SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,616
- 7,863
Nina maswali mengi sana yananiumiza kichwa na majibu yako ya jumla yanazidi kunichanganya, hivi huyu "babu" aliongea na Mungu kama alivyoongea na Musa wakati anampa amri kumi?
Hapana, kwa maelezo yake (Babu) ni wazi hakuwa anaongea na Mungu kama ilivyokuwa kwa Moses. Yeye amekuwa akipewa maelekezo na Mungu ndotoni. Mimi ninachokataa ni hoja ya kukataa 'unabii' huo kwa kigezo cha hiyo pesa inayotozwa.
Nadhani pengine kinachotupa shida watu wengi ni kutofahamu uwezo wa Mungu na namna anavyofanya kazi. Mungu amekuwa akitenda kazi na kufanya miujiza mara nyingi ila kwa sababu we take most of things for granted, tunashindwa kuyaona au kuyashuhudia kama alivyofanya Babu na tunaishia kufikiri pengine mambo yanatokea kwa uwezo wetu tu.
Babu angeweza kusema amefanya 'utafiti' wake na amegundua dawa/tiba ya hayo magojwa anayodai kuyatibu (hata kama kiukweli hakufanya utafiti huo, bali 'ameoteshwa tu' dawa hiyo!). Kama kweli inatibu (say HIV), angeweza kucharge mamilioni na kwa tabu ya gonjwa hili, tungezitoa tu bila maswali - maana zinatibu.
Shida imekuja kwa yeye kukiri hadharani kuwa dawa hiyo haitokani na uwezo wake bali ameoteshwa tu (ametoa ushuhuda!) - ni kama amekataa ku-claim credits kwa jambo ambalo halifanyi kwa uwezo wake.
Kumbuka pia Mungu amekuwa akiwatumia wataalamu na wanasayansi mbalimbali kutatua matatizo ya kitabibu na mengineyo yaliyowakabli binaadamu - ndui, polio etc lakini katika yote haya (hata kama kwa hakika Mungu aliwaonesha dawa hizo/aliwapa solution wataalamu hao ndotoni) hakuna aliyeweza kumshuhudia Mungu (si wanadhani yamefanyika kwa uwezo wao!).