??hicho ndicho anachokiogopa zaidi
   
 14. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nakushukuru mpendwa.

  kwa haya machache uliyoandika umesaidia sana angalau watu wajue kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya huyo babu na Yesu. kilicho dhahiri hapa ni kuwa hata baadhi ya wanaonukuu biblia, hawaijui vizuri biblia yenyewe.

  pia sijui kwa nini wameamua kukaa kimya kuhusu vitambaa vya rwakatare!

  Glory to God
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  MISS JUDITH
  KWANZA NINGEFURAHI UBADILISHE AVATOR YAKO,MAANA KWA BABU UKIJA HIVYO ANAKUPA MKOJ BADALA YA MAJI..YAANI HATA UKINYWA MAJI UTOPONA

  PILI SINA PINGAMIZI NA WAZO LAKO.HAYO N MAONI NA UKATAZWI KUYATO..ILA UKIWA KAMA MTUMISHI WA MUNGU NAOMBA UZIDI KUMWOMBEA BABU AZIDI KUISHI NA ZAIIDI YA YOTE OMBEA KUSUDIO LA MUNGU LITENDE KAZI JUU YAKE HICHO NDICHO MUHIMU ZAIDI...WAPO WAKINA DK MANYUKI WAMESIMAMISHA HEKAHEKA ZA WATU WENGI WALIOKUWA WAMELALA LAKINI KWA KUWA KUSUDI LA MUNGU ALIKUWA JUU YAKE LEO HII WENGI NI ZAIDI YA SUPERGET,NINI NAKUSHAURI USIKATE TAMAA MUNGU ANAJIDHIRISHAKWA WATU WENGI NI SISIS NA IMANI YETU..WAKATI MWINGINE TUJUE SHETAN NAE ALALI..TENA ANAKESHA KUPITA WATU WA MUNGU SOMA BAIBO..SO WEWE KAMA MTUMISHI WA MUNGU OMBA KUSUDI LA MUNGU JUU YA BABU LITENDE KAZI NA ZAIDI YA YOTE AKUPE IMANI ZAIDI YA THOMASO......

  UBARIKIWE MPENDWA
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  jana nilikuwa naangalia EMMANUEL TV ya TB JOSHUA kwa wale wanaofuatilia yeye anaponya kwa ktumia maji yanaitwa anointed water ssa hivi kaleta mpya ipo kwenye chupa ndogo saana km zile za rangi ya kucha. sasa alichosema ni kuwa ile chupa alibidi iwe tupu lkn alimwomba mungu aweke maji kwa vile kizazi hiki kisicho na imani wala matumaini itakuwa vigumu kuamini so mle ndani kuna maji na yana nguvu ya ajabu. hapa nataka kuwaambia wale wasio na imani kwamba babu anaponya kwa kile kikombe na mizizi ile ikishabarikiwa inakuwa na nguvu ya ROHO MTAKATIFU wewe binadanu wa kawaida unaona maji ya kawaida lkn ROHO MTAKATIFU anakuwepo pale kukupa wewe uponyaji
  v
   
 17. t

  toyoyobig Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, nadhani umefika njia panda kidogo. Labda nikusaidie kidogo kuhusiana na maandiko juu ya oponyaji na imani. Labda tusome Yohana 5:2 NAHUKO YERUSALEM ( Arusha, Loliondo) PENYE MLANGO WA KONDOO PANA BIRIKA, IITWAYO KWA KIEBRANIA BETHZATHA, NAYO INA MATAO MATANO. 3 NDANI YA HAYO JAMII KUBWA YAWAGONJWA WALIKUWA WAMELALA, VIPOFU, VIWETE, NAO WALIO POOZA, WAKINGOJA MAJI YACHEMKE ( wakingoja dawa ya babu ichemke). 4 KWA MAANA KUNAWAKATI AMBAPO MALAIKA HUSHUKA, AKAINGIA KATIKA ILE BIRIKA( kikombe cha babu tayari malaika alisha shuka wakati dawa ya babu inachemka), AKAYATIBUA MAJI. BASI YEYE ALIYE INGIA WA KWANZA BAADA YA MAJI KUTIBULIWA, AKAPONA UGONJWA WOTE ULIO MPATA.( hapa sasa ni tofauti na babu, kwa babu yeye sio mtu anayekunywa wakwanza dawa, bali WOOOOTE watakao kunywa dawa kwa imani ya kupona WATAPONA, HAKUNASHARTI LA MARAMOJA KWA MTU MMOJA KWA SIKU) (ENDELEA KUSOMA HADI MSTARI WA 9)[/B]. Sasa ndugu yangu, n kwamba hakuna namna, sisi wanadamu tunavyo weza kumpangia Mungu juu ya uponyaji wake, ama kufikiri Mungu anatibu kwa namna moja tu ama kama tutatakvyo taka sisi.

  Pia tafakari namna NAAMAAMAN ALIVYO PONYWA UKOMA WAKE 2 Wafalme 5:1-27, hapa utaona namna Naaamana alivyo ponywa, lakini alipo pewa masharti ya kuponywa hakuamini hadi wafanyakazi wake walipo mshawishi ndipo akakubali akaenda na kujichovya mara SABA naye akapona.


  Lakini hata Yesu ALIPO WAPONYA WATU ALIWAPA MASHARTI YA KUTO TENDA DHAMBI TENA BAADA YA UPONYAji, (Hii ni sawa na kwa babu kuambiwa unakunywa dawa mara moja, kwa maana Mungu anakuponya mara moja tu, ukirudia dhambi ukapata tena ukimwi inamaana nafasi ulipewa ukamjaribu tena Mungu) sasa hapa tofautisha kutenda dhambi nakusamehewa dhambi, na kutenda dhambi na uponyaji ni vitu viwili tofauti.

  Swala la vitambaa vya mama Lwakatare, Soma Matendo 19:11-12 sasa hapo kunahitajia kana ufahamu wakiroho, maanake nirahisi sana kwa watu kutumia style hii hali hivyo vitambaa vimechakachuliwa na nguvu za giza.


  Mungu awabariki wote.
   
 18. Rainbow

  Rainbow Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You're very wrong my friend. kwanza spelling za hilo jina, pili, kama kuna mtu amekwambia kuwa Muhammad (pbuh) ndie alieanzisha uislam huyo amekudanganya. na km kuna mtu amekwambia kuwa Yesu (amani juu yake) ameanzisha ukristo nae pia kakudanganya. go do your homework properly.
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Kama wanapona kweli basi tumpe nafasi maana kwanza kajionyesha hamaindi pesa ,na gurani inasema kila gonjwa mungu kaweka tiba,tutajua tu kama ni mambo za kinaijeria ama ni vipi after yote bible ilisema siku za mwisho watatokea manabii wengi wakifanya kuponya kwa uwezo wa yesu ambaye siku ya mwisho wakitaka kufunguliwa mlango wa peponi watasema tuliponya kwa jina lako naye yesu atawambia ONDOKENI SIWAJUI ni unabii unatimia kutakuwa na matetemeko(japan,ireland)tetesi za vita-mashariki ya kati.
  Mwisho uko karibu zaidi udhaniavyo kuna watu wametabili disemba 2012 mambo yanayotokea sasa yananifanya niwaze sana hebu google 2012 end of world usome mwenyewe.hata wimbi la uarabuni linaloendelea wanasema ni maandao ya the return of mahd,yani masiha alieahidiwa kama ni kweli tuna mwaka mmoja tu na nusu TUBU.and google that upime mwenyewe
   
 20. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Kama wanapona kweli basi tumpe nafasi maana kwanza kajionyesha hamaindi pesa ,na gurani inasema kila gonjwa mungu kaweka tiba,tutajua tu kama ni mambo za kinaijeria ama ni vipi after yote bible ilisema siku za mwisho watatokea manabii wengi wakifanya kuponya kwa uwezo wa yesu ambaye siku ya mwisho wakitaka kufunguliwa mlango wa peponi watasema tuliponya kwa jina lako naye yesu atawambia ONDOKENI SIWAJUI ni unabii unatimia kutakuwa na matetemeko(japan,ireland)tetesi za vita-mashariki ya kati.
  Mwisho uko karibu zaidi udhaniavyo kuna watu wametabili disemba 2012 mambo yanayotokea sasa yananifanya niwaze sana hebu google 2012 end of world usome mwenyewe.hata wimbi la uarabuni linaloendelea wanasema ni maandao ya the return of mahd,yani masiha alieahidiwa kama ni kweli tuna mwaka mmoja tu na nusu TUBU.and google that upime mwenyewe
   
Loading...