Hadithi ya Mch. Msigwa na mithali ya "Hasira, hasara"

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
703
Reaction score
1,143
Kwakuwa leo ninamuongelea Mch. Msigwa ningependa nianze na fungu la biblia kutoka waraka wa Yakobo 1:20 usemao "Hasira ya mwanadamu haitendi haki"

Moja ya mambo yaliyoharibu maisha ya watu wengi ni kufanya maamuzi ukiwa katika hali ya hasira. Bila shaka huu ndio msingi wa wa methali ya "hasira, hasara"

Mch. Msigwa alijipambanua kama mwanamageuzi, nguli wa siasa za upinzani na bila shaka mmoja wa wabunge machachari wa CHADEMA na UKAWA.

Kama kuna watu ambo hawakudhaniwa kuwa siku moja wangeihama CHADEMA, nadhani mmoja wao alikuwa ni Mch. Msigwa. Pengine hii ilitokana na taarifa kuwa Rais Magufuli mwenyewe alishamtaka Mch. Msigwa ajiunge na CCM kwa ahadi ya ubunge na jamaa akachomoa!

Katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kinyang'anyiro cha uenyekiti wa kanda ya nyasa, ambapo mchungaji aliangushwa na Sugu, watanzania walishuhudia jambo ambalo hawakulitegemea, nalo ni Mch. Msigwa kuhamia CCM kwa madai kuwa Mbowe alimhujumu ili amuweke Sugu badala yake.

Kuhama kwa Mch. Msigwa kulivuta hisia za wengi. Itakumbukwa Lema alitoa maoni yake kuwa Mch. Msigwa amehama kwasababu ya kuhujumiwa na Mbowe, hata Lisu pia alikiri Mch. Msigwa alikuwa rafiki yake, kama ilivyokuwa kwa wana CHADEMA wengine wengi.

Baada ya tukio lile Mch. Msigwa alianza rasmi kufanya siasa za chama cha mapinduzi na siraha yake kubwa ikawa ni kuiponda CHADEMA na sera yao ya "No reforms, No election"

Hata hivyo safari yake haikumpa matokeo aliyoyatarajia. Kwani aligombea uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini bila mafanikio. Na bila shaka amesubiri uteuzi, na mwishowe amekata tamaa.

Sasa Mch. Msigwa ametangaza amerudi CHADEMA kwa kisingizio cha October 29. Hili ni jambo linalochekesha sana kwani ni wazi Mch. Msigwa alikimbia CHADEMA kwa kuukosa uenyekiti wa kanda ya Nyasa, na sasa anakimbia CCM kwakuukosa ubunge wa Iringa mjini pamoja na uteuzi.

Ipo hadithi katika vitabu vya kiada vya elimu ya msingi iliyomuhusu fisi aliyetaka kuhudhuria sherehe mbili kwa wakati mmoja na mwisho akakosa kote. Hadithi ile ni kama ilikuwa ikitabiri haya yaliyomkuta Mch Msigwa.

Kwa ujumla Mch. Msigwa amejishushia heshma yake sana. Hawezi kuaminika tena kama zamani. Sasa hivi ameshawapa adui zake sababu zenye nguvu za kumdogodesha kila atakapofungua mdomo wake.

Kwa vijana tunaoanza siasa tunalakujifunza kutoka kwenye kisa cha Mch. Msigwa. Wahenga walituasa, mvumilivu hula mbivu!
 
In politics, this ain’t unusual. Historically, a lot of mazafakas (e.g., Wasira, Makongoro, Lowassa, Sumaye) have walked this path!
 
Bado atapewa uongozi aje atudanganye wananchi. Daa ! ila siasa ni kama uchawi wa mazingaombwe...Huyo bwana TAMAA MBELE AND THE TWO FEASTS hafai kupewa hata ubalozi wa nyumba kumi.
 
In politics, this ain’t unusual. Historically, a lot of mazafakas (e.g., Wasira, Makongoro, Lowassa, Sumaye) have walked this path!
Ukishakuwa na historia ya kutokuaminika, ukihama watakupokea, ila daima watakutilia mashaka. Itachukua muda kuirudisha hiyo imani.
 
Kwakuwa leo ninamuongelea Mch. Msigwa ningependa nianze na fungu la biblia kutoka waraka wa Yakobo 1:20 usemao "Hasira ya mwanadamu haitendi haki"

uvu za kumdogodesha kila atakapofungua mdomo wake.

Kwa vijana tunaoanza siasa tunalakujifunza kutoka kwenye kisa cha Mch. Msigwa. Wahenga walituasa, mvumilivu hula mbivu!
Mkuu na wewe ni kijana?
 
Ebu soma UNESCO na WHO uniambie unakuwaje Kijana, unashangaa watu wanawaita akina Mwigulu and likes vijana.
Kubali kuwa wewe ni Mzee
Hapa kwetu ki CCM, CCM, kijana mwisho miaka 40!
 
Kwakuwa leo ninamuongelea Mch. Msigwa ningependa nianze na fungu la biblia kutoka waraka wa Yakobo 1:20 usemao "Hasira ya mwanadamu haitendi haki"

Moja ya mambo yaliyoharibu maisha ya watu wengi ni kufanya maamuzi ukiwa katika hali ya hasira. Bila shaka huu ndio msingi wa wa methali ya "hasira, hasara"

Mch. Msigwa alijipambanua kama mwanamageuzi, nguli wa siasa za upinzani na bila shaka mmoja wa wabunge machachari wa CHADEMA na UKAWA.

Kama kuna watu ambo hawakudhaniwa kuwa siku moja wangeihama CHADEMA, nadhani mmoja wao alikuwa ni Mch. Msigwa. Pengine hii ilitokana na taarifa kuwa Rais Magufuli mwenyewe alishamtaka Mch. Msigwa ajiunge na CCM kwa ahadi ya ubunge na jamaa akachomoa!

Katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kinyang'anyiro cha uenyekiti wa kanda ya nyasa, ambapo mchungaji aliangushwa na Sugu, watanzania walishuhudia jambo ambalo hawakulitegemea, nalo ni Mch. Msigwa kuhamia CCM kwa madai kuwa Mbowe alimhujumu ili amuweke Sugu badala yake.

Kuhama kwa Mch. Msigwa kulivuta hisia za wengi. Itakumbukwa Lema alitoa maoni yake kuwa Mch. Msigwa amehama kwasababu ya kuhujumiwa na Mbowe, hata Lisu pia alikiri Mch. Msigwa alikuwa rafiki yake, kama ilivyokuwa kwa wana CHADEMA wengine wengi.

Baada ya tukio lile Mch. Msigwa alianza rasmi kufanya siasa za chama cha mapinduzi na siraha yake kubwa ikawa ni kuiponda CHADEMA na sera yao ya "No reforms, No election"

Hata hivyo safari yake haikumpa matokeo aliyoyatarajia. Kwani aligombea uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini bila mafanikio. Na bila shaka amesubiri uteuzi, na mwishowe amekata tamaa.

Sasa Mch. Msigwa ametangaza amerudi CHADEMA kwa kisingizio cha October 29. Hili ni jambo linalochekesha sana kwani ni wazi Mch. Msigwa alikimbia CHADEMA kwa kuukosa uenyekiti wa kanda ya Nyasa, na sasa anakimbia CCM kwakuukosa ubunge wa Iringa mjini pamoja na uteuzi.

Ipo hadithi katika vitabu vya kiada vya elimu ya msingi iliyomuhusu fisi aliyetaka kuhudhuria sherehe mbili kwa wakati mmoja na mwisho akakosa kote. Hadithi ile ni kama ilikuwa ikitabiri haya yaliyomkuta Mch Msigwa.

Kwa ujumla Mch. Msigwa amejishushia heshma yake sana. Hawezi kuaminika tena kama zamani. Sasa hivi ameshawapa adui zake sababu zenye nguvu za kumdogodesha kila atakapofungua mdomo wake.

Kwa vijana tunaoanza siasa tunalakujifunza kutoka kwenye kisa cha Mch. Msigwa. Wahenga walituasa, mvumilivu hula mbivu!
📌🔨...🤝%💯
 
Ukishakuwa na historia ya kutokuaminika, ukihama watakupokea, ila daima watakutilia mashaka. Itachukua muda kuirudisha hiyo imani.
Hata kwenye biashara ukila mtaji lazima ujenge upya. Hapa napo political capital restoration efforts zinahitajika.
 
Back
Top Bottom