Mch. Msigwa akabidhi misaada kituo cha islamic center!!

Mch. Msigwa akabidhi misaada kituo cha islamic center!!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
ImageUploadedByJamiiForums1406196824.429427.jpg
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.
ImageUploadedByJamiiForums1406197022.092942.jpg
Baadhi ya misaada iliyotoa mbunge wa Iringa mjini mch. Peter Msigwa kwa kituo cha chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.

MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono Waislamu katika mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi katika mazingira magumu.

Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.

Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi ya shilingi milioni 1.5.

Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.

Akishukuru kwa msaada huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120 ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua watu wake.

"Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza kutoa msaada huu na utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa mjini." Alisema |Chalamila

Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.
 
Katika kuonyesha kuwa Mchungaji Msigwa ni kiongozi HALALI wa wana Iringa anayekubalika, kupendwa, kuheshimiwa na nanaye heshimu na kuwapenda watuy wa Imani zote, amewafuturisha ndugu zetu Waislam ambao sasa wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufuku wa Ramadhani.

Mchungaji Msigwa ameidhihirisha kwa vitendo falsafa ya Chadema ya NGUVU YA UMMA kuwa ni lazima itekelezwe kwa kuunganisha nguvu za watu wote bila kujali rangi, dini, kanda na maeneo wanayotoka.

Asante Mchungaji Msigwa, Asante Chadema, Asante wana Iringa kwa kuendelea kuiamini CHADEMA, Asanteni kwa kuendelea kuimheshimu na kumpenda mpambanaji wenu Mchungani Msigwa

CC: kamandamakini

12189_707548255959157_3684430165731013944_n.jpg



10563081_707548289292487_7800131234127173521_n.jpg



10517575_707548322625817_330202302262129030_n.jpg


10570472_707548382625811_3642002134432325074_n.jpg



10523989_707548425959140_4317209202998313765_n.jpg


10574527_707548475959135_6678316817627699964_n.jpg


10583855_707548512625798_514225903316440853_n.jpg
 
Last edited by a moderator:
sijakuelewa mkuu, amewafuturisha ili waendelee kuiamini CHADEMA?
 
Katika kuonyesha kuwa Mchungaji Msigwa ni kiongozi HALALI wa wana Iringa anayekubalika, kupendwa, kuheshimiwa na nanaye heshimu na kuwapenda watuy wa Imani zote, amewafuturisha ndugu zetu Waislam ambao sasa wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufuku wa Ramadhani.

Kwenye hiyo picha kuna mwislamu hapo? Naona watu waliovaa bargashia na kanzu tu?.Mkristo kafuturisha waislamu mkristo hapo yuko wapi mbona naona mtu kavaa tishet tu ya CHADEMA? Mbona Sioni futari wala mwislamu hapo kwenye picha? AU MACHO YANGU?
 
Safi sana kamanda Msigwa.
Endelea kuwaunganisha watanzania wote bila kujali imani zao. Umekuwa ni kiongozi wa mfano. Umetupa Heshma wana Chadema wenzio. Upendo uliouonyesha sio wa kawaida. Ubarikiwe sana Mheshimiwa Mchungaji Msihgwa.

10530792_706802242700425_3573694080029074469_n.jpg
 
Kwenye hiyo picha kuna mwislamu hapo? Naona watu waliovaa bargashia na kanzu tu?.Mkristo kafuturisha waislamu mkristo hapo yuko wapi mbona naona mtu kavaa tishet tu ya CHADEMA? Mbona Sioni futari wala mwislamu hapo kwenye picha? AU MACHO YANGU?
Sio jukumu langu kujua kuna Muislam au hakuna muislam kwenye hiyo picha. Ninachojua ni kuwa Mchungaji Msigwa ameonyesha kwa vitendo dhana ya upendo kwa watu wote inayohubiriwa na CHADEMA kila siku. Suala la kipimo cha nani muislam sana, nani muislam nusu, nani ni muislam-kafiri hiyo tunawaachia nyie mliona mawazo ya kidini ya kipumba.vu
 
Kwani kutoa msaada nako ni kufuturisha?

Itategemea na unavyotafsiri. Kwetu sisi tunaojifunza kutokana na matendo mema ya viongozi wetu wema kama Msigwa, tunaamini kuwa MSIGWA na CHADEMA wanahimiza na kutekeleza DHANA YA UPENDO kwa vitendo
 
Sio jukumu langu kujua kuna Muislam au hakuna muislam kwenye hiyo picha. Ninachojua ni kuwa Mchungaji Msigwa ameonyesha kwa vitendo dhana ya upendo kwa watu wote inayohubiriwa na CHADEMA kila siku. Suala la kipimo cha nani muislam sana, nani muislam nusu, nani ni muislam-kafiri hiyo tunawaachia nyie mliona mawazo ya kidini ya kipumba.vu[/QUOTE


Mkuu umemjibu vizuri Sana.Unajua Ccm walishazoea kupima watu kwa Masaburi,ndio tatizo ukiishi kwa kutegemea Ulozi hauoni thamani yawengine
 
Nakala THE BIG SHOW ha ha ha ha ha ha ha najua utasema hii ni photoshop ha ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
nikikumbuka maneno ya huyo jamaa sidhani kama kuna la maana. sema tu uchaguzi umekaribia, basi. mengine hayo tuache tu yapite.

Safi sana kamanda Msigwa.
Endelea kuwaunganisha watanzania wote bila kujali imani zao. Umekuwa ni kiongozi wa mfano. Umetupa Heshma wana Chadema wenzio. Upendo uliouonyesha sio wa kawaida. Ubarikiwe sana Mheshimiwa Mchungaji Msihgwa.

10530792_706802242700425_3573694080029074469_n.jpg
 
12189_707548255959157_3684430165731013944_n.jpg
10563081_707548289292487_7800131234127173521_n.jpg


Ukiachia mbali kwamba Msigwa ni mchungaji, lakini pia ni mbunge wa wote. Hapa Kamanda Msigwa akitoa Futari kwa waumini wa dini ya kiislamu walio katika mfungo wa Ramadhan.
 
Back
Top Bottom